TAMISEMI ongezeni muda wa kutuma maombi ya ualimu na afya

Ondoa hofu wana kibao tu wamepata check number, we tuma maombi muda unaelekea kuisha.
Huyu ndugu yetu anamashaka na utumishi nazani kule ajira portal sio tamisemi kama sijakosea maana kule wana wengi wanadai vyeti ni lazima viwe verfied na mwanasheria
 
Muda n mfup na mbaya watoto wa maskin taarfa zinawafkia late na wengine unakuta vyet bado vko chuo na nauli Gafla hana
 
Ni kweli mtoa hoja una a valid concern, kwa bahati mbaya ni kua idadi ya siku za Tangazo kua wazi zimepangwa kwa kuzingatia vigezo.

Kwa upande mwingine deadline haiwezi kubadilishwa kwa kuangalia “subjective factors” mfano mtu fulani hajachukua transcript and all that, ila kwa vigezo ambavyo viko fair kwa waombaji wote.

Najua kuna watakaoumia ila pia wengi wata meet timeline iliyowekwa.

The earlier, the better!
 
Kuna watu wako Dodoma kule, hamtaki kuwatumia kwa masuala ya haraka kama ya huko MCT, mnakuja humu kusumbua. Akina Dodoma messengers wana kazi gani kule,msiwapigie wawaharakikishie michakato na utumwaji wa nyaraka zenu?

Ngoja siku ziyoyome muone,mwisho wa siku aje Luhaga Mpina, ashike urais, afanye Kama JPM, azuie kuajiri, ndipo ambapo mtamkumbuka huyu mama, na kulaumu uzembe wenu.
MCT wanakuta ufuate leseni mwenyewe na sio kumtumia mtu ila pia Wana uwezo wa kkukutumia kwa njia ya EMS au hata kwa DMO ama RMO tatizo ni kwamba haitofika kwa wakat
 
Ndugu zangu ningeomba tutumie huu Uzi kutoa maoni Kwa kuwaomba TAMISEMI kuongeza Muda wa watanzania kutuma maombi ya Kazi za ualim na Afya.

Kwanza muda uliotolewa no siku ambazo sio Chini ya 20 na yawezekana wengi wasiombe na kukosa Fursa ya Kuajiriwa(Kwa wale watoto wa maskini) ambao hawana plan yoyote ile.

Tunaomba Mama yetu ANGELA KAIRUKI uongeze Muda ili wafuassi wako wapate kupona. Sababu kubwa za Kuomba muda uongezwe no hizi hapa;
1. Ucheleweshaji wa Transcript na Leseni za MCT
Kwa ambao mmenda NACTE pale Kuna watu waliomba Transcripts za Kada ya Afya Kwa muda mrefu lakini Huwa zinacheleweshwa. Mtu analipa ili atumie Transcripts mkoani anaisubiri haimfikii anaamua Kufunga safar mpaka NACTE ili apatiwe anatumia siku Mbili Toka Mkoani mpaka Dar akifika pale tayari muda unakuwa umeisha kabisa au anapewa majibu ya subiri.

2. Ulazima wa kuwa na Leseni za MCT na Bodi nyingine kama Za Famasia na Uuguzi Kwa Nursing. Kama mnavyojua anayemaliza chuo Kwa Afya ili afanye kazi lazima awe na leseni. Hii wengi hawaipingi ila tatizo ni pale ambapo Leseni hizi zinachelewa. Mfano mtu kamaliza chuo 2020 ama 2021. Akishamaliza chuo anapaswa awe na leseni leseni kuipata sio Chini ya 400K yaani ada zake na Enrollment Fees. Kwa watanzania walio wengi kupata Laki nne ya kulipa ili apewe leseni kwanza ni Kizungumkuti. Pili Kwa wengine akishalipia Leseni haifiki Kwa wakati. Mfano hapo MCT Kuna mtu alilipia leseni Wiki Iliyopita Jumanne akaambiwa ndani ya Siku Tano itapatikana akaamua Kurudi Mkoani amekwishafika anaisubiri anaambiwa bado. Ina maana Mpaka Deadline inafika atakua hajaipata.

Kama mnavyojua wengi hufuatilia vyeti vyao pale ambapo kazii hutangazwa lakini Kuna yrasimu MKUBWA wa kupata vyeti haswa vya kitaaluma na ukitoa wiki mbili owe deadline ya kutuma maombi watu wengi wanaumia
Zipo sababu nyingi sana ambazo zinachelewesha watu kutokupata Documents zote za kuombea kazi.

