Tamko la kamati kuu ya CHADEMA kuhusu mchakato wa katiba

Jamaa unajaza maneno yako ndani ya midomo ya wenzio. Dha! unaakili kama ya Intarahamwe.
 
Mdau nakushukuru,nimekisoma hicho kipengele na kukielewa vema.Na kwangu nadhani hoja kubwa iko hapa,nanukuu"5. Kamati Kuu inaamini kuwa pamoja na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa, bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja, nia, mchakato na misingi ya Katiba Mpya." mwisho wa kunukuu. Kimsingi sina tatizo na hoja hii. Lakini binafsi nilidhani kwamba ingekuwa jambo la busara zaidi kama Kamati kuu ya CDM ingekuja kwanza na azimio hilo la kutaka kukutana na JK kabla ya kuutangazia umma maazimio haya. Maana hii sentensi niliyoinukuu inajiielekeza huko.Baada ya kukutana na Rais Kikwete ndipo sasa,kamati kuu ya CDM ndipo ingekuja na maazimio yao.Hapo binafsi naamini ingekuwa imekaa vema.Maana sasa ninachokiona hapa ni kwamba maazimio ni mazito yakimlenga moja kwa moja Rais JK. Sasa unapotaka kukutana na mtu huyo huyo baada ya kuwa umeshamsema,mmm kidogo inaleta shida.Sina tatizo na wazo la CDM kukutana na Rais.Lakini approach ndio inanisumbua.

chadema wameweza kuwa wazi kueleza yale watakayomshauri mkuu,ili nae mkuu ajiandae na hayo mapendekezo yao. Ila kwa watu wanafki ni ngumu kuelewa hii approach..hizi issue ni kwa maslahi ya taifa,tufichane ya nini?? issue sio kusema kabla, Lol
 
Ni tamko zuri sana, lakini tusiliangalie kisiasa na wala kishabiki. tuliangalie kwa maslahi ya taifa na nyuma ya pazia ya objective za CDM, CCM, Makumdi ya CCM na watu wanaofadhili makundi ya CCM na nyuma ya pazia ya objectives za CDM katika mustakabali wa taifa hili. Hili ni tamko jepesi sana kuliandika na kulishabikia kimaslahi, lakini ukiangalia kwa makini ni tamko gumu kwa vizazi vyetu vijavyo vya Tanzania kama taifa. Bwana Pascal ktk thread moja ambayo ipo na bado ni hot kuendelea kuchangiwa, amewakosoa CDM kuwa walichemka kutoka bungeni, na hakatai kuwa walikuwa na pointi za msingi. walichofanya CDM ni sawa na opponents wa Liberia. Kwa kifupi CDM wametangaza serikali yao nje ya mfumo rasmi, na kwa hili tusitegemee chochote chema kwa taifa letu zaidi ya vurugu za umwagaji damu. hii ni kwakuwa, iliyopitishwa naitakayosainiwa kwa mbwembwe na mtukufu raisi, ndiyo sheria, na inabaraka zaidi ya nusu nusu ya wabunge wa upinzani, forget about kambi rasmi ya upinzani(Hawajiamini hawa jamaa, na ndiyo maana wanajiita kambi rasmi). CDM ni wapotoshaji, na huitaji kuwa na PHd ya phychology kujua hawa jamaa ni wapotoshaji na waongo.

Mkuu Kiminyio, katika jukwaa kama hili la watu walioenda shule huwezi kusema CDM ni wapotoshaji halafu ukaishia hapo. Watu watakudharau. Ainisha mambo in point form ni mambo gani wamepotosha na kivipi wamepotosha.

Kama huna tulia tu kama unanyolewa.
 
Ikiwa hilo ndiyo tamko la magwanda, ama kweli mna "wasomi" na si wasomi. Hivi kama chama cha upinzani mmekaa haswa mkachemsha vichwa vyenu mkaja na tamko kama hilo? nashindwa kuamini nnayoyasoma kuwa yanatoka kwenye "wasomi". Khaaaa!

Nna uhakika hayo kayaandika Mbowe.

