Umerudishwa nyuma na nani? kuku?
Kabda icho kitambaa cheupe na damu
Hiyo ni mbinu tu ya kukudhoofisha,umefanya usafi na kuanza kazi hiyo ni hatua nzuri sasa fanya kazi kwa bidii zaidi hata ukikuta ng'ombe kachinjwa mlangoni we fanya usafi na kupiga kazi watachoka wenyewe.
Katika hali isiyo ya kawaida leo asubuhi nimefika Ofisini kwangu. Si unajua tena mambo ya kujiajiri. Nina ka salon kangu na mtaani kuna salon mbili nyingine. Lakini kufika mlangoni nikakuta kuna kichwa cha kuku, kitamba chekundu na damu. Pembeni kidogo nikaona kuna shimo limechibwa ndani kukiwa na kuku mweupe. Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma.
Pole sana mkuu watu kama hao hata kwetu wapo! Dumu kwenye maombi tu. Ila sijakuelewa hapo uliposema kuwa " Mi sio mtu ya kuamini Mambo ya kishirikina. Nimefanya usafi na kuendelea na biashara yangu.
Lakini kwa nini tunafanyiana hivi. Tunarudisha nyuma"