TAKUKURU yakamilisha uchunguzi wa DED aliyedaiwa kwenda China kwa fedha za Halmashauri

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,538
8,547
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imekamilisha uchunguzi safari ya China aliyokwenda aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi.

Uchunguzi huo ulioanza mwanzoni mwa Novemba 2023, ulitokana na agizo la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe la kuitaka Taasisi hiyo kuchunguza safari ya mkurugenzi huyo kama ilikuwa na masilahi ya halmashauri au ni maslahi binafsi.

Pia, aliitaka taasisi hiyo kubainisha kama matumizi ya safari hiyo yalitokana na fedha za halmashauri au ni za binafsi na endapo watabaini alitumia fedha za halmashauri, zirejeshwe na zielekezwe kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza leo Aprili 25, 2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita, Azza Mtaita amesema uchunguzi umekamilika, kwa sasa jalada lipo kwenye hatua nyingine ya kupata maoni ya kisheria ili hatua nyingine ziweze kufikiwa.

Hata hivyo, Mtaita hakueleza kilichobainika katika uchunguzi huo.

Zahra aliyehudumu kama mkurugenzi wa mji wa Geita kwa zaidi ya miaka miwili na Desemba 2023 alihamishwa kwenda Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro wakati uchunguzi huo ukiendelea.
 
Babati maamuzi yalitoka mapema huku taratibu zingine zikifatwa

Mafia maamuzi yalitoka mapema Hulu taratibu zingine zikifatwa/fata

Huku NAzani maamuzi yalikuwa kumsogeza sehemu nyingine ili asije athiri uchunguzi, japo wananchi walitamani maamuzi ya kuwekwa Kando Kama yalivyofanyika kwa wengine

Hii inaweza kuwa kiashiria cha yeye kubakia madarakani

Sijajua kama aliyemtuhumu bado yupo pale au ameamishwa au na yeye amewekwa pembeni?

Kama ameamishwa ina wezekana ni namna ambayo Naye hasije athiri kinacho endelea

Ni taratibu za kawaida katika utawala wa sheria
 
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imekamilisha uchunguzi safari ya China aliyokwenda aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi.

Uchunguzi huo ulioanza mwanzoni mwa Novemba 2023, ulitokana na agizo la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe la kuitaka Taasisi hiyo kuchunguza safari ya mkurugenzi huyo kama ilikuwa na masilahi ya halmashauri au ni maslahi binafsi.

Pia, aliitaka taasisi hiyo kubainisha kama matumizi ya safari hiyo yalitokana na fedha za halmashauri au ni za binafsi na endapo watabaini alitumia fedha za halmashauri, zirejeshwe na zielekezwe kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza leo Aprili 25, 2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita, Azza Mtaita amesema uchunguzi umekamilika, kwa sasa jalada lipo kwenye hatua nyingine ya kupata maoni ya kisheria ili hatua nyingine ziweze kufikiwa.

Hata hivyo, Mtaita hakueleza kilichobainika katika uchunguzi huo.

Zahra aliyehudumu kama mkurugenzi wa mji wa Geita kwa zaidi ya miaka miwili na Desemba 2023 alihamishwa kwenda Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro wakati uchunguzi huo ukiendelea.
DED NI KADA WA CCM HAKUNA KESI HAPO
 
Back
Top Bottom