Tambwe Hizza amshambulia Mwanakijiji

tambwe.JPG


accm03.JPG


Mzee wa Propaganda ndani ya CCM

Hii mijamaa ya CCM mbona iko minene minene hivi? Halafu mashori wa kibongo eti wanaiona iko sexy...WTF!?!?!
 
Kama ni RICHARD HIZA TAMBWE hakuna lolote la kumsikiliza. Ni mmoja wa wanasiasa ambao maslahi yake binafsi yako mbele kuliko ya chama, na taifa lake. Jamaa ni cheap sana alikuwa hot cake CUF akanunuliwa kwa bei chee CCM, atatumiwa kwa muda na atutupwa soon.

Nakumbuka kuna kiongozi mmoja bungeni naye alianza kujibizana na mwanakijiji, nae alisema hivyo hivyo kuwa mwanakijiji mzushi, lakini it appeared kuwa mwanakijiji was right. I wonder whether this time around Mwanakijiji has boobed and HIZA has got it right.
 
Hii mijamaa ya CCM mbona iko minene minene hivi? Halafu mashori wa kibongo eti wanaiona iko sexy...WTF!?!?!

Hahaha, shoris za Yo Yo Tell 'em hizo lol... Huyo Tambwe Hiza ndio anahama hama vyama kila kukicha?

Lakini hiyo closing remark yake amembait mwanakijiji, kutokuijibu itakuwa kugumu sana.
 
Hii mijamaa ya CCM mbona iko minene minene hivi? Halafu mashori wa kibongo eti wanaiona iko sexy...WTF!?!?!
teh teh iko sexiiii kwa minjuluku ya ufisadi inayowamwagia mademu,na unene mzee si unajua mifisadi kadri inavyoiba ndivyo invyoongezea kujichana vyuku na bia mpaka ipasuke
 
.

Muosha uoshwa.

Mwana kijiji amekuwa akiwashambulia sana wana jf kwa majina tofauti humu ndani.

wacha na yeye achafuliwe.


Samweli akili yako ina akili kweli ? Wewe umesha wahi kushambuliwa ? Kwa hiyo unakubali maneno ya Tambwe ?
 
I guess so. Ila njaa kitu kingine aisee. Hebu fikiria lijitu kama Komba bila shati....OMG!
HAHAHAHAH!anakuwa na wrinkles za kufa mtu!bonge la tumbo,hahahahah!ukiwaleta 6 by 6,mshindo mmoja tu CHALI!MBONJI MPAKA ASUBUHI!

hahahahah!
 
wrong move on TAMBWE HIZA na CCM

Rule number 1: You dont pick a fight you cant win na hii ya kupick a fight na Mwanakijiji sidhani kama watamweza kwani mwenzao muda wa kujibizana na supporting data anazo..wao wameamua kumpeleka Tambwe kukabiliana naye duh!

Another wrong move ni kumpa platform MKJJ kujibu hoja sasa sijui kama watakuwa wamejiandaa na hiyo mi dossier aliyonayo

hawa jamaa wamekuwa kama headless chiken wapo wapo tuu.

Badala ya kutuambia lini wataongeza ufanisi bandarini wao wanatafuta watu wa kutukanana nao

tyatakayo wakuta saizi yao..asiyesikia la mkuu huvunjika guu
 
wrong move on TAMBWE HIZA na CCM

Rule number 1: You dont pick a fight you cant win na hii ya kupick a fight na Mwanakijiji sidhani kama watamweza kwani mwenzao muda wa kujibizana na supporting data anazo..wao wameamua kumpeleka Tambwe kukabiliana naye duh!

Another wrong move ni kumpa platform MKJJ kujibu hoja sasa sijui kama watakuwa wamejiandaa na hiyo mi dossier aliyonayo

hawa jamaa wamekuwa kama headless chiken wapo wapo tuu.

