TAKUKURU: Faili la Uchunguzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa TPA lakamilika, imebaki ofisi ya CAG kumaliza mchezo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa (Takukuru) imesema imekamilisha faili la uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko.

Machi 30, mwaka huu taasisi hiyo ilimkamata Kakoko ili kuhojiwa kuhusu tuhuma za ufisadi zilizomkabili ikiwa ni siku mbili baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza asimamishwe ili kupisha uchunguzi kuhusu udokozi wa fedha za umma.

Rais Samia alimwagiza pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dk Charles Kichere kuchunguza jinsi Sh bilioni 3.6 zilivyotumika kwenye mamlaka ya bandari.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema uchunguzi dhidhi ya bosi huyo na maofisa wengine umekamilika kwa asilimia 98.

“Asilimia mbili zilizobakia ni taarifa ya CAG ambayo ni muhimu sana, bila hiyo hatuwezi kwenda mahakamani.”

Mbungo alisema ripoti ya uchunguzi huo inahusisha pia sehemu ya taarifa ya CAG ili kudhibitisha tuhuma zinamkabili.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma:

 
Seth.jpg

Walipoingia angalia Walivyokuwa wamenawiri

sethpicc5-data.jpg

Daah! Jamani ni eidha waachiwe au wahukumiwe wanaweza kufia jela Matumbo yanazidi kurudi mgongoni.


John Magufuli has a net worth of around $1 million and $5 million. According to the information

Billioni sita za Kitanzania kaziacha hizo fedha zote alizitoa wapi?
 
Hivi ule uchunguzi wa akina Andengenye(kwasasa ni RC alikuwaga kamshina wa zimamoto) na kangi uliishia wapi? Takukuru waache kufanyia kazi maagizo ya kisiasa haya ya viongozi wa kitaifa
 
Yule kijana alyeambiwa na mama "ukinizingua tutazinguana mbona hachunguzwi?"

Baada ya Raisi kusema nanukuu " ofisi yako kama wakala wa meli imepoteza bilion 1.6"

Body language ya mtu aliyesimama wakati Raisi anamwambia uwizi huo, mwenye ofisi yake alikuwa anacheka all time

Back Tanganyika
 
Hivi ule uchunguzi wa akina Andengenye(kwasasa ni RC alikuwaga kamshina wa zimamoto) na kangi uliishia wapi? Takukuru waache kufanyia kazi maagizo ya kisiasa haya ya viongozi wa kitaifa
Wasukuma kazi mnayo,,kwaiyo unataka uyo jambazi Kakoko asishtakiwe
 
Hao nafikiri, next appearance wataachiwa huru either kwa mashsrti au bila masharti. Mbaya wao hayupo tena.
Ila hao Seth na Rugemarila sio wakuwaonea huruma kabisa, maana ndio waliokuwa wanasababisha mgao wa umeme miaka ile kwa hujuma zao na kina Lowasa
 
Back
Top Bottom