Tunawoamba TAMISEMI kuongeza Muda hata wa wiki mbili au zaidi ili watu wapate Fursa ya Kuomba Kazi na kuijenga Nchi.
Mkuu ondoa shaka wataongeza mpaka ijumaa ila endelea kufuatilia documents zako.
 
Kuna watu walimaliza Vyuo 2020 na 2019 lakini mpaka Sasa hawajafikiwa na Transcripts. Hebu nenda pale NACTE Mikocheni uone watoto wa Maskini wanavyohaha kupata Transcripts. Kuna watu wamesubiri vyeti hvyo zaidi ya Mwaka. Wakipiga simu mtu anaambiwa subiri. Muda uongezwe
Acheni uzembe Cheti unatakiwa uwe nacho unapokuwepo ili ikitokea tu ajira omba


Siioni haja ya kuongeza muda kwa kisingizio Cha Muda
 
Kuna watu walimaliza Vyuo 2020 na 2019 lakini mpaka Sasa hawajafikiwa na Transcripts. Hebu nenda pale NACTE Mikocheni uone watoto wa Maskini wanavyohaha kupata Transcripts. Kuna watu wamesubiri vyeti hvyo zaidi ya Mwaka. Wakipiga simu mtu anaambiwa subiri. Muda uongezwe
Uongo nakupinga asilimia mia
Mi nmemaliza 2021 mwaka jana 2022 nmechukua transcript yangu hapo Dodoma tena ilitumwa kutokea daresalam

Uongo hautakusaidia mzee
 
MCT wanakuta ufuate leseni mwenyewe na sio kumtumia mtu ila pia Wana uwezo wa kkukutumia kwa njia ya EMS au hata kwa DMO ama RMO tatizo ni kwamba haitofika kwa wakat
Mkuu kwa hapo usiwasingizie MCT,watu kibao huyo Dodoma Messengers kawachukulia,mskanie barua ya maombi ya cheti na leseni,mpatie na kitambulisho cha mpiga kura.Kazi imeisha.
 
Cheti pamoja na leseni wanachukuliwa,barua ya maombi na kitambulisho chà muombaji pamoja na kitambulisho chà aliyetumwa,ndiyo vinavyohitajika.Usiwavunje moyo.
 
Ndio maana Hii Nchi watu wanabeba mihela wakijua kuwa watanzania wengi hawawezi wafanya lolote na watawanyamazia. Mtu anaibua hoja ambayo watanzania wengi wanakutana nazo unaibuka huko eti sio lazima uajiriwe.. Points zote ambazo mtu anatoa ni Uhuru wake na ni kilio Cha walio wengi na haujalazimishwa kuandika Hapa. Wakati mwingine ni vyema kukaa Kimya kuliko kuongea ukkonekana mjinga
Utaomba wakati ujao mkuu..
 
Mkuu kwa hapo usiwasingizie MCT,watu kibao huyo Dodoma Messengers kawachukulia,mskanie barua ya maombi ya cheti na leseni,mpatie na kitambulisho cha mpiga kura.Kazi imeisha.
Sawa chief, hivi ofisini za MCT ziko maeneo gan ? Na mtu anatakiwa kushuka wapi ukitokea Dar?
 
Sawa chief, hivi ofisini za MCT ziko maeneo gan ? Na mtu anatakiwa kushuka wapi ukitokea Dar?
Jamaa unaweza ukashukia stendi ya Shabiby au Kimbinyiko au maeneo yaliyopo karibu na hizo stendi,ukachukua boda kwa 1000 akakukimbiza Jakaya Kikwete,utahudumiwa,ndipo walipoweka kambi,ila kikawaida huwa pale Kambarage Tower,bilashaka wameona waende Jakaya Kikwete Convention Center kwasababu ya jam.
 
Mdau ambaye una jambo la kufuatilia,liwe la kiofisi au siyo la kiofisi,na halikulazimu wewe kuwepo Dodoma au upo Dodoma ila umebanwa na kazi nyingi,wasiliana na 'DODOMA MESSENGERS' kwa 0765920855,usaidiwe kulifuatilia na kulitatua ukiwa hukohuko uliko,kwa gharama nafuu.
 
Back
Top Bottom