Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Nikiwa kama kichwa cha familia, nyumbani kwangu ni sheria zangu, na linapokuja swala la sheria kwa wageni huwa zimekazwa mno kwa wageni wa kiume ambao ni miaka 28+ maaana hawa tayari ni wanauume na asili yetu ni kupambana ili kujitegemea......changamoto za kimaisha na harakati za kiupambanaji wakati mwingine zinapelekea kujikwaa lakini ni mwiko kukata tamaa kusimama kwenye asili yetu huku mipango na malengo vinabakia vichwani mwetu.

Ni takribani wiki 2 zilizopitata nilipata ugeni wa kaka yake mke wangu mwenye miaka 33

Alifika mida ya saa 2 bila taarifa na niwe muwazi kwamba hata mgao wa chakula ulivurugika, namjali sana house girl wangu namchukilia kama mwanafamilia na wife alikuwa kapata ugeni, hivyo ilibidi niende kula mgahawani.

Usiku ule ule tukiwa chumbani nilikuwa namhoji wife kwanini ndugu yake kaja bila taarifa ila nikapotezea nikijua labda atakaa siku 2 au 3.

Kuna vyumba vya wageni vimejitenga na nyumba kuu ndiko tulipompa hifadhi, na choo / bafu ni humo humo.

Sasa ni takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye akitafuta hata shughuli, yani yupo tu.

Wife akimuuliza hali, yeye anasema kaja kutusalimia huwa nabaki kukuna kichwa tu

Asili ya sisi wanauume ni kujitegemea......changamoto za kimaisha na harakati za kiupambanaji wakati mwingine zinapelekea kujikwaa lakini ni mwiko kukata tamaa kusimama kwenye asili yetu huku mipango na malengo vinabakia vichwani mwetu

sasa navyomoona mwanaume mwenzangu yupo comfortable na hali ya kuwa tegemezi na hana tatizo lolote la kumfanya asishughulike, binafsi najisikia vibaya.
 
Ujasimamia nafasi yako kama mwanaume. Inaonyesha tangu amefika hapo kwako, unamkwepa kuzungumza naye, inawezekana labda unajua changamoto zake, hasa fedha; fanya yafuatayo: kesho ukitoka kwenye miangaiko yako, mtoe 'out' kama anakunywa pombe, mnunulie. zungumzeni mambo mbali mbali pamoja na sababu ya yeye kuja kwako.
 
Back
Top Bottom