TAKUKURU: Chenge hahusiki na tuhuma za RADA

Hawa takukuru wapumbavu sana,yani kwa vile huyu Chenge anaandaliwa kuwa spika wanajifanya kuja kumsafisha wakati wao sio walio fanya uchunguzi.


Watanzania tumekwisha na sasa mafisadi wanatuandalia kifo chetu rasmi kwa kumueka huyu jamaa kuwa spika.

mods naomba msim-ban mtu yoyote kama atamwaga matusi kwenye hii thread manake ina kera mno na ndio njia rahisi yakutoa frustrations zetu za hawa mashetani wanao taka kututawala kwa mabavu.
 
Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.

Why now...................na kama Chenge hahusiki ni nani anahusika?..........................Takukuru walisema Richmond siyo Rushwa lakini bunge likasema ni yenyewe.................Nobody in his right frame of mind will believe Takukuru nonsense................Utamu wa mwanaadamu ni kuwa kunakufa basi huko hakuna kuchakachua.......

 
Hii taarifa wangetoa SFO ningeamini. Lakini siyo taasisi hii ya kulinda mafisadi ndani ya CCM! By the way si PCCB ndiyo ilikuja na kitu cha namna hii kumsafisha Lowassa?

Mkuu SFO hawawezi kwenda kinyume na taarifa yao ya mwanzo kwani walichukua mda kuifanya na wengine walisha hukumiwa huyu kapona kwa vile wenzake wamemlinda nchini kwetu.


Anasafishwa kwa vile yeye ndio spika wetu wa bunge lijalo hili aende kuizima mijadala yote ya maovu kwa watanzania.
 
SFO waliwahi kusema wanao ushahidi wa kumpandisha Chenge mahakamani. Takukuru wanapinga hili? Ngoja nitafute link husika na nina hakika hwajatoa another statement ya kurefute hiyo ya kwanza!
 
Na Mkuu wetu wa kaya, baada ya kupata mtikiso katika uchaguzi kutokana na jinsi alivyosimamia ufisadi anaruhusu kamchezo haka kaendelee?
 
Why now...................na kama Chenge hahusiki ni nani anahusika?..........................Takukuru walisema Richmond siyo Rushwa lakini bunge likasema ni yenyewe.................Nobody in his right frame of mind will believe Takukuru nonsense................Utamu wa mwanaadamu ni kuwa kunakufa basi huko hakuna kuchakachua.......


Huyo ndiye Hosea, polisi namba moja, mwanasheria wa shahada 3, aliyekabidhiwa taifa alilinde dhidi ya vitendo na mielekeo ya rushwa (yaani kuzuia) na kuishinda(kupambana). Why now! Kwa sababu wanataka Chenge aende mjengoni kama Spika, na sitashangaa EL kuwa Waziri Mkuu, na Rostam waziri wa fedha....

Taasisi zetu za kiserikali hazina tamaduni yeyote, maana taasisi ni sura za watu! Ukimwondoa Hosea, taasisi yake inaweza ikawa tofauti kutegemea ni nani umemweka. NI NANI ANAWEZA KUNIBISHIA KAMA NIKISEMA WATU WALIOKABIDHIWA TAASISI ZETU NI WACHAFU!!!?
 
jamani jamani jamani Kikwete, nakuombea Kikombe hiki kikupite maana mafisadi wanavyojipanga, wataisambaratisha nchi yetu mbele ya macho yako!! Hizo kura Milion 5 ulizopata zilitoka kwa watu ambao hawakuwa na uhakika kama wewe ni sehemu ya mafisadi, lakini haka ka mchezo ka TAKAKURU ka kumsafisha Chenge kama walivyokuwa wamemsafisha Rich wa monduli ukijumlisha na jinsi walivyo wakalia shingoni Wabunge waliokuwa wamejipambanua kama wapambanaji dhidi ya Mafisadi, kataathiri utawala wako sasa.
Nakuombea pamoja na kutokukupigia kura umalize ngwe hii salama na nchi yetu utuachie ikiwa salama.
 
Samahani Bw Hosea, unaipeleka nchi hii pabaya kutokana na pesa za wachache:

SFO: Hivi ndivyo Chenge alihusika kashfa ya rada

Achunguzwa na vigogo wengine saba
Makachero wadai ana kesi nzito ya kujibu


Wakati kampuni ya kutengeneza zana za kijeshi ya Uingereza, BAE Systems, imekubali kulipa faini ya Dola za Marekani milioni 450 ili kumaliza kesi mbalimbali zilizokuwa inaikabili kutokana na udanganyifu wa kuuza zana za kujeshi kwa nchi kadhaa duniani Tanzania ikiwamo, suala hilo linamweka njia panda aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kutokana na suala la kuhusika kwake kwenye kashfa hiyo kurejeshwa mikononi mwa serikali.