Badala ya kutuambia lini wataongeza ufanisi bandarini wao wanatafuta watu wa kutukanana nao

tyatakayo wakuta saizi yao..asiyesikia la mkuu huvunjika guu
naona mzee unalia na bandari!watakusikia tu!vipi hauhitaji ''ka-nzi?''hahahahah!mimi nipo tz na hii kazi naiweza sana,hasa ukinipa kazi ya kuangalia ufisadi katika ugavi na zabuni!i know ins-and outs
 
naona mzee unalia na bandari!watakusikia tu!vipi hauhitaji ''ka-nzi?''hahahahah!mimi nipo tz na hii kazi naiweza sana,hasa ukinipa kazi ya kuangalia ufisadi katika ugavi na zabuni!i know ins-and outs

basi usimwage mtama mwingi kwnye ndege

mie ni TRA,BANDARI na ARDHI nina ugomvi nako mkubwa tuu
 
Who is Tambwe Hiza?
Nadhani picha peke yake zitakuwa hazikutoshelezi,

Basi soma chini hapa:-

Richard Tambwe Hiza, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezaji wa Chama cha Wananchi (CUF) na sasa amepewa kazi mpya kama hiyo na na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

CCM ni almost imempa Tambwe kazi ya kuvibomoa vyama vya upinzani. Kwa hiyo chama alichokuwa akikisifu, sasa anakikashifu, na kile alichokuwa akikikashifu, sasa anakisifu!

Wananchi walijiunga na CUF baada ya hotuba zake na hii leo Tambwe kishageuka. Anajitahidi kukichambua Chama cha CUF. Lakini kwa vyovyote anapata wakati mgumu. Maana yake kama CUF imeoza, yeye mwenyewe ni sehemu ya uozo wa CUF anaouzungumzia!

Si kazi rahisi kwa mtu yeyote kugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli, isipokuwa kama tu mtu mwenyewe ni mwongo.

Akiwahutubia wananchi wa Morogoro wakati wa sherehe za
CCM kutimiza miaka thelathini, Tambwe alidai kuwa vyama vyote vya upinzani kwa sasa vimepoteza mwelekeo wake na badala yake vimebakia na sera ya uongo.

Hapa mtu analazimika kujiuliza, tangu lini vyama vya upinzani vimepoteza mwelekeo? Baada ya Tambwe kuondoka upinzani? Kwani Tambwe alikuwa Mkurugenzi wa Habari wa Umoja wa Vyama vya Upinzani?

Ni uongo mwingine kutudanganya kuwa hivi sasa vyama vyote vya upinzani vina sera ya uongo.

Anajuaje utendaji wa vyama vingine wakati hajawahi kufanya kazi kwenye vyama hivyo kama kauli yake si ya mtu aliyefunzwa kusema uongo na haraka amebobea?

Tambwe, kama ni mkweli, asingethubutu kudai kuwa vyama vyote vya upinzani vina sera ya uongo bila kutuchambulia uongo wa CHADEMA, TLP, NCCR – Mageuzi, UDP na vyama vingine vya upinzani. Ukweli ni kwamba Tambwe hakuelewana na chama chake cha CUF.

Kumbe katika kuifurahisha
CCM ili izidi kumfurahisha anakuja na uongo kwamba wapinzani wote ni waongo. Kwa hiyo yeye amekuwa mkweli baada ya kujiunga na CCM! Uongo mwingine.

Kuna methali moja ya Kiswahili inayosema kuwa ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.

Tambwe ni mtu aliyepitwa na wakati. Wakati wananchi wamekitoa maanani
Chama Cha Mapinduzi, yeye anajitokeza kukitia maanani chama hicho. Anashangaza.

Tukizungumzia uongo kama sera ya vyama, Tambwe analazimika kukubali kuwa uongo ni sera ya
Chama Cha Mapinduzi. Si sera ya vyama vya upinzani.

Ninaamini kuwa Tambwe anajua kwa kiasi fulani umuhimu wa katiba ya nchi. Katiba ya nchi si kitu cha kupambwa na uongo. Lakini Chama Cha Mapinduzi tunachoaminishwa kuwa kina sera ya ukweli kimejaza uongo ndani ya Katiba ya nchi.

Je, Tambwe anakubali maneno ya Katiba ya nchi yetu kuwa “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa?” Tambwe hajawahi kusema katika mikutano yake kwamba
CCM ni Chama cha kidikteta?

