Tamko la CHADEMA - Aprili 14, 2013

Status
Not open for further replies.
Kisimani hata mm nilikuwa na hofu kama yako issue ni kuwa washazidaka, issue za kuomba mahakama iruhusu ni kwa ajili ya kufuata taratibu tu!

Hata kama CDM wana ushahidi, hauwezi kutumika mahakamani maana kwa vyovyote haujapatikana kihalali-hata kama ni ushahidi wa kweli. Mawasiliano ya simu ni siri, na hivyo hutolewa kwa kibali cha polisi tu. Nakubaliana na njia iliyotumika na CDM, kwamba kwakuwa ni kesi ya kisiasa, basi waende kisiasa!
 

Zitto ni kwanini uliacha kuitumia namba hiyo. Au baada ya kazi yake kukamilika?. Haya mambo ya kufukia laini ya simu tumezoea kuona katika sinema za kijasusi!. Naanza kukuogopa!
 
Nimeikumbuka hii kauli ya JK aliyoitamka kwa kujiamini "Wanaotaka CCM ife watakufa wao", Kumbe vifo vyenyewe ndiyo hivi vya kung'oa watu meno, kunyofoa kucha na kutaka kukiua CHADEMA kwa hila chafu za namna hii!, Hakika Mungu yu upande wa wenye haki. Atawaumbua wote wenye kutumia mamlaka zao vibaya, atawaumbua wote wenye kutumia nguvu za giza na mapepo kutaka kuwadhuru wengine. Washindwe na walegee.
 

To be smart, technical terms are unnecessary but the content do.
 
kweli nimeamini mungu mkubwa,lile sakata la ulimboka limerudi tena,mwigulu ni zaidi ya shetani,kwanini ulishiriki kumtesa huyu daktari wa watu,damu yake na ya absalom kibanda zinakulilia.

Mwigulu ni muuaji PERIOD
 
Nakubaliana nawe Pasco kwamba ktk hali ya kawaida, hili halikupaswa kufanyika hivi. Lakini kwasababu suala lenyewe limejaa siasa toka mwanzo, CDM hawakuwa na jinsi isipokuwa kutoka namna hii. Hii ni preemptive strike, yaan hata CCM wakiweza kuchakachua mawasiliana, bado watakuwa wameshikwa pabaya maana jamii itajuwa wamechakachua! Kama bado hawajachakachua, sasa wataona aibu maana wamegundulika-sanasana watafuta kesi. Nakubaliana nawe kwamba hii kesi itafutwa.
 
Mungu Ibariki Chadema
Hakuna jiwe litakakosalia juu ya jiwe jingine..... Uovu wote utafichuliwa.
Natanzania huru itanyanyuka
......Freedom is Coming....
 
To be smart, technical terms are unnecessary but the content do.

Subiri details za kilaza kigagula mpiga picha Michuzi ziletwe ndo utasema kama content is necessary. Mnajifanya nanyie mnajua software
 

Pathetic!
 
unajua chadema walisha kaa kimya na walikuwa wanafanya uchunguzi wao kimyakimya, ila sababu ccm wanaendleza hilo zogo la kuchafua cdma hvyo ndo maana wameamua kutoa hizo detail na hii ni kufanya wajue kuwa kuna ushahidi wa kutosha.

Kama ni hivyo, kwa nini wasisubiri wakautoa huo ushahidi mahakamani?
 
...... utapitishwa ndani, ndipo nitaitwa na nitakutembeza tembeza sehemu mbalimbali!, hadi desk la jf, nitakuonyesha majina halisi ya vimbelembele wote hadi locations na ip address zao!. Karibu sana!.
Pasco.
Kumbe wewe huna maana, ni kuwadi la kutupwa, upo kwa ajili ya maslahi ya bwana zako. Unawapigania ili wapande juu, kana kwamba wewe ulizaliwa uwe ngazi! What a spineless man!!
 

Kama hujui sheria nyamaza tu, acha kuandika vitu visivyokuwepo. Tatizo lako unakurupuka sana Pasco. Mwanasheria yoyote akiona ulichokiandika hapo atapata kichefuchefu. Ni ushauri tu.
 
