TAKUKURU: Chenge hahusiki na tuhuma za RADA

TAKUKURU: Chenge hahusiki na tuhuma za RADA

Sitta alishaapa kwamba atadili na Hosea akiukwaa Uspika kwa kosa la kumdhalilisha mke wake. Hapo unategemea Hosea afanye nn!
 
:A S angry:Hivi kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayeamini taarifa za TAKUKURU? Kumbuka waliwasafisha RICHMOND halafu baadaye Richmond ikaonekana ni kampuni hewa ya mafisadi. Vivyo hivyo kwa sakata la rada aingii akilini kwamba SFO imemsafisha Chenge. Hii ni mbinu ya PCCB kuwasafisha mafisadi. Ebu PCCB ituambie ni nani wanaohusika na sakata la RADA na wako wapi na nini kinachuzuia kuwafikisha mahakamani?
 
NCHI IMEUZWA, kaka yangu akiomba rushwa ya elfu 2 hospitali, ni ishu!

SIJUW TUOMBE NYERERE AFUFUKE NA AJE TENA ATUONGOZE!
 
Sitta alishaapa kwamba atadili na Hosea akiukwaa Uspika kwa kosa la kumdhalilisha mke wake. Hapo unategemea Hosea afanye nn!

Ameshindwa kumwajibisha kipindi akiwa spika ndio aweze sasa hivi? Hizo ni promo tu za sitta kijiweka ktk position nzuri ya kuukwaa uspika tena.
 
ameshindwa kumwajibisha kipindi akiwa spika ndio aweze sasa hivi? Hizo ni promo tu za sitta kijiweka ktk position nzuri ya kuukwaa uspika tena.

lakini takukuru kumsafisha sitta siyo promo za hosea kutaka mnyantuzu mwenzake awe chief mjengoni?
 
Hizi zote ni dalilli tu as to why JK was purely a bad choice, kuiba watuibie na tambo juu.Halafu eti TAKUKURU wanakusafisha, Cn these guys be serious? Yaani hivyo viparagraph viwili vitufanye tuamini ni utetezi dhidi ya mabilioni waliyoiba kwenye dili ya rada? Kweli Tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
Uwepo wa TAKUKURU unanitia shaka. kwa tathmini ya harakaharaka tangu iundwe mpaka sasa hakuna kubwa ilichofanya. Mafisaji wakubwa wote hawana hatia!!!
 
Wana JF,

Twaomba Tujua shughuri Kuu muhimu za TAKUKURU ndani na Nje ya nchi hiii?

TAKUKURU leo ndio Chajifanya ndio CIA,FBI,MI6,MOSSAD,KGB,NSA ya Tanzania???? au mbona watakuwa ni wanafiki hawa.

Hivi TAKUKURU wanatuonaje sie WATANZANIA jamani kwa kuwa hatuzi jui sheria au?? jamani hawa wajamaaa nadhani wanatakiwa warudi tena Darasani kuperuuuzi na Kudadisi kuona kama watanzani ni mazuzu kiasi hicho.

SFO walituma report huku TZ na hakuna hata tume imeundwa kwenda UK kujiridhisha kwa madai hayo na kama iliundwa basi ni kinyume na katiba ya nchi na kulikuwa kuna jambo ndani la kumlinda mtu hapo.

Chenge kama yeye alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali for 10yrs lazima tu katika vifungu vyetu vya sheria kwa muji wa Katiba kuna mahali tuu lazima aitwe na jopo la watu na kujibu tuhuma hizi lakini hili halijawahi fanyika ni kuwa alijiuzuru kwanini? kwasababu kulikuwa na kashifa za RADA na unapo jiuzuru ni jukumu la serikali kuunda jopo la tume fulani kufanya uchunguzi juu ya jambo ambalo lilimfanya Chenge ajiuzuru wadhifa wake wa Uwaziri na tupewe majibu ya tume hiyo mpaka leo hola hakuna kitu wametupiga chenga.

Mbali na hilo Chenge kuwa M/Kitiu wa Maadili CCM duuuuh jamani hili ni zito zaidi mbona huu mfumo wa CCM unatuchanganya sana ati?? katika Chakachua yao si ndio jamaa hapa atamaliza Sitta. Maana huyu jamaa amedhamilia kuua upinzani na kutaka kuitetea CCM huko bungeni na kuilinda serikali.