Je, aliwahi kusema mahali popote kwamba
CCM ni Chama cha kidemokrasia? Hajawahi kusema kuwa CCM imepoteza mwelekeo wake wa kujenga ujamaa na sasa inajenga ubepari Tanzania?

Leo anataka kutuaminisha kuwa
CCM ni chama kinachojenga demokrasia na ujamaa Tanzania? Uongo mwingine.

Tusiende mbali. Turudi mwaka jana tu. Je, Tambwe amesahau haraka mawaziri wa serikali ya
CCM walivyotudanganya mwaka mzima kuhusu upatikanaji wa umeme wa kampuni yao ya Richmond? Hapa hii ni sera ya uongo ya CCM au ni ya wapinzani?

Hakika. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno. Tambwe ni mtu aliyepitwa na wakati. Anakishabikia chama kinachokimbiwa na ambacho wananchi wanakitema mate.

Hapana shaka Tambwe amepata habari kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya
CCM Dar es Salaam sherehe za CCM mwaka huu zilidoda kwa sababu zilikimbiwa na wananchi wa Dar es Salaam.

Mapema siku hiyo ya sherehe
CCM kama kawaida yake ilipeleka mabasi ya kuchukua wanachama wake maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam. Lakini tofauti na miaka mingine ambapo wanachama wa CCM walikuwa wanajikusanya mapema kusubiri mabasi, safari hii mabasi yalipoteza wakati mwingi yakisubiri wanachama wa CCM. Maandamano ya CCM yakadoda. Mkutano wa CCM ukadoda pale Jangwani jambo ambalo si la kawaida.

Bila
CCM kujaza pale Jangwani wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee, Uwanja wa Jangwani ungebaki wazi.

Lakini haya yote ni matokeo ya nini? Ni matokeo ya wananchi kuchoshwa na sera ya uongo ya
CCM.

CCM inatangaza maisha bora kwa kila Mtanzania huku ikiharibu mali za watu waliojitahidi kujipatia wenyewe maisha bora.

Ni lazima tuseme kweli. Tambwe hakuwa mpinzani. Mpinzani wa kweli hawezi kurudi
CCM. Akikorofishana na chama chake ama atajiunga na chama cha upinzani au atabaki bila chama.

Tambwe hakuwa mpinzani wa kweli. Na wenzake wa kundi lake pia. Na wazunguke mikoa yote kuua upinzani Tanzania.

Kwa vyovyote katikati ya Serikali ya
CCM iliyojaa uozo ni jambo la kubahatisha kufuta upinzani.

CCM imedhoofika kiasi sasa imevamia vyuo vikuu kugeuza wanavyuo kuwa wanachama wa CCM na wanafunzi wa shule za sekondari kuwa chipukizi wa CCM wanaofanya halaiki katika sikukuu za CCM.

Ukweli ni kwamba tangu mwanzo wake, mfumo wa vyama vingi haukutakiwa kuhusisha masuala ya siasa kwa wanajeshi, mahakimu, watumishi wa serikali, wanavyuo na wanfunzi.

Na kwa upande wa wanachuo, iweje wanachuo wale wale walioandamana mpaka Jangwani wakiipinga Serikali ya
CCM, siku chache baadaye wajiunge na CCM?

Nani hajui kuwa
CCM imewarubuni wao kwa kuwatumainisha kuwa watapata mikopo na U-DC wakajiunga na CCM? Kwa hiyo kule wamefuata mikopo. Hawakufuata CCM. Na kama Serikali ya CCM imerubuni wanachuo kujiunga na CCM maana yake ni kwamba CCM imeruhusu pia wanachuo kujiunga na upinzani.

Hizi si habari njema. Maana yake ni kwamba
CCM imekaribisha mapambano ya kisiasa mashuleni na vyuoni, ambayo yatavuruga amani na umoja katika maeneo hayo.

Na kwa kuwa
CCM ni chama cha ukandamizaji, bila shaka serikali ya CCM itawasumbua wanavyuo itakaowatuhumu kuwa ni wapinzani ikishirikiana na wakuu wa vyuo hivyo waliobariki hatua ya wanavyuo kujiunga na CCM.