Basi si wangetulia ili ukweli ujidhihiri kuwa hawana hatia au Lwaka hana hatia? Kwa nini wanaendelea kuhangaika kutoa maelezo kuanzia bungeni hadi kwenye press

Unajua ungesoud vizuri sana kama ungemwambia mwigulu alikosea kuanza na media kutangaza mkanda huo, na kisha you tube, ndipo akapeleka polisi.

Bado haajaridhika na mahakama sasa anataja majina ya watu Bungeni kwa kupanic kama mwehu. Halafu jinsi Mungu anavyowaumbua, anatembea na ushahidi wa polisi hadi bungeni bila kujua kama anazidi kuthibitisha kwamba hii ni syndicate ya magumashi.

Unaonekana wa pekee kidogo, unapo attack Chadema kwa kusema na press.
haalfu pia naona una tatizo la wanaccm wenzako wa kutokusoma vitu na kudandia juu kwa juu bila kuelewa. Lengo la cDM kwenda press limewekwa wazi sana. sijui ninin unauliza.

Tatizo ccm hamsomagi vitu ndiyo maana mnsainishwa mikataba na kusomeshwa hotuba za ajabu.
 

Lakini kwa wenye akili za kujitosheleza wanajua kuwa hizi ni siasa za chooni ambazo zinakiuka misingi ya utoaji wa haki. Na ni ubakaji wa haki kama ilivyotokea kwenye kesi ya Lema.
 
Naww hapa ndiyo mwisho wako wa kufikir na kuandika ushuzi huu? Mhh samahan huenda tatizo sio wewe!


KWA USHAURI TUU, MSINHANGAIKE NI THREAD AU COMMENT ZA BUNGENI, KWA NI ID MPYA YA MGONJWA MAARUFU WA JF CHRIS MKOSO aka CHILISOSI aka BUNGENI. YANI ANAFUKA CONSISTENTLY KIASI KWAMBA HATA ANGEAZIMA ID YA RITZ BADO NI RAHISI KUBAINI KUWA NI YEYE KWA VILE SPECIAL ASSIGNMENT ALIOPEW NA LUMUMBA NI KUFUKA BILA MPANGILIO ALAFU ANATUMIA ID ZAKE ZOTE KULIKE POVU LAKE. WATCH OUT GUYZ CHILISOSI ''THE AMPLIFIER'' IS STILL LIVE, as BUNGENI.
 

Mkuu ZZK.
Kwanza heshima mbele na hongera kwa kuwa bold enough kujitokeza na kukisema kile ambacho chama chako kimeshindwa kabisa kukifanya toka sakata hili liibuke!.