BAE Systems imeamua kulipa kiasi hicho cha fedha ili kumaliza kesi zilizofunguliwa dhidi yake na Ofisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) pamoja na Wizara ya Sheria ya Marekani.

Katika fedha hizo, Wizara ya Sheria ya Marekani italipwa Dola milioni 400, wakati SFO watalipwa Dola milioni 47.

Fedha za SFO zitakwenda kwa nchi ambazo zilikuwa zikiendesha uchunguzi kuhusu biashara zilizofanywa na BAE System ikiwamo Tanzania, Jamhuri ya Czech, Romania na Afrika Kusini.

Wakati BAE wanakiri kuboronga mambo kwa kuwasilisha taarifa za uongo kwa serikali ya Marekani kuhusu biashara ya zana za kijeshi na jinsi ya kuepukana na rushwa, kwa Tanzania inakiri kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi kuhusu biashara ya kuiuzia Tanzania rada mwaka 1999.

BAE Sytems inakiri kwamba kwa kuboronga mambo katika uuzaji wa rada kwa Tanzania, inaridhia kulipa fidia ya Pauni milioni 30, sehemu ya kiasi hicho kikiwa ni msaada kwa ajili ya Tanzania.

Hatua hizi mpya za BAE System sasa zinaacha mamlaka za Tanzania katika mtihani mgumu ambao hazikutarajia hasa kutokana na uchunguzi wake kuwagusa baadhi ya wakubwa nchini akiwamo Chenge na Dk. Idris Rashidi.

Katika uchunguzi wa SFO dhidi ya Chenge, yafuatayo ndiyo yaliwekwa bayana kuwa ni tuhuma mahususi kwa mbunge huyo wa Bariadi Magharibi ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu Aprili 2008 baada ya SFO kufichua kuwa amejihifadhia kitita cha zaidi ya Dola milioni moja (Sh. bilioni 1.2) katika akaunti kisiwani New Jersey kikihusishwa na rada hiyo.

Ripoti kamili ya uchunguzi
Barua ya Machi 21 mwaka 2008 iliyoandikwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa (SFO), kwenda Mwanasheria Mkuu wa Tanzania inasema.

Mpendwa Mwanasheria Mkuu wa serikali,
Yahusu: Bae Systems PLC, Red Diamond Trading Ltd & Merlin International Ltd, Envers Ltd, Tanil Kumar Chandulal, Somaiya, Shailish Pragji Vithlani, Andrew Chenge na wengineo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa (SFO) anawasilisha kwa Mamlaka za Kisheria za Tanzania na hususan Mwanasheria Mkuu, taarifa hii ili kupata msaada utakaowezesha uchunguzi zaidi wa tuhuma kuhusu makosa makubwa yaliyofanyika nchini Uingereza.

SFO iliundwa kutokana na Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 1987 (CJA 1987) na ikaanza kufanya kazi Aprili 6 mwaka 1988. Chini ya CJA 1987, mkurugenzi wa SFO anaweza kuchunguza na kufungua mashitaka ya jinai dhidi ya tuhuma atakazoona ni kubwa na nzito zilizofanywa nchini Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini. Mkurugenzi anafanya kazi chini ya uangalizi wa Mwanasheria Mkuu wa Uingereza na Wales.

Wanasheria katika taasisi hii (SFO) wana nguvu sawa kama wanavyopewa na mkurugenzi katika kuchunguza, kufungua na kuendesha mwenendo wa kesi. Mimi (Matthew Cowie) ni mwanasheria na nimeteuliwa na mkurugenzi kuwa msimamizi mkuu wa kesi hii ambayo kwayo tunaleta maombi haya ya kutaka msaada wako.

Watuhumiwa
SFO kwa kushirikiana na Wizara ya Polisi na Ulinzi (MDF) tunachunguza taasisi na watu wafuatao: Wa kwanza ni Bae System PLC, yenye makazi yake namba 6 Carlton Gardens, London, wa pili ni Michael Peter Rouse aliyezaliwa Januari 29, mwaka 1948. Anaishi nyumba namba 26 Badgers Hill, Virginia Water, Surrey.