Tuhitimishe kwa kukumbushana kuwa leo ni miezi minane tangu Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipoidhinisha shilingi bilioni moja kupelekwa kila mkoa.

Na fedha hiyo haijawafikia bado wananchi. Wakati Serikali ya
CCM ilisema kuwa fedha hiyo itatolewa kwa wananchi bila masharti magumu, mabenki yamewapa wananchi masharti magumu.

Je, katika mazingira haya, maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana? Ukweli ni kwamba
CCM inaendeleza sera yake ya uongo.

Kwa hiyo imepoteza mwelekeo. Na imepoteza mvuto, ndiyo maana inakimbiwa


Hii Ndiyo Habari aliyotoa wakati anahamia
Chama Cha Mapinduzi


Tambwe Hiza: Sikuwahi kuwaza kurejea CCM

Kutoka Gazeti la Nipashe,
Na Mashaka Mgeta

Hivi karibuni aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Ueneza wa Sera wa
Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Richard Tambwe Hiza alitangaza kujiondoa rasmi kutoka katika chama hicho chenye nguvu kubwa ya upinzani na wafuasi wengi na kujiunga katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Bw. Hiza anaelezea masuala mbalimbali yanayohusiana na hatua yake hiyo.

Swali: Bw. Richard Tambwe, hivi karibuni ulitangaza uamuzi wa kujiondoa katika
Chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga CCM. Unaweza kuelezea chanzo cha msukumo uliokufanya kufikia hatua hiyo?

Jibu: Ni kweli nimeamua kujiondoa kutoka
CUF kutokana na sababu mbalimbali, kubwa zaidi zikiwa zinahusu mambo binafsi na ukweli wa hali halisi.

Kwa upande wangu kama mtu binafsi, nilijitolea sana kukijenga chama cha
CUF na kukitumikia kwa uadilifu mkubwa, hadi kukifanya kuwa ngome imara ya upinzani.

Ni kutokana na uongozi wangu nikiwa Mwenyekiti wa
CUF wilaya ya Temeke, nilifanikisha kupatikana ushindi wa Mbunge mmoja, madiwani watano na wenyeviti 51 wa serikali za mitaa wilayani humo. Rekodi hii sina hakika kama inaweza kuvunjwa hivi karibuni.

Na mafanikio hayo yalitokana na jitihada binafsi nikiwa kiongozi mkuu wa
CUF wilayani kuwaunganisha vijana, wazee na wanawake na kusimamia utekelezaji wa sera za chama kiasi cha kufikia mafanikio hayo. Lakini katika hatua ambazo zilionyesha kutojali mafanikio na mchango wangu, ilifika mahali CUF waliona kuwa wamenitumia kiasi cha kutosha, na mimi nikaona mahali pale hapanifai tena, nikaondoka.

Swali: ulizungumzia sababu ya ukweli wa hali halisi kuwa ni miongoni mwa msukumo uliokufanya kufikia hatua hiyo, unalizungumzia vipi suala hilo?

Jibu: Kwa kweli katika uhalisia wake, ni kwamba imefika wakati wanasiasa wawe wakweli kwa ajili ya maslahi ya watu wanaowaunga mkono na taifa kwa ujumla.

Kwa muda mrefu, hata nilipokuwa katika upinzani nilishiriki kuudanganya umma na kutoa tuhuma mbalimbali dhidi ya
CCM na serikali zake kwamba hazijaleta maendeleo kwa taifa hili.

Hatua hiyo haikuwa na sababu nyingine zaidi ya kutaka kuungwa mkono na watu hasa wasiokuwa na upeo kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii.

Swali: Kuondoka kwako
CUF kunadaiwa pia kulitokana na hatua ya chama hicho kukuvua uongozi ulipokuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Sera?

Jibu: Hilo linaweza kutafsiriwa hivyo, lakini suala la kunivua uongozi ni miongoni mwa vielelezo vya wapinzani wanaodai kutetea haki sawa na misingi ya demokrasia inayokidhi matakwa ya Katiba ya nchi, huku wenyewe wakiwa hawafuati katiba za vyama vyao.

