Waziri Sitta amlipua Lowassa Bungeni

Waziri Sitta amlipua Lowassa Bungeni

...Sitta ana kashfa ya kutumia mabilioni ya fedha kujenga ofisi ya spika jimboni kwake Urambo kana kwamba alitarajia atakuwa spika wa maisha, na mrithi wake atatoka Urambo.
Itatusaidia sana tukijenga utamaduni wa kuchunguza systemic flaws za mfumo mzima wa uendeshaji mambo badala ya kuangalia symptoms za tatizo tu.

Sitta hana password ya safe box la Hazina, kuna mtu alimpa hizo hela, nani huyo, kwa nini hakuuliza kama makao makuu ya kudumu ya Spika yanahamia Urambo, kiasi gani alimpa, kwa nini, kabla ya kutoka zilikuwa earmarked kwa bajeti gani, Sitta alisema anaenda kufanyia nini, sheria inasemaje, makaratasi yako wapi, mfumo mzima ukoje? Ultimately, si kosa la Sitta kuomba hela na kupewa.
 
nadhani baanda ya kauli hiyo wabunge wa ccm walipiga makofi kama kawaida yao......lakini pia huwa simwamini sita na kwa lile kosa la kuupotezea mjadala wa richmond sitamsamehe........ni mtu wa ajabu na mnafiki mkubwa

Edson tuko page moja, hata mimi huyu jamaa namuona ni mnafiki tu anaangalia upepo unavuma vipi anafuata hakuna lolote, ni wale wale..
 
hawa jamaa natamani siku wazichape kavu kavu then tutajua nani anamaamuzi magumu na nani ni 10%
 
=========

Hapa sina uhakika nani ni pedi kati ya Lowassa na Sitta. Mtumiaji anaeleweka ni Kikwete. Na mtumiaji hana uchaguzi wa pedi. Akiwa na shida ni lazima atumie pedi iliyo karibu. Wakati ule wa nchi ikiwa kwenye giza, Pedi alikuwa Lowassa. Sasa nchi iko gizani, Pedi ni Sitta. Kuna wakati pedi lilikuwa kundi la Lowassa ndani ya NEC likimsulubu Sitta. Ni makosa makubwa kumwamini Kikwete katika habari ya kutumiwa kama pedi. Kila mtu ana zamu yake ya kutumiwa. Kinachohitajika ni pedi zenyewe kujipanga vema, ili Kikwete akizitumia zimletee mwasho mapajani!

Nawasilisha
duh naona umeamua kuweka matumizi ya pedi kwa uzuri zaidi
 
Sawa,Sita kasema hivyo yuko sahihi,ila nimkumbushe neno moja ambalo nae kwa upande wake linamgusa sana kuhusu neno hili maamuzi magumu,yeye na kamati ya akina Mwakyembe walishindwa kusimamia walichowaaminisha watanzania kuhusu kashfa ya richmond mwisho wa siku walipotishwa na chama chao waliufyata na yeye na mwakyembe wameishia kupewa uwaziri kwishney.
 
Wooote hao mwisho wa siku wanatetea matumbo yao na ya jamaa zao
Sawa,Sita kasema hivyo yuko sahihi,ila nimkumbushe neno moja ambalo nae kwa upande wake linamgusa sana kuhusu neno hili maamuzi magumu,yeye na kamati ya akina Mwakyembe walishindwa kusimamia walichowaaminisha watanzania kuhusu kashfa ya richmond mwisho wa siku walipotishwa na chama chao waliufyata na yeye na mwakyembe wameishia kupewa uwaziri kwishney.
 
Itatusaidia sana tukijenga utamaduni wa kuchunguza systemic flaws za mfumo mzima wa uendeshaji mambo badala ya kuangalia symptoms za tatizo tu.

Sitta hana password ya safe box la Hazina, kuna mtu alimpa hizo hela, nani huyo, kwa nini hakuuliza kama makao makuu ya kudumu ya Spika yanahamia Urambo, kiasi gani alimpa, kwa nini, kabla ya kutoka zilikuwa earmarked kwa bajeti gani, Sitta alisema anaenda kufanyia nini, sheria inasemaje, makaratasi yako wapi, mfumo mzima ukoje? Ultimately, si kosa la Sitta kuomba hela na kupewa.

Unajua vitu vingine mkivitetea inaonyesha aidha hujui unachoongea au unafuata ushabiki tu. Kiongozi hachaguliwi kuombaomba fedha kwa matumizi yasiyo na msingi. Ni jukumu la kiongozi kuona kuwa anaomba pesa ambazo zina manufaa kwa watu anaowaongoza. Kusema mbona nilipoomba sikunyimwa ni dalili ya kutojua maana ya uongozi ni nini.