Watatu ni Sir Richard Harry Evans (aliyezaliwa Julai 9 mwaka 1942). Yeye anaishi Hallcross Manor, Lancashire. Wa nne ni Michale John Turner aliyezaliwa Agosti 5 mwaka 1948 ambaye kwa sasa anaishi namba 79 Fairmile Lane, Cobham, Surrey wakati Julia Aldridge aliyezaliwa Machi 31, 1957 ni mtuhumiwa wa tano. Yeye anaishi nyumba namba 102, Barabara ya Forest, Liss, Hampshire, Uingereza.

Mtuhumiwa wa sita ni Andrew John Chenge (aliyezaliwa Desemba 24, mwaka 1946) mkazi wa nyumba namba 546 katika Barabara ya Ghuba, Oyster Bay, S.L.P 11 958 Dar es Salaam, Tanzania, wa saba ni Tanil Kumar Chandulal Somaiya (aliyezaliwa Julai 7 mwaka 1965) mwenye hati ya kusafiria namba A 0163862. Barua zake zinapitia Merlin International Limited, Ghorofa ya 1. Avalon House, Barabara ya Zanaki, S.L.P 4013, Dar es Salaam, Tanzania na tisa ni Shailesh Pragji Vithilan. Akiwa amezaliwa Oktoba 3, mwaka 1964 ana hati ya kusafiria namba B 404501 barua zake hupitia kwa Merlin International Limited, Ghorofa ya 1. Avalon House, Barabara ya Zanaki, S.L.P 4013, Dar es Salaam, Tanzania.

(Hata hivyo mtuhumiwa namba saba hatajwi)

Makosa ya Jinai wanayotuhumiwa
Uingereza ni moja ya nchi zilizotia saini Mkutano wa mwaka 1997 juu ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo katika Kudhibiti Rushwa inayofanywa na maofisa wa umma wa Kimataifa katika Biashara. Mwezi Desemba mwaka 2001, Uingereza ilianza kutekeleza azimio hilo kwa kuanzisha Sehemu ya 12 ya Sheria dhidi ya Ugaidi, Makosa na Usalama ya mwaka 2001 (2001 Act). Sheria hiyo ya mwaka 2001 iliifanyia marekebisho Sheria ya Uzuiaji Rushwa ya mwaka 1906 kwa malengo ya kuiwezesha serikali kupanua wigo hadi nje ya mipaka. Vifungu vya marekebisho ya sheria ya Kuzuia Rushwa ya mwaka 1906 vilianza kutumika rasmi nchini Uingereza Februari 14 mwaka 2002.

Kuna sababu kadhaa zinazotufanya tuamini kwamba watu wote waliotajwa hapo juu pamoja na makampuni wamefanya makosa ya kupokea ama kutoa rushwa kinyume cha kifungu namba 1 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa ya mwaka 1906.

Kiwango cha juu cha adhabu ya mtu anayepatikana na makosa haya ya rushwa ni kifungo cha miaka saba jela.

SFO na Wizara ya Polisi na Ulinzi ilipata habari kwamba kulikuwa na uchunguzi wa ndani kuhusu tuhuma za rushwa katika mchakato wa Bae kuiuzia serikali ya Tanzania rada ya kuongezea ndege. SFO kwa upande mwingine, inaendelea kufanya kazi sambamba na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Ukweli kuhusu hili ‘dili'
Katika kujua nini hasa kilijiri katika mchakato mzima wa kuuziana rada hii, SFO iliomba maelezo kupitia barua zifuatazo:

Barua ya maombi ya Juni 13 mwaka 2006, Barua ya nyongeza ya maombi ya Machi 14 mwaka 2007 na Barua nyingine ya Nyongeza ya Maombi ya Oktoba 1, mwaka 2007.

Yaliyojulikana
Mwaka 1999 Bae iliingia katika mkataba wa kuuza rada na vifaa vyake kwa Serikali ya Tanzania. Rada hiyo ilitakiwa ifanye kazi katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Kadhalika rada hiyo ilikuwa na uwezo wa kuongoza ndege za kiraia na za kijeshi.

Bei ya ununuzi wa rada hiyo ilikuwa Dola za Marekani milioni 40. Kilichogundulika ni kwamba mpango wa kununua rada kwa ajili ya Tanzania ambao uliihusisha Bae ulianza mwaka 1992, lakini wakati huo ukifanywa na kampuni ya Siemens Plessey Systems (SPS). Katika kipindi hicho, serikali ya Tanzania ilikuwa inataka kununua vifaa vya kijeshi kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 88.