Kwa mfano, mimi nilikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Sera wa CUF, lakini Mwenyekiti wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba alinivua madaraka hayo na Wakurugenzi wengine na kuteua Wakurugenzi wengine, kuanzisha Kurugenzi mpya madaraka ambayo kwa mujibu wa vifungu namba 82.1 na 63.1(e) vya Katiba ya
CUF, yanapaswa kufanywa na Baraza Kuu la Uongozi.

Kwa hiyo hatua ya kutofauta katiba ni mapungufu yaliyopo kwenye uongozi wa chama hicho na hivyo inaweza kuwa tafsiri halisi ya miongoni mwa sababu za kuondoka katika
CUF.

Swali: Pamoja na mapungufu hayo, unafikiri kwa mtazamo wako kuna mambo ya msingi na yenye maslahi kwa umma yaliyofanywa kutokana na mchango mkubwa wa
CUF?

Jibu: Ni kweli kuna mambo yaliyotokana na shinikizo la kisiasa hasa kutoka CUF ambayo yamewezesha kuleta mabadiliko kadhaa kwenye jamii yetu ingawa kwa upande mwingine ninaweza kusema mafanikio yote hayo yasingefikiwa kama siyo mchango wa busara za viongozi wa CCM na serikali zake

Hivyo
CUF wamejitahidi sana kuikosoa serikali ya CCM ingawa kwa mambo machache yaliyokuwa na ukweli na mengi yakiwa yanatokana na haja ya kutaka kuungwa mkono huku yakiwa yamejikita katika upotoshaji mkubwa.

Kwa mfano mafanikio ya kuwepo kwa muafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar, ulitokana na busara za viongozi wa
CCM.

Muafaka huo ni sehemu ya matukio kadhaa yaliyoimarisha tofauti za kisiasa hasa visiwani Zanzibar na kutishia umoja wa kitaifa.

Swali: Unadhani kuna mambo mengine yenye mapungufu uliyoyashuhudia yakifanywa na
CUF ama upinzani kwa ujumla?

Jibu: Kwa hakika yapo mambo mengi. Labda nianze na hili la jumla linalohusu madai yenye nguvu kutoka kwa
CUF yanahusu masuala yenye maslahi kwa Zanzibar badala ya taifa katika ujumla wake.

Ukiacha suala hilo ambalo sipendi kulizungumzia kwa undani zaidi, mambo mengine yanayoenezwa na upinzani kwa lengo la kujiongezea umaarufu wa kisiasa ni madai kwamba
CCM haijaleta mafanikio ya kimaendeleo tangu taifa hili lilipopta uhuru wake.

Kauli kama hiyo ni miongoni mwa dhambi kubwa niliyoifanyia
CCM na Watanzania kutokana na kauli nilizokuwa ninazitoa wakati nikiwa CUF.

Swali: Ulikuwa miongoni mwa wanasiasa vinara walioaminika kwa misimamo mikali ndani ya
CUF, hivi kuna wakati uliwa kufikiria kuwa utajiunga CCM?

Jibu: Kwa kweli sikuwahi kufikiria kuwa nitajiunga
CCM na hili lilitokana na mfumo wa mapokeo niliyoyapata kwenye upinzani hasa katika CUF. Lakini pia mimi nilikuwa na dhamana kubwa katika chama ambacho sikustahili kuwepo huko.

Hivyo mara kadhaa nilijikuta kwenye wakati mgumu, kwamba wakati kulikuwa na kundi kubwa la watu waliokuwa wakiniamini katika yale niliyokuwa ninayafanya na kuyasema, dhamira yangu ilibaini ukweli na kuhisi kutaka kuondoka upinzani ili nirejee
CCM, hatimaye nikafanikiwa.

Swali: Uliondoka
CUF ukiwa Mkurugenzi na kiongozi wa ngazi za juu katika chama hicho. Sasa kuna hisia za watu kuwa kurejea kwako CCM kunaweza kukufanya upoteze umaarufu na pengine ukose hata wadhifa kama uliokuwa nao CUF?

Jibu: Mimi nilijiunga
CCM siyo kwa lengo la kutaka cheo, matarajio yangu ni kama waliyonayo Watanzania wengine wote kwa chama tawala na serikali zake.

