Tamko la CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhosni, Feb 17, 2011.

 1. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MAAFA YA GONGO LA MBOTO: WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI WAJIBIKE!

  TAARIFA KWA UMMA
  DODOMA, FEBRUARI 17, 2011

  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika Ghala la Kuhifadhi Silaha la Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana jioni.

  Aidha, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya maafa haya. Pia Kambi hiyo imezitaka mamlaka zote za umma zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wote walioathirika na maafa haya wanapatiwa huduma zote wanazohitaji katika kipindi hiki cha msiba huu. Hii ni pamoja na kuwapatia huduma za maziko wale wote waliofariki, matibabu kwa waliojeruhiwa na hifadhi kwa wale waliopoteza makazi yao. Aidha, ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha ulinzi wa mali za wananchi katika maeneo yote yaliyoathirika na ambazo zitakuwa hazina ulinzi baada ya wananchi kukimbia maeneo yao.

  Taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kwamba tukio hili ni la kushtusha na kusikitisha hasa kwa kuzingatia kwamba haijapita miaka miwili tangu tukio la aina hiyo hiyo litokee katika Ghala ya Silaha ya Kambi nyingine ya JWTZ katika eneo la Mbagala, Dar es Salaam, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini na uharibifu mkubwa wa mali za umma na za wananchi binafsi. Aidha, milipuko ya Mbagala ilipelekea Serikali kutumia mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya malipo ya fidia kutokana na vifo, majeruhi na uharibifu wa mali binafsi za wananchi.

  Akielezea tukio la milipuko ya Gongo la Mboto, Msemaji wa Ulinzi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Joseph Selasini alisema: “Milipuko ya Gongo la Mboto inaonyesha dhahiri kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haijajifunza lolote kutokana na maafa yaliyotokea Mbagala mwaka juzi. Maana kama Serikali ingejifunza kutokana na maafa hayo ingeshachukua hatua za dharura na za haraka kuhakikisha kwamba maafa ya aina hii hayatokei tena.” Mh. Selasini alizitaja baadhi ya hatua hizo kama ni pamoja na kuhamisha maghala yote ya silaha na mabomu yaliyo karibu na maeneo wanayoishi raia na kuyapeleka katika Kambi za JWTZ zilizoko mbali kabisa na maeneo ya raia. “Haiwezekani kwa Serikali kuendelea kuweka maghala ya silaha katika Kambi za Jeshi zilizo karibu na wananchi na hivyo kuhatarisha maisha yao namna hii”, alisema Mh. Selasini.

  Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewataka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kujiuzulu mara moja ili kuwajibika kisiasa kutokana na maafa ya Gongo la Mboto na ili kupisha uchunguzi huru na wa kina wa chanzo na/au sababu za milipuko hiyo. Mh. Selasini alisema: “Dr. Hussein Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati wa maafa ya Mbagala; na Jenerali Mwamunyange alikuwa Mkuu wa Majeshi. Maafa ya Mbagala yalitokea chini ya dhamana na/au usimamizi wao. Na mara baada ya maafa hayo, Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange waliliahidi taifa kwamba maafa ya aina hii hayatatokea tena. Sasa yametokea. Inaelekea, kwa hiyo, kwamba ahadi yao ilikuwa sio ya kweli na/au hawakuhakikisha kwamba inafanyiwa kazi ili iwe ya kweli. Viongozi hawa hawana budi kuwajibika kwa hiari yao wenyewe au kuwajibishwa kama itahitajika.”

  Mh. Selasini aliongeza kusema kwamba hadi leo hakuna taarifa yoyote rasmi iliyowahi kutolewa hadharani kwa wananchi na/au kwa wawakilishi wao Bungeni ya chanzo na/au sababu za maafa hayo. “Hadi leo hii wananchi na/au wawakilishi wao Bungeni hawajaambiwa kama kulikuwa na makosa ya makusudi na/au ya uzembe na/au kama hatua zozote za kinidhamu na/au za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya mtu yeyote kutokana na kusababisha na/au kuwajibika kwa maafa hayo. Jana maafa mengine ya aina hiyo hiyo yametokea tena na kwa kadri ya taarifa rasmi ya Serikali watu wengi wameuawa na wengi wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa. Kwa sababu hizo, huu ni wakati muafaka kwa Dr. Mwinyi na Jenerali Mwamunyange kuonyesha uadilifu wao kwa kujiuzulu nafasi zao ili kuwajibika kwa maafa haya.”

  Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imependekeza iundwe Tume Huru ya Uchunguzi na/au Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza kwa kina chanzo, sababu na madhara yote yaliyosababishwa na milipuko ya Gongo la Mboto. “Kwa kuzingatia historia ya uchunguzi wa milipuko iliyotokea Mbagala mwezi Aprili 2009, Tume Huru na/au Kamati Teule ya Bunge lazima itoe taarifa yake hadharani kwa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, alishauri Mh. Selasini.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Good chadema ......the peoples party. Huwezi kusikia hata siku moja ccm ikatoa tamoko km hili
   
 3. Pilato2006

  Pilato2006 Senior Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hata Mkuu wao aliyewateua aachie ngazi. Yeye ndiye awe wa kwanza
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja, Mh Dr H. A. Mwinyi, na General Mwamnyange onyesheni uadilifu wenu.
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Eee waunde tume huru siyo kuendelea kulindana, na wajiuzulu mara moja wasijifanye ndo wako busy wanashuhulikia tatizo. Waachie wengine wafanye hiyo kazi
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Lakini hao chadema nao wakiishia kwenye kauli peke yake hakuna litakalotokea. Hata mauaji ya arusha walitoa kauli, tena nzito!!!!
   
