Liberal man
Member
- Nov 2, 2010
- 5
- 0
Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.
Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.
Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.
Huyu jamaa anajiita mwiba mimi nadhani hayuko sawa, hivi ni uchunguzi gani unataka ufanyike wakati mabomu yameua innocents tanzanians..tena ni zaidi ya mara moja imetokea.. maboma yamelipuka ni uzembe wa wahusika au uniambie yale ya mbagala CCM walisema nini Tatizo, au kuna mtu yeyote aliwajibishwa? usilete ushabiki wako wa CCM wakati suala hili very serious..wewe labda ni Fisadi au mtoto wa fisadi au kibaraka fulani, njoo maeneo ya Gongo la mboto alaf uongee ujinga wako kama utatoka mzima..