Zitto uko wapi? tazama hawa wenzako wanavyokitia aibu chama ulichokipagania mpaka kwa afya yako. Pole sana Zitto najuwa una kazi kubwa sana, Mwenyeezi Mungu atakulinda na kukusaidia. Sikuwepo kwenye hicho kikao wala sijasikia zaidi ya hayo niliyoyasoma hapo juu, lakini nna uhakika hukutia hata lako moja. Hii si "calibre" yako.

Crap !!!!!!.......
 
Mkweche umesema kweli kuwa JK ni rais wa Tanzania hadi 2011. Lakini napingana nawe kuwa JK alichaguliwa na watanzania; Kiuhalisia JK alichaguliwa na watanzania takribani 5,000,000 baada ya mahesabu ya kura kuchakachuliwa na NEC. Najua unafahamu kuwa nchi yetu ina watu zaidi ya 46,000,000, na idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura ilikuwa ni about 21,000,000. Hii inadhihirisha kuwa zaidi ya wapiga kura 15,000,000(76.2%) hawakumchagua JK. Ni katiba mbovu ndiyo inayohalalisha watu wengi kuchaguliwa rais na wachache. Rais wa namna hii hana Legitimacy ya kutawala Watanzania walio wengi. Ndio maana kila kona ya nchi hii kuna malalamiko kuhusu uongozi mbovu unalisababishia taifa hili matatizo mengi kama vile njaa(pamoja na kilimo kwanza), mfumuko wa bei, utawala kandamizi wa kutumia jeshi la polisi dhidi wananchi wanaodai haki zao za msingi, ufisadi uliokithiri nk.

Rais wa namna hii ataendelea kutumia nguvu ya dola na uwingi wa wabunge wa chama chake kutunga sheria ambazo wananchi wengi hawakubaliani nazo. Mswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba hauna maslahi kwa watanzania ndio maana umepingwa na watu walio wengi. CCM na wabunge wake walipaswa kusikiliza maoni ya wanachi kabla ya kupitisha msawada ule. CDM walifanya sahihi kukataa kushiriki kupitisha mswada uliolazimishwa kusomwa mara ya pili kwa lengo la kuwanyima wananchi uhuru wa kutoa maoni yao. CCM walijua wangeruhusu wananchi kutoa maoni yao, mswada ule ukipingwa na usingepita. Hivyo Wabunge wa CCM na spika wao aliyewekwa na mafisadi(kwa mujibu wa Samweli Sitta) wakatumia wingi wao badala ya hoja kupitisha mswada ule.

Kwa mtazamo wangu JK na CCM hawana dhamira ya dhati ya kuwawezesha watanzania kupata katiba mpya itayokidhi mahitaji ya watanzania; wanachofanya(CCM) ni kuhakikisha inapatikana katiba itakayolinda maslahi ya chama chao na mafisadi ili waendelee kutawala kwa mabavu. Kamwe kwa utaratibu huu haitapatikana katiba bora.
Ndugu yangu upo sahihi KABISAA!
Shaka yangu ni kumfata mtu ambaye system yake ipo Kazini!sidhani kama ya Bungena yatatofautiana na atakayosema!Vinginevo ni bora kukiri yeye ndio Last Say katika hili
 
Nimepitia tena tamko la Chadema kuhusiana na mapungufu katika mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya. Ki msingi, kuna maoni mengi waliyoyatoa baadhi nakubaliana nayo na mengine aidha sikubaliani nayo au sijayaelewa vizuri. Kwa hili, nitafurahi kama wasomaji wenzangu watanielimisha au kunikosoa pale nitakapokuwa sijaelewa vizuri.

1. Kuhusiana na uamuzi wa kususia mjadala wa Bunge siwezi kusema kama walikuwa sahihi ama walikosea. Ila kwa mtizamo wangu binafsi ningetofautiana nao. Ningeonelea kwamba hoja zilizoandikwa katika Tamko lao juu ya mapungufu pamoja na hoja nyingine wanazoziona mhimu wangeweza kuzijadili ndani ya Bunge. Hilo lingeweza kuwaathiri baadhi ya wabunge wa CCM na vyama vingine na pengine wangeweza kuamua vinginevyo. Kuna masuala mengi Bungeni dhidi ya chama tawala na mengine yaliyoanzishwa na wabunge wa Chadema yaliyoweza kupita kwa namna hiyo. Sikuona uharaka uliyowafanya watoke nje badala ya kuingia katika mjadala na kuona hatima yake, kama huo mswaada ungepitishwa kama ulivyo au maoni yao yangezingatiwa.

