Taifa maskini linaloongozwa na Sheria zisizofaa. Inaingia akilini kumjengea nyumba aliyehudumu Serikalini miaka zaidi ya 20?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Inakuwaje taifa ambalo toka limepata uhuru uhaba wa madarasa, maji na huduma za afya ni jambo la kawaida, umaskini mkubwa kwa raia wake ni jambo la kawaida halafu bado linakuwa na sheria ambayo ilitungwa na Bunge kuhudumia na kulipa mafao viongozi wakuu wa kisiasa waliostaafu?

Inaingia akilini kumlipa mafao ya kumjengea majumba ya kifahari Rais au Waziri Mkuu ambae alishawahi kuhudumu serikalini zaidi ya miaka ishirini?

Kama Taifa linalojali wananchi wake kwanini hizi pesa zisitumike kuimarisha huduma za afya, elimu na miundombinu ili kuondoa umaskini?

Mtu alihudumu kama waziri kwa miaka ishirini, kisha anakuwa Rais kwa miaka kumi bado tu anahitaji nyumba na gari ya bure? Tena ya mabilioni ya shilingi? Kwa nini asijenge kwa mshahara wake?

My take: Kuna sheria zingine hazifai kuwepo kwenye nchi kama hii ambayo bado sana ipo nyuma kimaendeleo.
 
Acha wale. Wenzako mpaka wanafika hapo wanamwaga damu kwa mikono yao. Refer uchaguzi wa mwaka 2020 October. Usidhani wanafika hapo walipo kwa mteremko. Acha wale. wanastahili. Kazi wanazodanya wewe huziwezi.

Unaweza kuchunja mtu wewe? Kama huwezi kaa kimya.
 
Rais mstaafu anastahili hizi: 80% ya mshahara wa rais aliyepo madarakani; ofisi na wafanyakazi wanaolipwa na serikali; walinzi; gari; matibabu kokote duniani; diplomatic passport; air ticket kila mwaka kwenda popote anapotaka; and yet anajengewa hekalu!
 
Je, Mwalimu alipojengewa Butiama alikuwa amehudumu miaka mingapi? Je JPM alipomjengea JK ulikuwa wapi kuanzisha mada ya kupinga hilo? Ikiwa ulishindwa kuzuia jambo hilo na kulikemea asubuhi hii jioni ndio utaweza? Ama unaandika kujifurahisha? Je huo utamaduni wakugawana keki mliojiwekea chama chenu umebadilika?
 
Walah pigo mlilopata hakika hamtosahau maisha yote, na sasa tuna utawala mpya. Kaeni kwa kutulia hamuwezi hameni NCHI, OVER!!
 
Sheria zingekuwa zinatungwa na wenyeviti wa mitaa/ vijiji au madiwani hii nchi ingekuwa mbali sana,hawa Wabunge wetu fuata upepo shida tupu, wanaumiza meza tu. JPM walikuwa wanampigia makofi SSH wanampigia makofi hata akifanya tofauti na yale aliyopigiwa makofi JPM.
 
Inakuwaje taifa ambalo toka limepata uhuru uhaba wa madarasa, maji na huduma za afya ni jambo la kawaida, umaskini mkubwa kwa raia wake ni jambo la kawaida halafu bado linakuwa na sheria ambayo ilitungwa na Bunge kuhudumia na kulipa mafao viongozi wakuu wa kisiasa waliostaafu?

Inaingia akilini kumlipa mafao ya kumjengea majumba ya kifahari Rais au Waziri Mkuu ambae alishawahi kuhudumu serikalini zaidi ya miaka ishirini?

Kama Taifa linalojali wananchi wake kwanini hizi pesa zisitumike kuimarisha huduma za afya, elimu na miundombinu ili kuondoa umaskini?

Mtu alihudumu kama waziri kwa miaka ishirini, kisha anakuwa Rais kwa miaka kumi bado tu anahitaji nyumba na gari ya bure? Tena ya mabilioni ya shilingi? Kwa nini asijenge kwa mshahara wake?