 7. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Jamani hili la ajali lichukuliwe kwa uzito wake na si kwa ushabiki wa kisiasa...kiungwana nadhani zifanyike juhudi za haraka za kuokoa maisha ya wahanga wa tukio hili na zichukuliwe hatua za haraka kuhakikisha hakuna maafa zaidi baadaye...na baadaya hali kuwa shwari mamlaka husika zijipime kama kuna uzembe wowote katika hili uwajibikaji uwepo!
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,931
  Trophy Points: 280
  Chadema walishatuonya wakati wa kampeni kuwa kuichagua CCM ni kuleta maafa katika nchi hii,sasa nimeelewa maana ya kauli ile. Maafa kama haya ya kizembe yataendelea kutokea siku hadi siku (nasi tutabaki kusema Mungu aepushilie mbali) kwa vile hakuna wa kumwajibisha mwenzie ndani ya serikali hii. Wale wabunge wa chama kinachowakilisha watanzania kila wakisema yaliyo ya msingi wanaishia kuzomewa na hao wabunge maslahi.
   
 9. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa mkuu Chadema haina Serikali wala haiwezi kuwajibisha hao watu ndo maana inaishia kutoa kauli tu otherwise we unapendekeza Chadema wafanye nini?
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  na shimbo aendelee? maana for sure shimbo hapendi kumwona mwamu kuwa bosi wake.
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  sasa hii ni reported speech au ndio tamko lenyewe, mie sijaelewa manake aya zingine unaonekana unatoa taarifa ya alichosema selasini na mwisho naona saini yake!

  any way hata hivyo umeeleweka na ujumbe umefika.

  poleni waathirika wote na RIP wenzetu mliotangulia mbele ya haki. hakika damu zenu zitaililia nchi hii hadi hapo itakapowatendea haki kwa kjali maisha ya watu. amen
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kweli watanzania tumelogwa hii tungekuwa tumelichukulia kwa uzito hawa watu wange jiuzuku kwa shinikizo la watanzania wenyewe siyo kwa maneno ya mtu moja moja haswa wabunge wetu wa chadema ndiyo watetezi wetu ccm bure kabisa
   
 13. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Serikali dhalimu huandamwa na mikosi na balaa nyingi. Watanzania wasome ishara hizi na kuikataa serikali hii. Viongozi wanaosababisha matukio yote haya tunayoyaona yakitokea, kamwe hawataki kuachia ngazi. Hii ni aibu kubwa kwelikweli. Ninadhani wanataka tuwang'oe kwa mtindo wa Tunisia na Misri.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukisikia viongozi hawana dira ndio hawa ,yaani baada ya kuitisha uchunguzi unakurupuka na kusema nani na nani wajiuzulu,basi huyo msemaji nae ajiuzulu ,wacheni uhuni,yaani unarukia watu wajiuzulu wakati hujui ni nini chanzo cha tukio.

  Wandugu mkisikia watu wanajiuzulu huko majuu msifikiri wanakurupuka tu na kuachia ngazi kuna stage mbalimbali hupitwa na ndio kufikia ni nani wa kujiuzulu.

  Mi nilifikiri katika taarifa hiyo CDM wamefanya uchunguzi na kugundua chanzo na sababu ni ya wakuu flaniflani ,kumbe hamna kitu ni mazungumzo baada ya habari.
  Kwa ufupi tahadharini na habari za mitaani na kuzivalia njuga ,mtakuja kuumbuka baadae,embu wekeni kitengo cha uchunguzi na muwe mnazifanyia uchunguzi habari kabla hamjazitilia ubavu, yaani mkiulizwa suali la papo kwa papo kwa nini hao wajiuzulu sijui mtajibu dudu gani ? Zaidi mtasema ni uzembe ,mkiulizwa uzembe gani mtaanza kutafuna kucha.
  WaCDM wacheni hizo karata za magarasa tumieni turufu ,natumai nimeeleweka.
   
 15. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mh..Gurudumu, hebu toa mawazo yako..wewe unafikiri Chadema wafanye nini??
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani hizo intelijensia zingesaidia sana kwenye masuala kama haya badala ya kutumika kuua raia wasio na hatia wala silaha kwenye maandamano ya amani. Kila mtu alitarajia tukio la mbagala lingetoa funzo kwa wahusika kuchukua hatua stahiki lakini hawakufanya hivyo mbali ya kukataa kujiuzulu. Sasa tunapoteza watu wasio na hatia na wengine kupata ulemavu. Huu ni UZEMBE WA HALI YA JUU. Rais, Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi LAZIMA WAJIUZULU.
   
 17. S

  SURNAME Member

  #17
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema walishatuonya wakati wa kampeni kuwa kuichagua CCM ni kuleta maafa katika nchi hii,sasa nimeelewa maana ya kauli ile. Maafa kama haya ya kizembe yataendelea kutokea siku hadi siku (nasi tutabaki kusema Mungu aepushilie mbali) kwa vile hakuna wa kumwajibisha mwenzie ndani ya serikali hii. Wale wabunge wa chama kinachowakilisha watanzania kila wakisema yaliyo ya msingi wanaishia kuzomewa na hao wabunge maslahi.


  Tuache ushabiki wa kisiasi,hili ni janga.Sidhani kama chadema walijua janga hili kwa umoja wetu tuhakikishe wahanga wanahudumiwa kwanza,watu wanawajibishwa tena kwa uwazi hasa viongozi.
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  tUACHANE NA SIASA KWANZA NDUGU ZANGU TUKACHANGIE KWA HALI NA MALI KWA WAATHIRIKA!
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hili la tume ambapo taarifa wanazikalia wao wenyewe na kuwa siri ni bora wajiuzulu kwanza then the rest will follow kila siku tume tumechoka bwana
   
 20. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri kuna mtu anasimulia....na sio tamko lenyewe!
   
Loading...