2. Hoja kwamba Mswaada uliosomwa mara ya kwanza na huu uliopitishwa ni tofauti mimi sikubaliani nayo. Nijuavyo mimi, Mswaada ni huo huo baada ya kufanyiwa marekebisho. Hata kama huu wanaouona ni tofauti na wa kwanza ungesomwa mara ya kwanza kama Chadema walivyotaka, bado ule ambao ungesomwa mara ya pili usingekuwa sawa na huu kama ulivyo, maana ungefanyiwa marekebisho kutokana na maoni ambayo yangetolewa. Lakini marekebisho yasingeufanya kuwa mswaada tofauti.

3. Mamlaka ya Raisi kuunda Tume mimi binafsi naona ndio utaratibu wa kawaida. Raisi japo ni Mwenyekiti wa CCM haundi Tume kama Mwenyekiti wa CCM bali kama Raisi. Hata madaraka yake mengine ya kiraisi anayatumia kama ofisi ya Raisi na sio mwenyekiti wa CCM au baba wa familia ya mzee Kikwete. Sijui ndugu zangu wa Chadema wangependa mamlaka hayo apewe nani sasa. Ukisema lipewe Bunge ndio hilo hilo tunalilalamikia kwamba ni la CCM. Ukiondoa Bunge tunabaki na Mahakama na Serikali sijui nani kati ya hawa wapewe mamlaka ya kuunda hiyo Tume na kwa mjibu wa sheria gani.

4.Mamlaka ya raisi kurekebisha ripoti ya Tume kama Mswaada umekusuduia hivyo siafikiani nayo na hivyo nawaunga mkono Chadema. Kwa mujibu wa Mswada Tume itakayoundwa ni huru. Haipaswi kuingiliwa katika kazi yake pamoja na ripoti itakayotoa ili mradi tu iwe ni kwa mjibu wa sheria.

5. Kwamba Raisi naweza kuitisha Bunge la Katiba kupitisha Katiba nyingine kama hajaridhika na Mswaada wa Katiba, mimi kwa kadili nilivyoipitia Bill sikuona sehemu yoyote inayompa Raisi mamlaka kama hayo. Kwa hili naomba yeyote aliyeona kifungu hicho tueleweshane. Nijuavyo mimi, wenye mamlaka ya kupitisha mswaada wa Katiba kwa mara ya kwanza ni Bunge la Katiba. Wenye mamlaka ya mwisho kuifanya hiyo katiba ipate nguvu za kisheria ni wananchi kupitia Referandum. Mamlaka ya Raisi ni kutangaza tarehe ambayo hiyo Katiba itakuwa operational (itaanza kufanya kazi). Wananchi kupitia Referandum kama watakataa kwa wingi kuipitisha Katiba mpya, sheria inasema, katiba ya zamani itaendelea kutumika.

6. Kwamba Bunge la Katiba linaundwa na wabunge wengi kutoka CCM mimi suioni kama ni tatizo sana katika kipindi hiki ambacho hata Bunge la kawaida linawajumbe wengi kutoka CCM. Maana, hao wabunge wengi toka CCM wanatokana na utashi wa watu kutokana na uchaguzi uliopita katika kipindi kifupi kilichopita. Wanawakilisha watu wengi nyuma yao na wengine wakiwa sio CCM. Ndio maana wameweza kuunga mkono mamabo mengi katika Bunge ambayo kama wangeangalia maslahi ya kichama tu wasingeweza. Najua Chadema wangependa wajumbe wengi zaidi watoke kwenye chama chao na vyama vingine vya upinzani. Lakini suala hapa ni wapi uhalali wa wao kuwemo kwa wingi katika Bunge hilo unatokana? Kwa maoni yangu kwa kufanya hivyo tunakuwa tunawanyima haki wananchi wengi ambao 2010 walitaka wawakilishwa na wabunge wengi wa CCM.
 
