Tamba na Jicho 👁 la Ustawi wa Jamii Mtaa kwa Mtaa 🇹🇿

Tamba na Jicho 👁 la Ustawi wa Jamii Mtaa kwa Mtaa 🇹🇿

Mhe. Waziri Dkt. Gwajima, katika visa vingi vya matukio ya Mauaji, unyanyasaji na matukio mabaya ya kuwatesa watoto ambayo yamekuwa yakitokea katika jamii siku hizi ambayo tumekuwa tukielezwa kuwa sababu ni Wivu wa Mapenzi. Lakini ukifanya utafiti wa kina kabisa utagundua kwamba sababu halisi za kutokea kwa matukio haya ni:-
1. Kukosekana kwa Uaminifu katika Ndoa na kwenye Mahusiano (INFIDELITY).
2. Mwanamke Kumbambikizia Mwanaume, au Mpenzi wake kuhusu Mimba/ Mtoto ambaye siyo wake biologically, yaani PATERNITY FRAUD.

Sababu hizi mbili za hapo juu ndio zinaonekana kuwa zinaongoza kwa kusababisha Matukio mabaya ya Visa vya Mauaji, Vifo na Utesaji kwa Wanandoa, Watoto au wenzi katika siku hizi.

Mhe. Waziri, kutokana na kushamiri kwa matukio haya ya Mauaji kwa Wanandoa, Wapenzi pamoja na Watoto wao, Je, huoni haja ya kuanzisha Mpango wa LAZIMA kwa Wanandoa au Wapenzi wa KUPIMA DNA Mara tu Mtoto anapozaliwa ili kudhibiti na kupunguza kabisa matukio haya mabaya ya Mauji, vifo na mateso kwa Wananchi?

Kwa kuwa Uwaziri wako uko mwishoni Sana kwa Sasa kabla ya kufikia tamati yake, Je, huwezi kutumua siku hizi chache zilizobaki katika Kuandaa Mwongozo au Kanuni za kuwezesha Utekelezaji wa Jambo hili kwa vitendo la kuwalazimisha Wazazi kupima DNA kwa lazima mara tu Mtoto anapozaliwa?
Uwaziri wangu unapoelekea kukoma, huenda sasa ndiyo mwanzo wa mwingine ajaye hivyo, ngoja nimalizie niliyoyapanga halafu, ajaye sasa utaanza naye haya maoni yako🤗, okay?

Asalaam Aleikum, Tumsifu Yesu Kristu....
 
Kazi nzuri, ilitakiwa ustawi wa jamii wa Mkoa wapewe taarifa Kwanza.

Au hata wilayani.

kama hawakupewa, ukapewa wewe Waziri, Maana yake kuna Tatizo.
Hakuna hata tatizo, wakati mwingine wananchi wanataka tu kukusikia kisa uko online. Hao maafisa ustawi wa jamii wanachapa kazi mno, shuhudia matokeo haya kisha waunge mkono👇👇👇
 

Attachments

  • IMG-20250610-WA0013(12).jpg
    IMG-20250610-WA0013(12).jpg
    274.1 KB · Views: 11
Taarifa haijajitosheleza,
Huyo Binti ni mtoto wa huyo Mwanaume aliyekua anamlea?
Mama wa huyo Binti yuko wapi?

Kama mpaka binti maendeleo yake ya Shule yalikua yana sua sua ina maana kua hayo mateso ameyapitia kwa muda mrefu bila kujulikana,

Watoto waelimishwe kua wanapopata matatizo kama hayo,watoe taarifa kwa Walimu wao Shuleni kama hawana uwezo wa kutoa taarifa Polisi au sehemu nyingine yeyote ile.
Ni kweli taarifa haijajitosheleza kwani, mengine nimweka kwenye bracket hadi baadae. Lengo la haraka haraka hii, ni kuwapa moyo jamii kuwa, wakiita ustawi wa jamii, wataitikiwa daima, kuzuia na kuokoa watoto dhidi ya ukatili ni kipaumbele....
 
Kama huko chini hawapo serious,je ni nani anafaa kulaumiwa? Ni nani kiongozi wa hao waliopo chini?

Huoni kua hao waliopo chini,wapo chini ya waziri? Je ni jukumu la nani kuwarekebisha hao waliopo chini au kuwachukulia hatua?

Maafisa Ustawi wa Jamii wapo, na wanafanya kazi kubwa sana kuliko hii ninayofanya. Ninachofanya ambacho wengine HAMKIONI, nikuonesha njia na mfano wa kuongoza kwa vitendo na kwa ari ya kujitoa. Wako watu kupitia mfano wangu wanaamka na kuongeza kasi.

Ona matokeo ya kazi yao kwa ufupi kabisa 👇
 

Attachments

  • IMG-20250610-WA0013(12).jpg
    IMG-20250610-WA0013(12).jpg
    274.1 KB · Views: 8
Mheshimiwa mshauri mama apumzike(aache kugombea)ili watanzania wazidi kumpenda zaidi na zaidi.Utafiti unaonesha kuwa watanzania wengi hawajapenda mama kujiteua peke yake pasipo kushindanishwa na wengine.
 
Maafisa Ustawi wa Jamii wapo, na wanafanya kazi kubwa sana kuliko hii ninayofanya. Ninachofanya ambacho wengine HAMKIONI, nikuonesha njia na mfano wa kuongoza kwa vitendo na kwa ari ya kujitoa. Wako watu kupitia mfano wangu wanaamka na kuongeza kasi.

Ona matokeo ya kazi yao kwa ufupi kabisa 👇
Muheshimiwa,mimi nilimjibu huyo aliyesema kua maafisa wa ngazi za chini hawafanyi kazi ipasavyo,

Big up kwa kazi nzuri,hii ni wizara ni muhimu sana katika kua na taifa bora coz taifa bora huanzia kwenye ngazi ya familia kwenye malezi.
 
Mh. Dorothy Gwajima wewe ulistahili kuwa Rais wetu kuliko huyu Mama aliyeko.
Napishana na maoni yako ndugu. Rais tuliyenaye ni anatosha kabisa na kazi zake zinajieleza. Pia, kama mimi nafanya kazi zinazowabariki, ikumbukwe ni yeye ndiye ameendelea kuniamini katika nafasi ya kutumika kama waziri hata pale ambapo, hata humu wengi kwa jicho lao walisema maoni yao mazuri kabisa kuwa, hafai huyu bure kabisa. Au mmesahau kwani? Hivyo, nami maoni yangu ni kuwa, tunaye Rais anayeona kwa jicho la ziada pengine, tofauti na mimi na wewe. Tumpe ushirikiano, OktobaTuka✅️✅️✅️ ili tuendelee na kazi na utu tusonge mbele✍️.
 
Hapo tafsir ni kwamba Waziri yupo makini anafuatilia shida za watu

Huku chini hawapo serious,hii ni shida kubwa,siku zote huwa tunawapa ushirikiano wanao tupa ushirikiano
Ndio tafsiri niliyonayo.

Zaidi maana yake kuna mamia wanafanyiwa vitendo vya kikatili ila hawaoni sehemu ya kureport
 
Back
Top Bottom