Tamko la CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto

Tamko la CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto

Mkuu,

Umeenda hospitali ya amana kuna nesi mmoja nimesikia alitaka kudai hela eti dawa hakuna anasahau watanzania hawa wanalipa kodi zinazoilipa hospitali ya amana nasikia watu karibu wampige. Sasa serikali iwe na emergency plan ya pesa kama vitu vya kula, nauli na dawa. Mie tangu lianze hilo zahama jana usiku hadi sasa nimeshatumia pesa nyingi sana kwa ndugu jamaa na majirani maana kuna watu hata kadi za benki wameacha nyumbani. Vilevile huko majumbani kumeibiwa hakutamaniki sasa usiseme hela haina faida ni muhimu sana mkuu.

Pili kumfukuza mtu wakati hatujajua kosa sio sahihi ninavyoona mie. Kuna mtu amesema ni uwajibikaji lakini uwajibika wakati hujajua kama kuna makosa au uzembe umefanyika ni sahihi?. Hatujajua nini kimetokea mbagala tunakimbilia kuwaambia jamaa wajiuzulu niwaulize wajiuzulu kwa lipi??? Pia ikija ikagundulika akina Dr Hussein Mwinyi walifanya kazi yao ila ukata umesababisha hizo solution kutekelezeka mtasemaje? Au pengine zilitekelezwa but kuna watu wanafanya hujuma kuleta hofu nchini mtasemaje?? Bado sikubaliani nanyi kwa hilo I am very sorry.
Ni vigumu kujadiliana na watu wenye matatizo ya kuelewa mantiki pamoja na kanuni za uwajibikaji wa mawaziri. Naomba ndugu yangu ukajielimishe kanuni hizo na ndipo utaweza kutoa mchango chanya. Vilevile inaelekea wewe ni mtu asiyekubali kuwajibika kwa lolote lile kwani yote yanayotokea yamepangwa na hivyo mwanadamu hana cha kufanya!
 
Kwa chadema this is supposed to be a blessing in desguise. Wasipotumia hii nafasi kuongoza ukombozi wa nchi hii wamepoteza credibility yao. They are not fulfilling the People's expectations.

This is the day, the time, the only. Chadema please act

we will see and evaluate them soon!

halafu nyie cdm acheni kuingiza siasa kwenye issue siriaz, tunazungumzia vifo nyie mnafikiria kujiuzulu. ebu onyesheni kujali kwenu kwa wahathirika kwa vitendo, mfn ningesikia cdm wabunge au chama wametoa milioni kazaa kama pole, mnabaki kelele tu huku mnamun'gunya mamilioni ya posho na ruzuku ya uchaguzi. tuache siasa kwenye mambo ya ukweli tuishauli serikali kipi cha kufanya kwa sasa,

People like you are the reason why we have middle fingers! you better watch porno than sending this comment
 
Ni vigumu kujadiliana na watu wenye matatizo ya kuelewa mantiki pamoja na kanuni za uwajibikaji wa mawaziri. Naomba ndugu yangu ukajielimishe kanuni hizo na ndipo utaweza kutoa mchango chanya. Vilevile inaelekea wewe ni mtu asiyekubali kuwajibika kwa lolote lile kwani yote yanayotokea yamepangwa na hivyo mwanadamu hana cha kufanya!

Na vilevile ni vigumu kuwaelewa na kukubaliana na watu wenye kuingiza maslahi yao binafsi kwenye janga kama hili tuacheni na maumivu yetu tutaumia tutapona lakini hatutaki kutolewa kafara ili watu wengine wafaidike kisiasa. Kama mnauzalendo tusaidieni nyie wanachadema kwanza tuone uzalendo wenu na sio kutaka watu wajiuzulu tu bila sababu ya msingi....
 
Hawa wanajeshi wetu nao wameuchoka huu utawala uliooza ndio maana nao wameamua kufanya kweli.

* kuna taarifa za uhakika kuwa wanajeshi walishaanza kuwaonya raia toka mchana kuwa wakae majumbani, wasitoke, na kuwa kuna uwezekano wa milipuko maana ghala ilikuwa inafuka moshi kutokana na hitilafu za umeme kukatwa katwa na kurudi ghafla

* na kama ukweli utafahamika sio ajabu ikawa ni njama na mkondo wa wakubwa kupanga kuzusha hofu kwa wananchi ili wawe waoga kudai haki, kuandamana, na pia kubadili mkondo wa mawazo kuhusu kashfa na wizi wa dowans.

tuyatafakari na kufuatilia zaidi, nilifika hadi kambini mwisho-wa-lami, na wananchi wana hasira kila kona, wanasema hii ni jibu la taifa 'kutokuwa na serikali ya wananchi' maana waliokufa mbagala hawakuwagusa kifikra na maumivu viongozi ambao ndio hao hao wameacha ya sasa kutukia nao hawana majibu.
 
Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.
Ndugu yangu vipi mbona sikuelewi hivi usichoelewa ni 'kuwajibika kisiasa?' hawa viongozi walikuwepo wakati wa mabomu ya mbagara na wakaahidi jambo hili likijirudia watajiuzuru, sasa kuwakumbusha walichoahidi kuna ubaya gani? Au na wewe ni akina 'Chukua Chako Mapema?'
 
Tatizo lenu mna yenu na sio huruma za kizalendo hapo kwenye nyekundu ndio kunadhihirisha upungufu wa point yako. Hii kitu ilijulikana tatizo liko wapi nalo ni uzembe. Hembu nikuulize wewe unajua kilicholipua mabomu gongo la mboto, mbagala???? Sasa kama hujui kwanini ung'aka watu wajiuzulu???
Kilichosababisha hayo ni uzembe wa kuweka mabomu hayo katika sehemu za watu na kutoyatunza vizuri kuhakikisha hayalipuki. Hivi huu ubishi wa kimshipa unatoka wapi? Inabidi ukapimwe kuondoa unduli katika fikra zako.
 
mi ningefurahi if chadema wange chukua dola haya yote ya singe tupata, cz kila cku bora ya jana, huu ni mwezi wa pili bt maafa kama tume kaa miaka 20, ccm tumewachoka hamnajipya zaidi ya ufisadi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kilichosababisha hayo ni uzembe wa kuweka mabomu hayo katika sehemu za watu na kutoyatunza vizuri kuhakikisha hayalipuki. Hivi huu ubishi wa kimshipa unatoka wapi? Inabidi ukapimwe kuondoa unduli katika fikra zako.

Hivi kuna uchunguzi umefanyika kuonyesha uzembe ulifanyika? Tatizo lenu mna ajenda zenu za kisiasa zaidi kuliko hali halisi. Na wengine hatuwezi kukubaliana nanyie kijinga jinga tu. Mkishapata lenu mnapanda MVX mnaacha wananchi na simanzi tu hadanganyiki mtu wakuu. Nauliza tena ulifanyika uchunguzi ikajulikana uzembe??? Je ikija kuwa bahati mbaya, ukata utasemaje???
 
Nadhani ninazungumza na mtu mwenye utapiakili huu ni uzembe na wao watu wa Jeshi wanasema eti siku tatu zilizopita walifanya ukaguzi sasa kama walifanya ukaguzi wakashindwa kugundua kasoro zozote na baada ya siku tatu mabomu yanalipuka hiyo haikuonyeshi kuwa tuna wataalamu uchwara na kuwa huo ukaguzi ulikuwa ni wa bandia?

Kitu kilicho wazi ni kuwa maisha ya Watanzania wetu halali yamepotea kutokana na uzembe huo na hatuwezi kuwa taifa linakubali maisha ya wenzetu yapotee eti kwa "bahati mbaya." Hatuwezi kuongozwa na watu ambao wanaamini kuwa maisha na kufa kwa Watanzania ni bahati mbaya.
 
Nilikuwapo!!! ila nakuacha na maswali haya jiulize:-
a. Hata kama wamefanya ukaguzi siku tatu zilizopita huoni kuwa tatizo sio viongozi ni kwamba either hatuna wataalamu wa kutosha jeshini au ukapa wa vifaa na fedha nao umechangia.

b. Unaposema uzembe unaujua uzembe ndugu?? Ajali ya MV Bukoba ndio mfano wa uzembe kwamaana jambo lilijulikana muda mrefu likaachwa tu mwishoe yakatokea maafa. Sasa huo uzembe maana report zipo, taarifa zikatolewa na wataalamu mwishoe maafa yakatokea katika hili hatuna taarifa za kitaalamu, report yeyote tunakimbilia uzembe je nikuulize kuna report yeyote inayosema lolote?

c. Umedai mimi nina utapiaakili but nikuulize wewe mwenye akili je nipe sababu moja ya msingi ya kuandamana na kuwataka viongozi wajiuzulu?

Kwaheri katika thread ninajitoa.
 
Nikiongea nitarudia ya kwako!uko sawa MKUU,humu propaganda tu mpaka Blog nzima ya JF imegeuka CHADEMA.Acheni porojo za U-CCM na U-CHADEMA tunaumizwa sana na kufariki/kujeruiwa kwa wenzetu tunaomba serikali ikabiliane na yaliyojiri kisha tujadili kulingana na uchunguzi wa tukio.Hapa watakaobainika kama ni uzembe wa JWTZ ama GVT ni wakati wa kuchukua hatua.