  1. Number yako imeingia kwa bahati mbaya kwa sababu Chama chako, kinamtegemea "source" yule yule, aliyeweka mawasiliano yako na Jack Zoka, kwa kutumia number hiyo hiyo!. Kwa vile ndiye huyo huyo aliyewafanyia "udukuzi" alipoiona number ya Zoka, kwenye ile kazi ya mwanzo, akaicopy na ku paste huku, kumbe cakopy ya kwako!, bahati nzuri mimi namjua, na naamini na wewe unamjua!, kiukweli itajafika siku Chadema kama chama, mtaingizwa Chaka, au choo cha kike kwa kuletewa taarifa za "udukuzi" na nyinyi kuzianika bila kufanya any verification!. Sasa hii taarifa ya number yako, mpelekee Marando, kesho atoe tamko jingine kurekebisha kosa hilo, na kukuomba radhi kwa kukuchafulia jina!.
  2. JF itake kuthibitisha ili iweje?, taarifa ya nambo hiyo si iliwahi kuanikwa na mawasiliano yako yote si yaliwahi kufanyiwa "udukuzi" na hukukanusha chochote kule, kama number ukiisajili ni number yako, uitumie usiitumie ni yako, tena huwajibiki kutoa sababu zozote za kutiotumia kwa yoyote, unless kama hiyo ni number ya kazini, huku ndiko unaweza kutoa sababu na sio hapa jf!.
  3. Kwa vile aliyewafanyia "udukuzi" namfahamu, nakuhakikishia hiyo number imeingizwa kwa bahati mbaya katika copy and paste!.
  4. Umeliita hili tukio ni Upuuzi wa Ugaidi na Unyama dhidi ya Binadamu!, kauli yako hii inakwenda kinyume cha "collective resiponsibility ya chama chako, hakuna ugaidi wowote bali ni freming ya CCM na UWT, kwa vile chama chako hakiamini kuna ugaidi wowote, then hakuna kukuhusisha wewe kwa namna yoyote na ndio maana chama kinatumia juhudi kubwa kumkumbatia Rwakatare kuwa video ile ni fake na anasingiziwa tuu!.
  5. Haya uliyoyasema, ndio yalipaswa kusemwa na Chama chako since day 1, video ilipotoka tuu!. Kitendo cha chama chako kutumia negation kukanusha ukweli halisi, na badala yake kumkumbatia Rwakatare,na wewe kuja kukanusha uhusika wako, ni contradiction ma msimamo wa chama chako, na kanusho lako hili, linakupeleka tena against ile collective resiponsibility ya Chama chako uliotueleza siku ile ukiizungumzia leakage ya barua yako!, sasa ndio umeileta tena contents ile ile kwa mlango wa nyuma, ili ikithibitika ni kweli Rwakatare alihusika kwa namna moja au nyingine, wewe uwe tayari uliisha nawa mikono!. Collective resiponsibilities ni pale mkishakubaliana msimamo wenu kwenye jambo fulani ni huu, wote mnakuwa kitu kimoja na kuushikilia msimamo mmoja, hata kama hukubaliani nao!. Maadam chama chako hakijakanusha kitu, wewe hupaswi kukanusha kitu na ikitokea mmoja wenu akawemo, wote mtakuwemo!, you can't stand aloof!.
  6. Nakupongeza kusimama na Msacky, "that's what friends are there for" kama sisi tunao kuaminia, tunavyosimama na wewe no matter what!, ila kwenye hili la uwepo wa "kirusi" ndani ya Chadema, aliyempatia mkanda ule Mwigulu, kama ikitokea ukawa ni wewe!, kiukweli, sitakuelewa kabisa kwa sababu nitatishwa na "the motive behind" hiyo move!.
  7. Naungana na wewe katika hili la kusimama kwenye kweli daima kama mimi ninavyo amini kuhusu ule mkanda kuwa "bonafide genuine!" hivyo ukweli huu ukithihiri, kuna watu, wakubwa wazito na heshima zao, watatafuta pa kuficha sura zao!. Ukiaminiwa, jiaminishe!, ukishindwa kuaminika kwenye haya madogo kama "bonafide genuine!" kuuita fake, utaaminikaje katika makubwa?!.
  8. Hili la kuichia mahakama, nalo neno!, kama nyinyi wenyewe bungeni mmeshindwa kuiheshimu mahakama!, chama chako kinashindwa kuiheshimu mahakama, unategemea sisi jf, tutaiheshima vipi?!. Bado nakuaminia uwezo wako wa ushawishi na jinsi ulivyo "a man of principles!", naomba basi kwanza uanze na ku "practice what you preech" ndani ya chama chako, uje kwako binafsi na ndipo umalizie kutushauri na sisi!.
Asante.

Pasco wa jf.
NB. Pasco wa jf, ni mtu anayemkubali sana ZZK na amesimama na ZZK katika nia yake ya kuitumia haki yake ya kidemokrasia ndani ya Chadema,Urais 2015 Nasimama na Zitto; Kwa Sababu Naujua Msimamo wa Dr. Slaa ... ila pia huwa tunatofautia katika baadhi ya mitazamo, Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.
 
Hapo ndipo panapotushangaza sisi wote, ni kwa vipi anamtetea Msacky ilihali mlolongo wa matukio unaonyesha wazi kwamba ni mhusika? Kwanini asiassume kwamba Msacky anaweza kumgeuka sawasawa na ambavyo Ludovick alimgeuka Lwakatare waliyekuwa wanafanya kazi ofisi moja? Ila mimi nina uhakika kabisa, kwamba Zitto ndiye atakayekwenda kusimama mahakamani against CHADEMA. Katika hili tusubiri tu wakati.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…