A
Anonymous
Guest
Kuna haja kubwa sasa ya kuzungumzia changamoto inayowakumba Maafisa Ustawi wa Jamii nchini.
Pamoja na kwamba Wizara ya Afya na Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalumu zilitenganishwa tayari, bado katika Halmashauri nyingi Ustawi wa Jamii inaendelea kubaki chini ya Idara ya Afya kwa kutumia muundo wa zamani usioendana na hali ya sasa.
Hali hii imeendelea kuathiri utendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika kutekeleza majukumu yao muhimu kwa jamii kama:
✔️ Ulinzi wa watoto
✔️ Kupambana na ukatili wa kijinsia
✔️ Malezi na ushauri wa familia
✔️ Huduma kwa wazee na watu wenye ulemavu
✔️ Msaada wa kisaikolojia kwa jamii
✔️ Kushughulikia changamoto mbalimbali za kijamii.
Kutokuwepo kwa Idara inayojitegemea kunasababisha:
❌ Kudhoofika kwa taaluma ya ustawi wa jamii
❌ Kukosekana kwa maamuzi huru ya kitaaluma
❌ Upungufu wa rasilimali na vipaumbele
❌ Ugumu wa kuwafikia wananchi kwa ufanisi
❌ugumu wa kupitishiwa madokezo ya kiutendaji
Tunaiomba TAMISEMI pamoja na mamlaka husika walitazame upya suala hili na kutoa muongozo rasmi kuhusu hadhi ya Ustawi wa Jamii ndani ya Halmashauri.
Jamii inahitaji huduma bora za ustawi wa jamii, na hilo linawezekana ikiwa taaluma hii itapewa nafasi stahiki na muundo unaojitegemea.
✊ Ustawi wa Jamii si kitengo cha pembeni ni mhimili muhimu wa ustawi wa wananchi.