Multiple IDs ni ishara ya ujinga, tafakari chukua hatua.
 
Jamani hili la ajali lichukuliwe kwa uzito wake na si kwa ushabiki wa kisiasa...kiungwana nadhani zifanyike juhudi za haraka za kuokoa maisha ya wahanga wa tukio hili na zichukuliwe hatua za haraka kuhakikisha hakuna maafa zaidi baadaye...na baadaya hali kuwa shwari mamlaka husika zijipime kama kuna uzembe wowote katika hili uwajibikaji uwepo!

laiti kama ingekuwa ni mara ya kwanza kutokea at least watu wasingesema sana. juzi tu 2009 april jana tena? CDM ndo serikali mbadala lzm itoe tamko. ndo ukomavu huo. there is no news like bad news.
 
Kiongozi huajibika kwa makosa ya wadogo zake. Wanajeshi wakiweka vibaya makombora yakaumiza watu, anaajibika CDF. Na kisiasa anaajibika Waziri wa Ulinzi.

Ni kweli maofisa wakuu wa JWTZ hupendelea kukaa Oyster Bay na Masaki. Hilo halina tatizo. Lakini ni lazima wakae karibu na mabomu yao? Si wanaotoa tu amri na bomu linarushwa toka kokote lilipo? Au waangalizi wa kila siku wa hayo mabomu nao ni lazima wakae mjini?

WAZIRI WA Ulinzi na CDF wanapashwa kujiuzulu hata kama waliofanya makosa ni wadogo zao. They are responsible for the actions of their juniors.

Kuna wanaosema tatizo ni kukosa fedha. Sasa mbona wanazo fedha za kununulia magari ya kifahari hivyo? Kwani hatuoni magari mapya wanayotumia? Kama wameweka kipaumbele kwenye matumizi ya kifahari badala ya kutumia fedha kuteketeza mabomu chakavu kwanza, basi ni wazembe sana, wajiuzulu haraka.
 
Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.

Mwiba you're hopeless.

CHADEMA ina watu makini kuliko unavyofikiri. Mbona mamako Makinda alikurupuka juzi kumtaka Mhe. Lema kuwasilisha ushahidi wa Pinda kusema uongo Bungeni na badaye kaona aibu kumruhusu GLema kuweka mambo hadharani? CHADEMA kuna VICHWA baali CCM kuna VICHAA tena wa kuokota makopo.

Kama huna cha kusema ni afadhali unyamaze.
 
Nilikuwapo!!! ila nakuacha na maswali haya jiulize:-
a. Hata kama wamefanya ukaguzi siku tatu zilizopita huoni kuwa tatizo sio viongozi ni kwamba either hatuna wataalamu wa kutosha jeshini au ukapa wa vifaa na fedha nao umechangia.

b. Unaposema uzembe unaujua uzembe ndugu?? Ajali ya MV Bukoba ndio mfano wa uzembe kwamaana jambo lilijulikana muda mrefu likaachwa tu mwishoe yakatokea maafa. Sasa huo uzembe maana report zipo, taarifa zikatolewa na wataalamu mwishoe maafa yakatokea katika hili hatuna taarifa za kitaalamu, report yeyote tunakimbilia uzembe je nikuulize kuna report yeyote inayosema lolote?

c. Umedai mimi nina utapiaakili but nikuulize wewe mwenye akili je nipe sababu moja ya msingi ya kuandamana na kuwataka viongozi wajiuzulu?

Kwaheri katika thread ninajitoa.

Mdondoaji, pamoja na kwamba umeaga nimegundua kwamba mko kadhaa wenye multiple IDs kwa hiyo naamini utasoma hii kwa kutumia ID yako nyingine.

Nini kinakupa uthubutu wa kutetea jeshi na viongozi wao wa kisiasa? Unajuaje kama heshi limeishiwa wataalamu wakati wao hawajawahi kulalamika? Unajuaje kama hawana pesa wakati bajeti wao hawajawahi kulalamika hilo. Na je, kukosa wataalamu na pesa ndiyo justification ya kumishandle mabomu na kuua raia? Kwa nini wao hawakufa hata mmoja?
 
MAAFA YA GONGO LA MBOTO: WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI WAJIBIKE!​

TAARIFA KWA UMMA
DODOMA, FEBRUARI 17, 2011

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika Ghala la Kuhifadhi Silaha la Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana jioni.