Bae iliichukua kazi za SPS Oktoba 1997 na kurithi mipango iliyokuwa ikiendelea ambayo sasa ilikuwa katika hatua ya juu. Hata baada ya bei ya rada kupunguzwa hadi dola milioni 40, mauzo haya yaliendelea kupingwa na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha Duniani (IMF) pamoja na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa na Ofisi ya Mambo ya Nje za Uingereza. Pamoja na pingamizi hilo, kwa mshangao wa wengi, Bae ilipewa leseni ya kusafirisha rada hiyo na mkataba huo wa mauziano ukaridhiwa.

Mawakala wa Tanzania: Envers na Shailesh Vithlan
Mwaka 1999, Bae kupitia kampuni ya Red Diamond Trading Limited, kampuni iliyosajiliwa katika kisiwa cha Virgin, Uingereza, iliingia katika makubaliano na kampuni iliyosajaliwa Panama ya Envers Trading Corporation. Envers ilijitambulisha kama wakala anayefanya kazi Tanzania. Mawakala hawa waliwahi pia kufanya kazi na SPS na waliendelea kufanya kazi hata baada ya shughuli za SPS kuchukuliwa na Bae. Nyaraka zilizotolewa kwa SFO zinaonyesha kwamba Envers ilikuwa inatakiwa kupata kamisheni (cha juu) ya asilimia 30 ya mauzo ya rada hiyo.

Katika uchunguzi wa SFO, imegundulika kwamba Tanil Jumar Chandulal Somaiya na Shailesh Pragji Vithlani, walikuwa na nguvu za kufanya maamuzi ya kisheria katika Envers na walifanya kazi kupitia anuani inayohusisha kampuni ya Merlin International Limited (Merlin) yenye makazi yake Dar es Salaam.

Kati ya Januari 2000 na Aprili 2005 zaidi ya Dola milioni 8 zililipwa na Bae kwa Envers kupitia Red Diamond. Malipo haya yaliendelea licha ya kuanza kwa kutumika kwa Sheria dhidi ya Ugaidi, Makosa ya Jinai na Usalama ya mwaka 2001 hadi pale makubaliano baina ya Red Diamond na Envers yalipositishwa rasmi Desemba mwaka 2005 baada ya kulipana Dola 3,362,250.

Inajulikana kutokana na nyaraka ambazo SFO ilipata kutoka Bae kwamba Vithlani alikuwa anahusika katika sakata hili kama wakala wa SPS katika hatua za mwanzo za mchakato wa ‘dili' hili. Lakini hakuna maandishi yoyote kutoka kwa Vithlani yaliyopatikana kuonyesha malipo aliyolipwa, lakini taarifa kutoka kwa mtu aliye karibu na Vithlani zinaonyesha kwamba hakuwa mtaalamu wa rada wala mjuzi wa mambo ya biashara kuonyesha umuhimu wake katika suala hili kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Kwa sasa SFO inaona kwamba Vithlani alikuwa na kazi maalum ya kuwalipa ‘cha juu' maofisa wa serikali ya Tanzania wenye maamuzi muhimu kuhusu ununuzi wa rada hii. SFO inaamini kutokana na nyaraka ilizo nazo kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew Chenge, alikuwa ni mmoja wa watu muhimu kwa Vithlani kuwapa malipo kama mlungula kutokana na umuhimu wa maamuzi na mapendekezo yao kwa serikali.

Andrew John Chenge
Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania kati ya mwaka 1995–2006. Katika kipindi hiki, Bae na SPS walikuwa wanaendelea na mazungumzo kuhusu mauzo ya rada kwa ajili ya Uwanja wa Ndage wa Dar es Salaam na Serikali ya Tanzania. Chenge alihusika katika suala hili kwa namna mbalimbali, hususan kuhusu malipo ya ununuzi wa rada.

Kwa kifupi, ili kufikia makubaliano ya kulipia rada, ilikuwa ni lazima kuwepo na kujiridhisha kwamba mauzo hayo yalikuwa sahihi. Kwa mantiki hiyo, bila Mwanasheria Mkuu kukubali, malipo ya rada ambayo yalifanywa kupitia benki ya Barclays yasingeweza kufanyika. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilitakiwa kutoa maoni yake na kisha kukubali malipo yafanyike ama kukataa.

