NAHISI MAJIBU YA WAZIRI YANAWEZA KUA HIVI
Mimi Kama waziri sijiuzu na sitafukuzwa kazi kwa sababu zifuatazo
Nchi yetu hatuna historia ya kufukuzana kazi
Pia hatuna utaratibu wa kujiuzulu ovyo hovyo, wazungu wao hujiuzulu ovyo hovyo kwa sababu wanajiweza kifedha, Mi nikijiuzulu unataka familia yangu ikale wapi.
Tatu, tulisema milipuko kama ya mbagala haitatokea tena, kwa kuthibitisha hivyo, Mbagala yalipiga mchana, Gongo la Mboto yamepiga usiku, huoni hapo kama ni tofauti? Kua kama msomi, hata Mungu alipoahidi hataiangamiza dunia kwa mvua, haina maana mvua hazinjeshi tena.
Sababu ya milipuko ya Gongo na Mbagala ni tofauti, Mbagala ilikua ni uchakavu. Gongo ilikua ni sikukuu na mkusikia fataki hata moja, hii ina maana iliwakilisha fataki pia, Pia chama cha Riadha kinakufa kwa hiyo ilikua nafasi ya kuwapata wanariadha pia, pia hua tunafanya majaribia oa mioto, hii pia ilikua kujaribu milio ya Somalia pia.
Mwisho kabisa naomba kumwambia Selathin kua yeye mwenyewe Tembo husumbua wananchi wake kila mwaka huko Rombo, mbona hajiuzulu huo uwaziri kivuli? Kujiuzuli sio mchezo