Aidha, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya maafa haya. Pia Kambi hiyo imezitaka mamlaka zote za umma zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wote walioathirika na maafa haya wanapatiwa huduma zote wanazohitaji katika kipindi hiki cha msiba huu. Hii ni pamoja na kuwapatia huduma za maziko wale wote waliofariki, matibabu kwa waliojeruhiwa na hifadhi kwa wale waliopoteza makazi yao. Aidha, ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha ulinzi wa mali za wananchi katika maeneo yote yaliyoathirika na ambazo zitakuwa hazina ulinzi baada ya wananchi kukimbia maeneo yao.

Taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kwamba tukio hili ni la kushtusha na kusikitisha hasa kwa kuzingatia kwamba haijapita miaka miwili tangu tukio la aina hiyo hiyo litokee katika Ghala ya Silaha ya Kambi nyingine ya JWTZ katika eneo la Mbagala, Dar es Salaam, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini na uharibifu mkubwa wa mali za umma na za wananchi binafsi. Aidha, milipuko ya Mbagala ilipelekea Serikali kutumia mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya malipo ya fidia kutokana na vifo, majeruhi na uharibifu wa mali binafsi za wananchi.

Akielezea tukio la milipuko ya Gongo la Mboto, Msemaji wa Ulinzi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Joseph Selasini alisema: “Milipuko ya Gongo la Mboto inaonyesha dhahiri kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haijajifunza lolote kutokana na maafa yaliyotokea Mbagala mwaka juzi. Maana kama Serikali ingejifunza kutokana na maafa hayo ingeshachukua hatua za dharura na za haraka kuhakikisha kwamba maafa ya aina hii hayatokei tena.” Mh. Selasini alizitaja baadhi ya hatua hizo kama ni pamoja na kuhamisha maghala yote ya silaha na mabomu yaliyo karibu na maeneo wanayoishi raia na kuyapeleka katika Kambi za JWTZ zilizoko mbali kabisa na maeneo ya raia. “Haiwezekani kwa Serikali kuendelea kuweka maghala ya silaha katika Kambi za Jeshi zilizo karibu na wananchi na hivyo kuhatarisha maisha yao namna hii”, alisema Mh. Selasini.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewataka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kujiuzulu mara moja ili kuwajibika kisiasa kutokana na maafa ya Gongo la Mboto na ili kupisha uchunguzi huru na wa kina wa chanzo na/au sababu za milipuko hiyo. Mh. Selasini alisema: “Dr. Hussein Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati wa maafa ya Mbagala; na Jenerali Mwamunyange alikuwa Mkuu wa Majeshi. Maafa ya Mbagala yalitokea chini ya dhamana na/au usimamizi wao. Na mara baada ya maafa hayo, Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange waliliahidi taifa kwamba maafa ya aina hii hayatatokea tena. Sasa yametokea. Inaelekea, kwa hiyo, kwamba ahadi yao ilikuwa sio ya kweli na/au hawakuhakikisha kwamba inafanyiwa kazi ili iwe ya kweli. Viongozi hawa hawana budi kuwajibika kwa hiari yao wenyewe au kuwajibishwa kama itahitajika.”

Mh. Selasini aliongeza kusema kwamba hadi leo hakuna taarifa yoyote rasmi iliyowahi kutolewa hadharani kwa wananchi na/au kwa wawakilishi wao Bungeni ya chanzo na/au sababu za maafa hayo. “Hadi leo hii wananchi na/au wawakilishi wao Bungeni hawajaambiwa kama kulikuwa na makosa ya makusudi na/au ya uzembe na/au kama hatua zozote za kinidhamu na/au za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya mtu yeyote kutokana na kusababisha na/au kuwajibika kwa maafa hayo. Jana maafa mengine ya aina hiyo hiyo yametokea tena na kwa kadri ya taarifa rasmi ya Serikali watu wengi wameuawa na wengi wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa. Kwa sababu hizo, huu ni wakati muafaka kwa Dr. Mwinyi na Jenerali Mwamunyange kuonyesha uadilifu wao kwa kujiuzulu nafasi zao ili kuwajibika kwa maafa haya.”

Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imependekeza iundwe Tume Huru ya Uchunguzi na/au Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza kwa kina chanzo, sababu na madhara yote yaliyosababishwa na milipuko ya Gongo la Mboto. “Kwa kuzingatia historia ya uchunguzi wa milipuko iliyotokea Mbagala mwezi Aprili 2009, Tume Huru na/au Kamati Teule ya Bunge lazima itoe taarifa yake hadharani kwa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, alishauri Mh. Selasini.

Ni taarifa nzuri. lakini Je itafaniwa kazi?

Yetu macho!!!!!
 
Back
Top Bottom