Kuna usemi usemao, "An enemy of my enemy is my friend" yaani adui wa adui yangu ni rafiki yangu. Inajulikana wazi kuwa Chenge anao "uadui" wa kisiasa na Sita kwa sababu tu yu kwenye ile kambi akina Sita na wenzake akina Mwakyembe waliyoipiga vita (mafisadi). Vile vile mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU (Dr. Hosea) na Sita hawako "at par" kwa sababu Sita ndiye aliyekuwa Spika wa bunge lililoiagiza serikali imwajibishe kwenye ile kashfa ya Richmond. Dr. Hosea anajua kuwa Sita akirudi kwenye uspika anaweza kutonesha kidonda kwa kuibana serikali kwa lile swala la kumwajibisha. Kwa hiyo logically asingependa arejee uspika. Na kwa Chenge kugombea uspika basi ni faraja kwa Hosea kwa sababu anajua fika kuwa hataendeleza mambo ya Sita.
Katika mazingira hayo haishangazi kabisa TAKUKURU inayoongozwa na Hosea kumtetea Chenge kuwa ni safi. Chenge kama "adui" wa Sita ambaye naye ni "adui" wa Hosea kunamfanya (Chenge) awe "rafiki" yake Hosea. Kwa hiyo katika swala la Chenge na Sita, Hosea hapaswi na siyo halali kusema chochote kwa kuwa ana maslahi nalo. Hosea ni mwanasheria mzuri na kwa hiyo analielewa hilo. Kwa nini huku kutetewa kuwa ni safi kumekuja kipindi hiki Chenge anachogombea uspika? Mwenye macho haambiwi tazama, ni dhahiri kuwa ni kampeni ya kumpandisha kwenye kiti cha uspika, sio vinginevyo.
Jamii inapaswa kuikataa taarifa ya Chenge kwa kuwa ni ya kisiasa, na imetolewa na taasisi inayoongozwa na mtu mwenye maslahi na mhusika. Katika hili hata Hosea mwenyewe anajichafua zaidi. Anaifanya TAKUKUTU ipoteze imani kwa jamii.