Kutokana na matatizo aliyo nayo mahakamani ya Kuendesha gari kutokuwa na bima kwa mtu mkubwa kama yeye,Kugonga bajaji na kusababisha vifo vya dada wawili wa mwanza na mmoja wapo walikuwa wanafahamiana nae sana, kesi ya RADA. Kwa halii kamati ya maadili CCM itafanyaje sasa kama M/Kiti wao ni Mgombea Uspika na anatuhuma je atatakiwa kujivua hicho cheo nae kupingia kwenye kitimutimu cha kuchunguzwa maadili??
 
TAKUKURU wanatufanya kama hamnazo Watanzania wote. Walitakiwa tu wamsimamishe Chenge mahakamani aeleze ile akiba nono ya dola milioni moja aliipataje ili ajisafishe yeye mwenyewe. Badala wanabaki kumkingia kifua na kumfanya aendelee kutamba anavyotaka. Nchi hii wanaopaswa kuwa JELA ndio viongozi wetu wakubwa, matajiri wazawa na watu wanaoheshimika sana. Tutafanyaje? Ballot box imeshindwa!?
 
%$^^&~!!@##$%###@@@@@@@@@#%^^&*)(**&&**^*&^%^^&^$%^$%^%++_=-$#%^$#<><?:":|"::{P)(&*&^^^*^%#$@!@!~~#$%^&^:doh::doh::A S angry::A S angry:
 
Mithali 19:21
Kuna mipango(hila) mingi moyoni mwa mwanadamu lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.
 
Duh! yani ninachoona hapa kuna njama za kulazimishia
Chenge kuwa spika. Sababu naamini kabisa uchunguz wa pccb ulifanyika siku nying sana, sasa kwa nii mda wote hawakutoa hiyo taarifa yao? Hadi kipindi hiki chenge anagombea uspika ndio wana toa taarifa ya kumsafisha, huu ni usanii totally
 
Tukuru wanapingana na sfo?

Hosea anatumiwa, kama alivyotumiwa na EL katika kashfa ya Richmond. Ni dhahiri anasema uongo kuhusu SFO. Ni bora asingeitaja SFO katika kujenga hoja yake ya kumsafisha Chenge. Someni stori hii hapa chini imetoka katika Mwananchi ya leo na nimeweka msisitizo kwenye red.




Takukuru wamsafisha na kashfa ya ufisadi

Ramadhan Semtawa

TAASISI ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jana iliwasha moto mpya baada ya kutoa taarifa inayoeleza kuwa mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge hakuhusika kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, ikiwa ni siku moja baada ya mbunge huyo wa Bariadi Magharibi kutamba kuwa hahusiki.

Takukuru ilisababisha kizaazaa kama hicho mwishoni mwa mwaka 2007 wakati ilipotoa taarifa ya uchunguzi wa kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji wa umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development, ikielezea kuwa hakukuwepo na harufu ya rushwa kwenye tenda hiyo, jambo lililolifanya Bunge licharuke na kuunda kamati yake teule iliyofichua uozo mkubwa.

Taarifa ya kamati hiyo teule ya Bunge ilisababisha Edward Lowassa ajiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu na kufuatiwa na mawaziri wawili waliowahi kushika Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.

Wakati kashfa hiyo ikielekea kutulia, Takukuru jana ilitoa taarifa inayomsafisha mbunge huyo mteule wa Bariadi Magharibi katika kipindi ambacho Chenge ametangaza kuwania kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri, ambalo liliibua kashfa nyingi katika kipindi chake cha miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Takukuru iliyotolewa jana na afisa habari wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani uchunguzi wake kuhusu kashfa hiyo pamoja na ule uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza, umeshindwa kumhusisha Chenge na kashfa hiyo ya rada.

"Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa Rada umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge, katika tuhuma hizo," inasema taarifa hiyo fupi yenye aya mbili.

Kapwani ambaye alizingumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Takukuru, inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hicho kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na rushwa kwa kuwa jukumu hilo ni la wote.

Mwananchi ilipomuuliza mkurugenzi huyo mkuu wa Takukuru, Edward Hoseah sababu za kutoa taarifa hiyo sasa wakati uchunguzi ulikamilika tangu Februari, hakutaka kutoa ufafanuzi na badala yake alisema: "Nadhani afisa habari wangu amekwishatoa taarifa. Ni vigumu yeye aseme halafu na mimi niseme."

