Quod Nocet Saepe Docet
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 7,944
- 17,280
Wasalaam
Leo 24 Julai, 2025 asubuhi, nakiri kupokea taarifa kadhaa kutoka kwa Wananchi wa Kata ya Baraa, Mtaa wa Kibao cha Njano kwa Mrefu, Arusha.
Kwamba, mtu mmoja mzima analea binti wa umri kati ya miaka 8 hadi 10 hivi ambapo yaani ni anampa vipigo tu apendavyo yeye hivyo, mtoto amejaa makovu ya vipigo kila sehemu, ananyimwa chakula, anafungiwa mlango alale nje na mateso mengine aina hiyo hadi shuleni, maendeleo yanasua sua.
KILICHOFUATA: nimewasiliana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo, maafisa ustawi wa jamii wameelekea eneo la tukio mara moja.
UJUMBE GANI KWA JAMII: tuache kutesa watoto, jicho la ustawi wa jamii linatamba alipo mwanajamii yeyote kwa ushirikiano na wananchi wenye mapenzi mema.
Hima, tuendelee kutamba na jicho la ustawi wa jamii 👁🇹 kuwadaka watu katili wa watoto popote/kokote 🇹🇿✍️
Pia, kumbuka kupiga 116 kituo cha taarifa za watoto. Vilevile, kuna namba za maafisa binafsi na za vituo vya huduma kwa wananchi hapa chini👇zikumbuke, mpe na mwingine.....
Mhe. Waziri Dkt. Gwajima, katika visa vingi vya matukio ya Mauaji, unyanyasaji na matukio mabaya ya kuwatesa watoto ambayo yamekuwa yakitokea katika jamii siku hizi ambayo tumekuwa tukielezwa kuwa sababu ni Wivu wa Mapenzi. Lakini ukifanya utafiti wa kina kabisa utagundua kwamba sababu halisi za kutokea kwa matukio haya ni:-
1. Kukosekana kwa Uaminifu katika Ndoa na kwenye Mahusiano (INFIDELITY).
2. Mwanamke Kumbambikizia Mwanaume, au Mpenzi wake kuhusu Mimba/ Mtoto ambaye siyo wake biologically, yaani PATERNITY FRAUD.
Sababu hizi mbili za hapo juu ndio zinaonekana kuwa zinaongoza kwa kusababisha Matukio mabaya ya Visa vya Mauaji, Vifo na Utesaji kwa Wanandoa, Watoto au wenzi katika siku hizi.
Mhe. Waziri, kutokana na kushamiri kwa matukio haya ya Mauaji kwa Wanandoa, Wapenzi pamoja na Watoto wao, Je, huoni haja ya kuanzisha Mpango wa LAZIMA kwa Wanandoa au Wapenzi wa KUPIMA DNA Mara tu Mtoto anapozaliwa ili kudhibiti na kupunguza kabisa matukio haya mabaya ya Mauji, vifo na mateso kwa Wananchi?
Kwa kuwa Uwaziri wako uko mwishoni Sana kwa Sasa kabla ya kufikia tamati yake, Je, huwezi kutumua siku hizi chache zilizobaki katika Kuandaa Mwongozo au Kanuni za kuwezesha Utekelezaji wa Jambo hili kwa vitendo la kuwalazimisha Wazazi kupima DNA kwa lazima mara tu Mtoto anapozaliwa?