TAMISEMI yatoa orodha ya vituo vya afya 90 vitakavyojengwa kwa tozo za miamala

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
Awamu ya kwanza ya Vituo vya Afya 90 kati ya 207 katika Tarafa zisizo na Vituo vya Afya, ambazo zimepokea fedha Mil. 250 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la Maabara na Kichomea Taka hii hapa.

20210821_152305.jpg
20210821_152308.jpg
 
Hapa sawa.... wakate tu. Ila pia ni vyema tukapewa mrejesho tuvione vituo hivo vikiwa vinaendelea kujengwa au kuwa na taarifa za kukamilika kwake. Na kamwe sitolalamika...

Go Mama

RIP our Father JPM
 
Kwa nini za miamala waonyeshe vituo vya Afya watuambie Pia kodi za kwenye madini zimejenga nini, za luku %18 zimejenga nini, za majengo zimejenga nini, za mafuta ya kupikia zimejenga nini za mitungi ya gesi zimejenga nini, za mafuta ya gari zimejenga nini, tuachane na za wafanyabiashara(TRA kila baada ya miezi mitatu) hizo tunajua niza kula bata.
 
Huu ni utaratibu mzuri wa kuweka uwazi mapato na matumizi ya kodi za wananchi. Natumaini uwazi huu utaendelezwa kwenye sekta zote za umma.

Hata hivyo, fedha hizo zinaonyesha kuwa vituo vyote vimepokea kiasi sawa cha fedha, je matumizi yatazingatia fedha hizo tu au kuna fedha nyingine zitatumika? Kwa maana sidhani kama matumizi yanaweza kuwa sawa katika vituo vyote.
 
Dah ni vzur ila tatizo sijue nani katuloga utakuta hayatimii kama inavyotakiwa na hela hamna mtu anajua zimeenda wapi kwa ss hela tumetoa wenywe ngja mkurugenzi wale tunawahukumu ss wenyw hatusubir mahakama au takokuru
 
Kwamba watatoa hizi statstics miaka yote ambako tozo zitakatwa? mbona kama ni jambo mnafanya ili kutubrain wash tuone muyafanyayo yana mantiki
 
Tatizo hayo ni makaratasi
Implementation ndio tatizo.
Waweke na hela ya vifaa tiba na madawa tuone.
Sababu majengo bila hizo nyenzo ni kazi bure..
Kila nikikumbuka milioni 50 kila kijiji na laptop kwa kila mwalimu nachoka.
 
Serikali kupitia TAMISEMI imetoa Orodha ya tarafa 90 zitakazopokea fedha awamu ya kwanza katika ujenzi wa Vituo vya afya. Matokeo ya tozo mbalimbali yameanza kuonekana na kushikika maana wadau wengi waliomba Orodha ya hivyo vituo. TUJIPONGEZE TUKITHUBUTU TUTAFIKA
 
Attachments

  • ORODHA YA VITUO 90.pdf
    109.5 KB · Views: 5
Serikali kupitia TAMISEMI imetoa Orodha ya tarafa 90 zitakazopokea fedha awamu ya kwanza katika ujenzi wa Vituo vya afya. Matokeo ya tozo mbalimbali yameanza kuonekana na kushikika maana wadau wengi waliomba Orodha ya hivyo vituo. TUJIPONGEZE TUKITHUBUTU TUTAFIKA
Watu waanze kulipana posho kwenda kusimamia
 
Hapa sawa.... wakate tu. Ila pia ni vyema tukapewa mrejesho tuvione vituo hivo vikiwa vinaendelea kujengwa au kuwa na taarifa za kukamilika kwake. Na kamwe sitolalamika...

Go Mama

RIP our Father JPM
Mi pia nimependa bora tu wakate.
 
Hiyo vituo vya afya vilikuwemo kwenye ilani ya CCM ama vimeibuka kama uyoga?
 
Back
Top Bottom