Hata hivyo, taarifa ya SFO kuhusu kumalizika kwa uchunguzi huo iliweka bayana kuwepo na ufisadi ambao ulifanyika kwa kutumia ujanja wa kutotunza kumbukumbu za fedha na hivyo kampuni ya BAE System, ambayo iliiuzia Tanzania rada hiyo kukiri kosa hilo na kulazimika kulipa faini ya pauni milioni 30 ambazo zinatakiwa zitolewe kwa taasisi za hisani za kusaidia Watanzania.

Pia serikali za nchi husika kwenye sakata hilo zilitakiwa kufanya uchunguzi wake na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa, kitu ambacho Tanzaania iliahidi kukitekeleza lakini ikitaka fedha hizo za faini zisiende kwa taasisi zisizo za kiserikali.

Hata hivyo, hakuna taarifa zozote zilizotolewa na serikali baada ya kumalizika kwa uchunguzi huo hadi juzi wakati Chenge alipotangaza kuwa hahusiki na kufuatiwa na taarifa hiyo ya Takukuru.

Chenge alitajwa kwenye kashfa hiyo, iliyotikisa Bunge la Uingereza, baada ya SFO kubaini kuwa alikuwa amehifadhi takriban Sh1.2 bilioni kwenye akaunti yake ya benki moja ya nje ya nchi. SFO ilibaini akaunti hiyo wakati ikifuatilia mzunguko wa fedha zilizonunua rada hiyo.

Baada ya SFo kutangaza matokeo ya uchunguzi huo, Chenge alilazimika kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Miundombinu na alipoongea na waandishi wa habari alisema kiasi hicho cha fedha ni "vijisenti tu".

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliahidi kuwa serikali ingewashughulikia wote waliohusika baada ya Kampuni ya BAE Systems kutangaza matokeo ya uchunguzi wa kashfa hiyo.

Siku hiyo, Februari 9, Membe alisema: "Lazima tulifikishe suala hili mwisho; yaani lazima tujisafishe... tukae vizuri ili tuonekane kwamba mashimo yote ya rushwa yamefukiwa. Na kama kuna mtu yeyote amehusika katika kashfa hii, hiki ndicho kipindi ambacho utawala bora wa Tanzania unatakiwa kuimarishwa."

Juzi katika mkutano wake na waandiashi wa habari kuhusu sababu zilizomsukuma kuwania kiti cha Spika wa Bunge la Muungano na kufafanua kuhusu "makandokando" yanayozunguka jina lake, Chenge alitamba akisema: "Ninavyojua mimi, SFO wamelifunga jalada la rada. Kuweni na ujasiri kwenda kuuliza Takukuru na DPP, mkishindwa mkome kulihusisha jina langu na rushwa ya rada."

Taarifa hiyo Chenge inamaanisha kuwa alishakuwa na habari kuhusu msimamo wa Takukuru kwenye kashfa hiyo.

Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP), Eliezer Feleshi hakuweza kuzungumzia suala hilo jana kwa madai kuwa alikuwa kikaoni na hata alipofuatwa ofisini, aligoma kuzungumzia suala hilo.
 
Ni ajabu chombo cha umma kutoa taarifa kama hizo ikiwa tu kuna kiongozi anataka kugombea uongozi ktk ofisi vyeti kabisa nchini. PCCB mlitakiwa kutoa taarifa hizi kipindi tu mlipo maliza upelelezi wenu. Naona kwangu haiingia kwa kichwa.
 
Jamani, Mkiona mambo ni hivyo mjue Hoseah kaagizwa na aliyemteua (JK), NA MKIONA Hivyo mjue anayegombea usipika ni (Lowassa, Rostam na JK) Kupitia kwa Chenge, haingii akilini kwamba Hoseah anaweza kutoa taarifa kama hii wakati ikulu haina habari.
 
NDIO UTAWALA WA CCM HUO .........................HALAFU ETI WATU WANAPIGA MAKOFI NA KUSHANGILIA CCM IMESHINDA - HAWAJUI KUWA CCM KUTAWALA = HAKUNA UONGOZI, KILA KIONGOZI WA CCM ANAFANYA ANAVYOTAKA

LAKINI - huwezi kumwaga damu ya mtu ukawa salama; Huwezi kuiba jasho la walipa kodi watanzania ukawa salama - IKO SIKU DAMU ZA WATU, JASHO LA WATANZANIA - LITAWAKABA KOONI NA WATASHINDWA KUPUMUA - MUNGU YUPO, ANAONA NA ANAJIBU
 
Back
Top Bottom