Umuhimu wa namna ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilivyoshughulikia sakata hili unaonekana pia katika barua ya Juni 16, mwaka 2005 kutoka kwa maneja mauzo wa SPS, Naqvi pale anaposema:

"Kile kinachoendelea kuwa muhimu, ni hitaji la Mwanasheria Mkuu kuhusu kuona mkataba halisi wa mauziano haya."

Nyaraka ambazo SFO inazo zinaonyesha kwamba Juni 29, mwaka 1995 Mwanasheria Mkuu yeye mwenyewe (Chenge) alishiriki katika mazungumzo ya mauziano ya hii rada. Kutoka siku hiyo, ushiriki wa Mwanasheria Mkuu katika mchakato mzima wa malipo kuhusu rada hii unatajwa katika nyaraka nyingi za ndani ya SPS.

Kati ya mwaka 1996 na 1997 mchakato mzima wa kuuziana rada hii ulikuwa inaelekea ukingoni.

Taarifa zilizopatikana kwa mamlaka ya uongozi wa kisiwa cha Jersey kati ya Juni 19 mwaka 1997 na Aprili 17 mwaka 1998 zinaonyesha kwamba kupitia kampuni linayomilikiwa na Chenge ya Franton Investiment Ltd, Chenge alipokea dola za Marekani milioni 1.5 katika akaunti ya kampuni hiyo iliyoko katika benki ya Barclays, tawi la Jersey. Pesa hizi zinaonekana kwamba mapema zilihamishiwa huko kutoka tawi la Barclays la Frankfurt na kupitia nyaraka zingine zilizopatikana kutoka JO Hambro zinazoonyesha kuwa pesa hizo zilianzia benki ya LGT tawi la Liechtenstein. Nyaraka zinasema mlipwaji ni "mmoja wa wateja wetu".

Nafasi ya Vithlani katika kufanikisha mchakato mzima unaonekana katika nyaraka zilizotolewa na wafanyakazi kadhaa wa SPS. Hakuna ubishi kwamba anayetajwa kama "rafiki" au "mtu mnene" katika waraka huu kwa mfano ni Vithlani.

Mark Simpkins wa SPS alisema katika barua iliyotumwa kwa faksi Agosti 30 mwaka 1997:

"Nilikuwa na mazungumzo marefu na rafiki yetu na nilikuwa na mkutano asubuhi hii na Mwanasheria Mkuu ili kupitia masuala muhumu… Tulijadili mpango mzima katika kufikia mkataba halisi. Tumekubaliana kwamba ni muhimu tuwe tumekamilisha mambo yote ifikapo wiki ijayo. Amesema atawajulisha watu wake kinachoendelea. Mtu mnene, kama ninavyosema sasa, alisema ni muhimu kusaini nyongeza katika makubaliano haya… Anasema kwamba ameingia ahadi na wahusika wa zamani na wapya katika mpango huu hasa ikizingatiwa kwamba mchakato mzima umechukua muda mwingi kukamilika…"

Moja ya jambo muhimu katika mpango mzima wa majadiliano ilikuwa uchambuzi wa sheria pale kunapotokea mtafaruku katika mkataba wa mauziano haya. Hili lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa jukumu la Mwanasheria Mkuu.

Septemba 8, mwaka 1997, Simpkins aliandika:
"Pia mwishoni mwa wiki, rafiki yetu mnene alikuwa akijitahidi kushughulikia mambo yote ya kibiashara yanayojitokeza. Asubuhi hii amenijulisha kwamba vikwazo vyote vilivyokuwa vinaonekana kujitokeza amevimaliza kama ifuatavyo (pamoja na mambo mengine):

Sheria: Wamekubali kutumia sheria za Uingereza na Upatanishi wa kisheria (kama utatokea mtafaruku kwenye mkataba) utafanyika Uingereza.

Kutokana na maelezo ya hapo juu inaonekana kwamba ushirika wa Chenge na Vithlani ulipelekea makubaliano hayo ya kisheria ambayo yanaipunguza Barclays hofu ya kupoteza fedha zake kwa kuikopesha Tanzania. Pia inaonekana maelezo kwamba Vithlani ameingia ‘ahadi mpya' ni suala la kutoa rushwa. Na hii pia inaonekana kwenye nyaraka ambazo Vithlani alikuwa anafanya marekebisho mbalimbali ya uwakala wake.

Chanzo: Nipashe of February this year.

 
Mtu anapotangaza kugombea uspika,ndio PCCB wanamsafisha.Nafikiri ni wazi serekali inalea,inawaabudu,kuwalinda na kuwakumbatia hawa.ndio sisi m hiyooooooo.
 