Ndugu yangu upo sahihi KABISAA!
Shaka yangu ni kumfata mtu ambaye system yake ipo Kazini!sidhani kama ya Bungena yatatofautiana na atakayosema!Vinginevo ni bora kukiri yeye ndio Last Say katika hili

Du! Hapa mmezuai suala gumu sana kifalsafa. Ni kweli idadi ya watanzania ni zaidi ya milioni 40 na waliopiga kura ni sehemu ndogo ya asilimia ya watu waliostahili kupiga kura. Ni kweli katika watanzania milion 40 kuna watoto na wengine wasio na sifa ya kupiga kura kutokana na kwamba si watanzania, lakini bado hilo halifuti ukweli kwamba watanzania wengi hawakupiga kura. Suala gumu la kutatua ni tuna uhakika gani kama watanzania wengi hawakubaliani na utaratibu huu tunaoenda nao wa kuandika katiba mpya? Tunaweza kuwa na ushahidi gani mkubwa na wa kuaminika zaidi ya kwamba CCM inapendwa au haipendwi na watu wengi zaidi ya matokeo ya uchaguzi uliopita? Utaratibu wa kupiga kura Tanzania kwa mtizamo wangu haukuzuia moja kwa moja idadi ya watanzania wanaostahili kupiga kura kujiandikisha na kupiga kura za ndio na sio kwa watu wanaowataka na wasiowataka. Hoja ambayo wengine wanaweza kuijenga ni kwamba labda tu mfumo ungeweza kuruhusu uchakachuaji wa matokeo. Lakini suala la kujiuliza, CCM imepata zaidi ya asilimia sabini za wabunge wote. Sheria inaruhusu mtu asiyeridhika na matokeo ya uchaguzi wa Bunge kuyapinga mahakamani. Ni asilimia chache sana ya matokeo ya ubunge yamepingwa.

Lakini hata tukisema bunge lilipo kwa sasa haliwakilishi matakwa halisi ya watanzania, bado mfumo tuliyowekewa wa kuitafuta katiba mpya unatoa nafasi kubwa na ya juu zaidi kwa wananchi wenyewe. Wanayo nafasi ya mwisho ya kupiga kura kama wataitaka au hawataitaka hiyo katiba itakayotungwa. KIgezo kikubwa kwa maoni yangu, itakuwa ni kama yaliyomo katika hiyo katiba mpya yanareflect maoni na matakwa yao kama walivyoyatoa katika hatua mbalimbali za mijadala ya kuwa na Katiba mpya.

Labda tuitishe uchaguzi wa Bunge la Katiba ambalo ndio litajadili na kupitisha Katiba mpya. Issue itabaki vile vile kama watu wengi wataipigia CCM au chama kingine cha siasa. Lakini pia mtu anaweza kusema kwamba kati ya watanzania zaidi ya milioni 40 waliyomo katika vyama vya siasa ni chini ya milioni 5 ndio wanavyama wa siasa. Sasa hilo nalo tunalitibu vipi? Itabidi tuanze kwanza kurekebisha sheria zilizopo na Katiba alafu suala la Katiba mpya liwe baadae?. Turekebishe sheria za uchaguzi na katiba kuweka uhuru zaidi na uwepo wa wagombea binafsi. Hayo huko nyuma yalikuwa ndio maoni ya baadhi yetu nikiwemo mimi. Lakini wananchi kwa kigezo cha sauiti ya wanasiasa wenye nafasi ya kuweza kuvitumia vizuri vyombo vya habari walihalalisha uharaka wa kuwepo Katiba mpya. Wengine walitaka iwe ndani ya siku mia moja baada ya uchaguzi Mkuu uliopita. Kwa maana nyingine Katiba mpya ilipaswa kuwa tayari mwezi wa tatu mwaka huu. Ni kwa sababu hiyo ndio mana hapakuwa na umhimu wa kupata maoni ya awali ya wananchi kama wanataka katiba mpya au wanataka kuendelea na hii tuliyonayo. Maneno ya wanasiasa wachache yakikuzwa na vyombo vya habari yalichukuliwa kama ndio sauti ya wananchi wengi. Na huko ndiko tunakoelekea sasa. Kuna haja watanzania tukajifunza katika hili.
 
Back
Top Bottom