TAKUKURU Dodoma yakamata Tani 120 za Nondo zisizo na ubora zilizopangwa kujenga Barabraba ya Ihumwa-Bandari Kavu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma, imefanikiwa kuzuia matumizi ya nondo tani 120 zisizokuwa na ubora ambazo zilipangwa kutumika katika ujenzi wa barabara ya mzunguko nje (Ring-road) yenye kilomita 52.3 ya Nala-Veyula na Ihumwa- Bandari Kavu, iliopo jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa leo Agosti 23, 2023 jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Bw John Joseph, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu.

Bw. Joseph amesema TAKUKURU ilibaini Mkandarasi alipanga kutumia tani 120 za nondo ambazo ziko chini ya kiwango zenye thamani ya sh. milioni 204 ambapo kamazingetumika mradi ungetekelezwa chini ya kiwango.

“Baada ya njama hizo kubainika TAKUKURU ilichukua hatua za udhibiti ikiwa ni pamoja na kuziondoa tani zote za nondo ambazo zilikuwa eneo la ujenzi na Mkandarasi mshauri alishauriwa kuongeza umakini,” amesema Bw. Joseph

Hata hivyo amesema TAKUKURU Dodoma,imefanikiwa kudhibiti wizi wa sh milion 3.9 kutoka kwa mtumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chemba ambazo ni za wanufaika wa Mfuko wa TASAF wa kijiji cha Mlongia kilichopo wilaya humo, kwa ajili ya kukatiwa Bima ya Afya ilioboreshwa (CHF).

“Baada ya TAKUKURU kupata taarifa na kuingilia kati mtumishi huyo amerejesha fedha hizo na tayari zimewasilishwa katika mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya wanufaika 130 wa mfuko wa TASAF,”ameeleza

Aidha amesema kuwa wamefanya utekelezaji wa miradi 64 ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh billioni 12.7, ambayo ni ya Elimu, Afya, Ujenzi, Maji, na Mifugo, ambapo katika ufuatiliaji huo wameweza kuokoa kiasi cha sh Milion 41.2 ambazo zilikuwa katika hatari ya kufanyiwa ubadhilifu.

Katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2023, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma ilipokea Malalamiko 87 kutoka kwa Wananchi ambapo 54 yalihusu Rushwa ambayo yamefunguliwa Kesi

Uchunguzi wa Majalada 14 umekamilika na Majalada 10 yamewasilishwa Ofisi ya Mashtaka kwa hatua zaidi, Majalada 5 yamepata Vibali vya Kufungua Mashauri Mahakamani na Majalada 40 yako kwenye Uchunguzi

Mashauri 2 yamefunguliwa Mahakamani likiwemo shauri 1 linalohusu Rushwa ya Ubadhirifu wa zaidi ya Tsh. Bilioni 4.5 kutoka Idara ya Maliasili, Majalada 2 Watuhumiwa wake wamechukuliwa hatua za Kinidhamu

RUSHWA DODOMA
 
Dah, masikitiko, takukuru mna mambo mengi sana ya kufanya. Hili tena ndugu zangu la kawaida sana.
 

Attachments

  • 3AED5866-2577-4111-9110-9D505833DCF6.jpeg
    3AED5866-2577-4111-9110-9D505833DCF6.jpeg
    60.6 KB · Views: 4
  • 7B945073-BA0F-49C6-B465-B9B302794F79.jpeg
    7B945073-BA0F-49C6-B465-B9B302794F79.jpeg
    51.7 KB · Views: 4
  • 5D3687EF-D2C5-40F7-B2EA-11966A7DD729.jpeg
    5D3687EF-D2C5-40F7-B2EA-11966A7DD729.jpeg
    83.7 KB · Views: 4
  • 10733C58-5AB0-42B1-8218-4E3137FAF995.jpeg
    10733C58-5AB0-42B1-8218-4E3137FAF995.jpeg
    32 KB · Views: 3
Baada ya njama hizo kubainika TAKUKURU ilichukua hatua za udhibiti ikiwa ni pamoja na kuziondoa tani zote za nondo ambazo zilikuwa eneo la ujenzi na Mkandarasi mshauri alishauriwa kuongeza umakini,”amesema Bw.Joseph
Hawa jamaa n wanafki sometimes..
Huyu wanamuongezea umakini, lkn kuba mwanetu alidakwa kwa sababu ya buku 5 (yes, elf tano) na hadi leo ananyea debe.
 
Back
Top Bottom