Ndio maana Dr. Slaa alisema anataka wananchi wapige kura kupata Katiba Mpya. Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa sana. Hivi unategemea nini kwa mamlaka ambazo mteuzi wa Wakuu wake ni Rais?

TAKUKURU, TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI na zingine zinazofanana na hizo zote zinafanya maigizo tu!
 
Chenge atetea vijisenti vyake vya Tshs.Billioni 1.6 kuwa ni hela za mayatima!*?

Chenge ambaye alijaribu kuzungumza kwa ujasiri kuhusu kashfa zake, alijikuta akikabiliana na maswali mengi kuhusu tuhuma mbalimbali zinazomkabili na akaishia kuvituhumu baadhi ya vyombo vya habari akidai vinaipeleka nchi kubaya.

"Baadhi ya media (vyombo vya habari) vinalipeleka taifa letu pabaya..., tunachonganisha ndugu kwa mifarakano, mara kuwapachika majina kama mafisadi," alilalamika Chenge.

Kuhusu sehemu alikopata kiwango hicho kikubwa cha fedha wakati akiwa mtumishi wa umma, Chenge alijibu: "Kuhusu wapi nimepata fedha hizo, siwezi kueleza kwa sababu na mimi nina haki zangu kikatiba. Ndiyo maana tunajaza fomu za maadili."

"Kiutaratibu, mtu mwadilifu anapoomba uongozi wa umma huwa anapaswa kutamka mali zake kwa kuwa miongoni mwa sifa zinazombainisha kuwa kiongozi bora ni pamoja na kutokuwa mlarushwa, mwenye kuheshimu mali za umma, muwazi na mkweli.

"Hizi ni fedha za Trust (mfuko). Katika Trust kuna wadhamini na mimi ni mmoja wao kwa upande mmoja na upande mwingine yupo mke wangu Tina Chenge. Kama kuna mtu kasema nimeuza ng'ombe wa ukoo huyo ni yeye."

Chenge alikuwa akizungumzia kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba ambaye baada ya akaunti ya Chenge kukutwa na kiasi hicho cha fedha katika uchunguzi wa SFO, alinukuliwa na gazeti hili akisema "hata mimi sielewi labda kama kauza ng'ombe wao wote wa ukoo".

Chenge alijitetea kuwa fedha hizo zina malengo ambayo ni kusaidia yatima na wasiojiweza, lakini akisita kutaja jina la mfuko wenyewe, mahali ulipo na yeye aliwekeza kiasi gani zaidi ya kusema, "na mimi niliweka fedha zangu humo".

Kuhusu tuhuma za kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu wakati akiwa Mwanasheria Mkuu, mbunge huyo wa Bariadi Mashariki alisema kazi ya Mwanasheria Mkuu ni kuangalia kama mikataba imetimiza masharti ya sheria za nchi na kama imepata baraka za Baraza la Mawazira
na kuongeza kusema "hata waziri mwenye dhamana na sekta fulani hawezi kusaini mkataba bila kupata baraka za Baraza la Mawaziri".

Chenge alitwisha mzigo huo wa kusaini mikataba kwa baraza la mawaziri, wataalamu na hata marais akisema kuwa kutaratibu mikataba haiwezi kusainiwa bila kupita ngazi hizo kwa ajili ya kupata vibali.

Alitoa mfano wa mkataba uzalishaji umeme wa baina ya serikali na kampuni binafsi ya Independent Power Limited (IPTL), akisema ulipata baraka za baraza hilo.

"Baraza la mawaziri liliidhinisha mkataba wa IPTL; kingine ni matatizo ya kitaalamu... kama labda Tanzania ilihitaji megawati 40 kwa dola 100, hilo si suala la kisheria."?!"*

Source:KINYANGANYIRO CHA USPIKA: Chenge aushambulia uongozi wa Spika Sitta
 
Ndugu zangu wana JF nimechukia mpaka majibu yamenikauka.....ee mungu kweli nchi imeuzwa.:sad:
 
Sasa tumefikia mwisho wa kesi zote za ufiusadi ama zilizokuwa mahakamani au zilzokuwa zinachunguzwa !!! Chenge free!!!, Mramba Free!!!, fisadi yeyote uliyewahi kumsikia atakuwa cleansed!!!! Atakayesota jela ni Liyumba tu, na kosa lake kubwa ni kumzidi mzee kwa totoz tu, siyo ufisadi wa mali ya umma wala nini.
 
Back
Top Bottom