Bashungwa: Tozo zimejenga vituo vya afya 234

Mbaga Lazaro

Senior Member
Aug 9, 2020
132
107
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amesema Serikali imejenga vituo vya afya 234 kutokana na fedha za tozo ya miamala ya simu ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Bashungwa ameyasema hayo leo Septemba Mosi wakati akizungumzia manufaa ya tozo hizo ambazo zimekuwa zikipingwa na wadau mbalimbali kwa sababu tofauti ikiwemo kutozwa mara mbili au zaidi.

Amesema hadi kufikia Desemba 2020, Serikali ilikuwa imejenga hospitali za wilaya 102, vituo vya afya 487 na zahanati 1,198.

Amesema serikali ilifanya tathmini ya hali ya hospitali hizo na kuja na mradi wa kujenga vituo vya afya kwenye kila tarafa.

Amesema katika tarafa 570, tayari serikali imejenga vituo vya afya 234 kwenye tarafa 207 ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliingia madarakani Machi 19, 2021 baada ya kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli.

“Kupitia tozo za miamala ya simu, tumeweza kujenga vituo vya afya 234 kwa Sh117 bilioni kwenye hizi tarafa 207 na kila kituo cha afya kimetugharimu Sh500 milioni.
“Ukiangalia toka nchi yetu imepata uhuru na awamu zote zilizotangulia, kuweza kujenga vituo vya afya 234 ndani ya mwaka mmoja, si jambo la kawaida,” amesema Bashungwa.

Amesema kinachopatikana kutoka kwenye kodi jumuishi, kinakwenda kutibu kiu ya wananchi ya kupata huduma za msingi kama vile afya, elimu na barabara na inasaidia kupunguza pengo kati ya wenye nanchi na wasio nacho.

“Tutaendelea kuhakikisha kwamba tunazitumia fedha hizi kutoa huduma bora za afya ya msingi katika maeneo mbalimbali nchini,” amesisitiza Bashungwa.

Kwa upande wa sekta ya elimu, amesema kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwamba, serikali inatakiwa kuendelea kujenga madarasa 15,000 kila mwaka ili kukidhi mahitaji hayo.

“Tathmini ambayo tumeifanya tunahutaji kuendelea kujenga madarasa yasiyopungua 15,000 kila mwaka hadi hawa waliopo kidato cha kwanza watakapoingia kidato cha sita, niwaombe Watanzania hii nchi ni ya kwetu tuendelee kuipa ushirikiano Serikali,” amesema Bashungwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Muda utaongea.
Naomba sana Lisu arudi kwa kipindi hiki na ikiwezekana maandamano yaanzie hapohapo Airport kwani hii imezidi yaani watu wanadanganya hata aibu hawaoni.
Mm ni mwanaccm ila kwa hili hapana chama changu kiondoke tuu ili tuanze upya yaani mafao yangu mnakata Tozo
 
Hajasema wamekusanya jumla ya sh. Ngapi hadi sasa.
Hilo huwa hawalisemi kwa kuwa siagi yao inapopatikana.

Imagine wakati wa JPM walidai wamejenga vituo kibao, Maza pia na mikopo yake ya IMF wakadai amemwaga pesa na kujenga nyingi pia .... hivi Tanzania tunahitaji vituo vingapi vya afya, zahanati na hospitals. Inaonekana biashara ya kupiga pesa sasa iko kwenye shule na vituo vya afya ..... kama enzi zile za madawati.
 
Mimi huku nliko wala eneo la karibu sijaona shule mpya wala kituo kipya cha afya. Au pengine macho yangu.
Hilo huwa hawalisemi kwa kuwa siagi yao inapopatikana.

Imagine wakati wa JPM walidai wamejenga vituo kibao, Maza pia na mikopo yake ya IMF wakadai amemwaga pesa na kujenga nyingi pia .... hivi Tanzania tunahitaji vituo vingapi vya afya, zahanati na hospitals. Inaonekana biashara ya kupiga pesa sasa iko kwenye shule na vituo vya afya ..... kama enzi zile za madawatiwal
 
Mimi huku nliko wala eneo la karibu sijaona shule mpya wala kituo kipya cha afya. Au pengine macho yangu.
Hizi Hesabu wanazotupa Nina wasiwasi nazo. Tatizo journalists wetu ni wavivu kutafuta ukweli. Nakumbuka enzi za JPM tuliambiwa wametengeneza madawati 100 % na idadi ya watoto shule ime double... After one year tukaanza kusikia tena tatizo la madawati na madarasa.
 
Serikali ya Mama inawachekea naamini hata Mawaziri hawapendi huu utaratibu wa kuoleana kindezi na kudekezana bila sababu za msingi..

Na uhakika Mwendazake asingeruhusu huu utoto wa watu kukataa kulipa tozo za kuleta maendeleo..

Mwisho Hawa Hawa watu wa Dar wasiotaka kulipa tozo Wala hawana shida Wala kuona madhila ya watu wa Vijijini.
 
Back
Top Bottom