Nitafanya kazi kwa kadri ya maelekezo ya viongozi wangu na kwa vile
CCM ina taratibu nzuri za kuwasilisha maoni kupitia vikao halali, wafuasi wangu wasitegemee tena kuniona sana kwenye majukwaa ya siasa pengine pale nitakapohitajika tu.

Swali: Kuna madai yanayotolewa na baadhi ya wanasiasa hasa katika chama chako cha zamani, kwamba umenunuliwa na
CCM kama ilivyo kwa wanasiasa wengine wa upinzani wanaorejea CCM, nini mtazamo wako kuhusu hilo?

Jibu: Kama nilivyosema awali, wapinzani wanafanya mambo mengine na yaliyo mengi kwa lengo la kuleta matumaini kwa wafuasi na wanachama hao, na katika kufanya hivyo wanajikita kwenye kuibua hoja zinazopotosha miongoni mwao ikimwemo hiyo ya kununuliwa na
CCM.

Kwa hiyo sioni nguvu iliyopo mbele ya hoja hiyo kiasi cha kufanya umma uamini hivyo kwa sababu,
CCM inakubalika miongoni mwa takribani asilimia 98 ya Watanzania wote. Sasa chama kinachokubalika kwa kiasi hicho kitaweza vipi kuninunua mimi mtu mmoja, kwa manufaa gani niliyonayo zaidi ya wale waliomo ndani yake?

Historia fupi ya Bw. Hiza

Bw. Hiza alizaliwa mwaka 1959 alipata elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1976 ambapo baada ya hapo alianza kujihusisha na masuala ya binafsi kupitia sekta binafsi.

Hata hivyo, wakati akiwa anaendeleza biashara yake alishiriki katika kukuza na kuiendeleza sekta ya michezo ambapo mwaka 1989 alipata fursa ya kwenda kusomea utawala na uongizi wa michezo huko nchini Sweden na baadaye alisomea uandaaji wa michezo ya Olympic huko Ugiriki na kutunukiwa Shahada ya fani hiyo huko nchini Ugiriki.

Mwaka 1992, Bw. Hiza alijiunga katika chama cha
CUF hadi mwaka 1995 ambapo kutokana na mwamko wa vuguvugu la kisiasa lililoibuliwa na aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana kwa wakati huo, Bw. Augustine Mrema alipojiondoa CCM na kuingia NCCR-Mageuzi, aliihama CUF na kwenda NCCR-Mageuzi.

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ambapo Bw. Hiza aliogombea ubunge katika jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam kupitia
NCCR, aliamua kumfungulia kesi aliyekuwa mshindi wa kiti hicho katika uchaguzi huo, Bw. Ali Kihiyo wa CCM ambaye Mahakama ilitengua ushindi wake.

Bw. Tambwe anasema baada ya ushindi wa kesi hiyo, aliyekuwa Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi ambaye hivi sasa yupo TLP akiwa na wadhifa huo, Bw. Augutsine Mrema alitaka na hatimaye kushinikiza aungwe mkono kuwania ubunge wa jimbo hilo badala yake (Hiza), hali aliyoichukulia kama ni ukiukwaji wa haki na hivyo alimua kurejea CUF mwaka 1996.

Aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la
CUF na Katibu wa Kamati ya kuhamasisha uhai wa chama hicho mkoani Dar es Salaam, huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo akiwa Bw. Khatib Hassan na 1999 Bw. Hiza alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CUF wa wilaya ya Temeke.

Mwaka 2001 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango na Uenezi hadi mwaka 2004 alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Sera hadi Aprili 28 mwaka huu alipopata barua ya kuvuliwa wadhifa huo na hatimaye kurejea
CCM mwaka huu.
 
Hata kuweka AC kwenye Arrivals pale uwanja wa ndege wameshindwa! Utadhani uko kwenye warehouse!

escalator pia imekufa!lol!imeniuma sana hii kitu juzi kati hapo.wadogo zangu ambao wanasoma physics hata huko dar watakuwa wanaiangalia tu kwenye NELKON!lol!

it hurts me a lots bana
 
Back
Top Bottom