.........huku ndiko tunakoelekea, kwa jinsi mambo yanavyoenda hivi sasa hapa nchini hatuna jinsi!HII NCHI INA KAZI, kuikomboa inahitajika vita kubwa
Nafikiri kirefu hiki kimetulia zaidi, ingawa hakionyeshi kama kupamba rushwa ndiyo kusafisha wala rushwa!! je wana JF twaweza kukubaliana na kirefu rasmi cha taasisi hii?
Hii mijamaa ya ovyo kweli kweli, haina hata utu wala mishipa ya huruma kwa Watanganyika wanyonge wanaoibibiwa rasilimali za nchi yao kila siku! Hivi huyu hosea alizaliwa na mwanamke kweli? mbona mi namuona mtu feki sana? Hiyo Doctorate imepatikana je? au ametunukiwa na Mamet kile chuo cha Rostam na Salva Rweyemamu
Kwa sababu anagombea uspika ili akawalinde mafisadi bungeni.Kwanini hii taarifa itoke sasa wakati huyu fisadi anagombea kuwa spika? Mafisadi wanaendelea kulindana lakini upo mwisho wao.
Tiba
Politics za Tanzania ni kama michezo ya kuigiza ya comedy. Juzi juzi Kikwete aliwanadi washutumiwa wa kesi za ufisadi kuwa ni viongozi safi. Leo baada ya 'ushindi' na kuwa raisi, wanamtaka Chenge awe Speaker ili azuie mijadala ya ufisadi bungeni. Ghafla taasisi ya kuzuia rushwa inatokea sawia na kusema kuwa Chenge hahusiki na kashfa ya radar. What a coincidence.
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuonyeshwa huu mchezo ambao kusema kweli hauchekeshi bali ni mchezo wa mauti kwa Watanzania wengi. Poleni sana wale ambao hawakumchagua Kikwete, maana athari zake ndio zinaanza kujitokeza, hata juma halijapita tangu matokeo ya uchaguzi yatangazwe. Poleni sana, tena sana wale mliotaka kuondoa utawala wa kifisadi, lakini wakashinda kwa kutumia ufedhuli na nguvu za dola.
Hii michezo ya kuigiza ndio inaanza. Huu wa kwanza ni curtain raiser tu. Kuna mingine mingi inakuja, na sipendi kufikiri kuwa baada ya miaka mitano hali ya Watanzania itakuwaje. :A S angry:
..............waliokuwa wanautetea utawala ni kuwa wanafaidika nao!...Halafu kuna Mazumbukuku humu ndani hata hayaelewi kwa nini tulikuwa tunataka kuung'oa huu Utawala na yanautetea kwa nguvu na akili zao zote.
Bosi wa TAKUKURU Dk. Edward Hosea
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA
Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.
TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.
Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam.
Simu: 2150043-6/2150360
Nukushi: (022) 2150047
Baruapepe:dgeneral@pccb.go.tz
Mtandao Prevention and Combating of Corruption Bureau
Waandishi wa habari walio makini wanawezawasiliana na SFO kupata toka kwao wanasemaje. Nafikiri watapata full story ilivyokuwa. Uzuri wazungu hawana siri. Wanaweza wakasema wameachana na uchunguzi sababu hawajapata ushirikiano toka Tz.
Kama Chenge kaachiwa, Idrisa Rashid vipi?
Na je Hebu angalia mambo yalivyokuwa kwenye hii link
http://www.facebook.com/l.php?u=http%3A%2F%2Fwww.scribd.com%2Fdoc%2F11490017%2FSFO-Report-on-the-Radar-Saga&h=73ba5
Kweli SIRIKALI yetu hii kiboko (Source Global Publisher)