My take; Kuna sheria zingine hazifai kuwepo kwenye nchi kama hii ambayo bado sana ipo nyuma kimaendeleo.
Wakati anayafanya haya mwendazake mlikuwa mnamshangilia kwa mapambio kuwa ni kiongozi anayewajali watangulizi wake, ila kwa kuwa tu mama hamumpendi mnaanza kumkejeli. Halafu kwa taarifa yako nyumba aliyokabidhiwa kikwete imejengwa enzi za mwendazake. Gari aliyokabidhiwa mzee Ruksa ni hitaji la kikatiba kuwa kila mwaka Rais mstaafu/makamu wa rais na waziri mkuu au familia zao wanapewa gari jipya
 
Inakuwaje taifa ambalo toka limepata uhuru uhaba wa madarasa, maji na huduma za afya ni jambo la kawaida, umaskini mkubwa kwa raia wake ni jambo la kawaida halafu bado linakuwa na sheria ambayo ilitungwa na Bunge kuhudumia na kulipa mafao viongozi wakuu wa kisiasa waliostaafu?

Inaingia akilini kumlipa mafao ya kumjengea majumba ya kifahari Rais au Waziri Mkuu ambae alishawahi kuhudumu serikalini zaidi ya miaka ishirini?

Kama Taifa linalojali wananchi wake kwanini hizi pesa zisitumike kuimarisha huduma za afya, elimu na miundombinu ili kuondoa umaskini?

Mtu alihudumu kama waziri kwa miaka ishirini, kisha anakuwa Rais kwa miaka kumi bado tu anahitaji nyumba na gari ya bure? Tena ya mabilioni ya shilingi? Kwa nini asijenge kwa mshahara wake?

My take: Kuna sheria zingine hazifai kuwepo kwenye nchi kama hii ambayo bado sana ipo nyuma kimaendeleo.
 
J

Jamani haya makite(dogs) yanayopayuka sasa ni wale wale ambao bado hawaamini kuwa SSH ndio rais wetu ,ni kama wamepigwa ganzi na the good side ni kwamba (mzee wa mavi yenu ) israel alisimama na Watanzania
 
Inakuwaje taifa ambalo toka limepata uhuru uhaba wa madarasa, maji na huduma za afya ni jambo la kawaida, umaskini mkubwa kwa raia wake ni jambo la kawaida halafu bado linakuwa na sheria ambayo ilitungwa na Bunge kuhudumia na kulipa mafao viongozi wakuu wa kisiasa waliostaafu?

Inaingia akilini kumlipa mafao ya kumjengea majumba ya kifahari Rais au Waziri Mkuu ambae alishawahi kuhudumu serikalini zaidi ya miaka ishirini?

Kama Taifa linalojali wananchi wake kwanini hizi pesa zisitumike kuimarisha huduma za afya, elimu na miundombinu ili kuondoa umaskini?

Mtu alihudumu kama waziri kwa miaka ishirini, kisha anakuwa Rais kwa miaka kumi bado tu anahitaji nyumba na gari ya bure? Tena ya mabilioni ya shilingi? Kwa nini asijenge kwa mshahara wake?

My take: Kuna sheria zingine hazifai kuwepo kwenye nchi kama hii ambayo bado sana ipo nyuma kimaendeleo.
Mbaya zaidi huyo kiongozi unakuta hakuwa muadilifu, anahusishwa na matendo mengi ya wizi.
 
Eheee Mungu tuokoe sisi watu wako tunaangamia kwa kukosa maarifa
Ninadai milioni 3 Nssf sijalipwa huku kuna mamilioni ya zawadi Mungu uko wapi utuokoe kwani hapa si nyumbani kwetu jamani au ni kwa Jirani tumekua watoto Wa kambo kila miaka. Eheeee Mungu pindua huu udhalimu
 
Back
Top Bottom