Halafu Sitta na mwenzie Pinda waache kuangalia mtoa hoja, waangalie hoja ni nini. Je si kweli kwamba sasa hivi viongozi wanaogopa kufanya maamuzi magumu? Mfano mzuri ni Sitta na Nape, kama wanaweza kufanya maamuzi magumu walishindwaje kujiunga na CCJ waziwazi wakafanya hivyo chini kwa chini wakati mwenzao Mpendazoe aliweza kutoka waziwazi? Ni Sitta huyo huyo ambaye alimwambia Rais Kikwete kuwa anatakiwa kuwa mkali wakati wa suala la EPA (pale Kikwete alipohutubia bunge), je kumwambia awe mkali maana yake nini kama siyo kumwambia afanye maamuzi magumu?

Je si kweli nchi inatakiwa kujenga reli zetu ili tuweze kufungua biashara na nchi zinazotuzunguka? Je kuzipanua bandari za Mtwara na Tanga siyo jambo la msingi badala ya kufikiria kujenga bandari ya Bagamoyo?

Lowassa ana matatizo yake, lakini viongozi wanafiki jamii ya akina Sitta kujifanya eti wao wasafi hilo ni lazima lipingwe. Halafu orodha ya mafisadi iliyoongezwa na Sitta yumo vile vile. Ni Sitta huyo huyo aliyezuia hotuba ya Kikwete kuhusu EPA isijadiliwe bungeni, sasa kama huo siyo unafiki ni nini?

CCM kama mnaona mvuto kwa wananchi umeisha, ondokeni salama hizo sarakasi zenu za kutaka kuharibu nchi haziwezi kutusaidia.
 
Vita ya panzi huwa ni furaha ya kunguru......
unajua Mr. 6 kamlipua EL kimsingi kwa sababu EL alipokuwa anasema bungeni majuzi kuwa viongozi wasiogope kuchukua maamuzi magumu alimaanisha kuwa kwa nini viongozi hawawachukulii hatua za kuwafukuza kina Mr. 6, ...kembe na ...ape kwa kutofukuzwa katika chama kama wasaliti kwa kuunda SISIJEI wakiwa sisiemu kwa hiyo kila mmoja wao anajiona ni mteule huko sisiemu!!! kiza kimetanda......na kazi ipo
 
SS ana zunga tu yeye alikuwa kwenye rungu alichukua uamuzi upi mgumu au ule wa kumtoa ZITTO bungeni na Serikali yake inafanya uamuzi upi mgumu kwa sasa au kupandisha bei ya mafuta ya taa kuwa sawa na petrol maana baraza la mawari lilipitisha uamuzi huu kujua nani ataumia.
 
Hapa kuna mawili
la kwanza ni ss kulipiza kisasi
la pili inaweza kuwa ni calculated move well known na serikali[/QUOTE]

Ni kweli kabisa ndio mana JK akamteua Six kukaimu ili ammalize rafiki kiaina
 
fafanua kidogo mkuu, wengine tumegawiwa giza mchana. ha ha ha ha!!!!

Pole sana kwa kunyimwa Umeme ndio ahadi za Rais wa CCM umeona wanafanya sherehe ya kuzaliwa kwa TANU badala ya kufanya msiba wa kushindwa kuleta maendeleo miaka 50 sasa hakuna Shule, hakuna ofisi za Serikali tulizojenga hizi zilizopo nzuri ni zilizojengwa na wakoloni, reli aliyoacha Mjerumani umetumika impaka Mhindi kauziwa kuiba vyuma lakini hakuna maendeleo yeyote tokeawalipo oondoka wakaloni
 
Yapo mambo Mengi yanayotukabili na changamoto nyingi sana ziko mbele yetu kama Taifa hasa sisi vijana. Niwakati wetu wakuamua tunataka kwenda watu,kwa njia ipi na kwa sababu zipi,wazee wetu wanaweza kisema,je sisi tunaona nini ktk maneno yao.Wasalaaa wakuu.
 
No one is perfect, lakini kwenye mizani ya nani alifaa kwenye nafasi ya Uwaziri mkuu (kwa changamoto za sasa) kati ya Pinda na Sitta naweza kusema SITTA angefaa zaidi. Walau anaweza kukuangalia machoni akasema yaliyo rohoni mwake, Pinda is a 'thoerist' with no real sense of the challenges on the ground. Na atawaletea shida ccm na serikali unless abadilishe approach. Jambo linalonisumbua kuhusu Pinda ni hili:

1. Kwa nini au kulikuwa na logic gani kwake yeye kupanda ndege kwenda kwenye jimbo la Magufuli na kumkataza 'kusimamia' sheria (bomoabomoa), alishindwa nini kufanya hivyo hapa Dar es Salaam? Why was it important kutoa hilo tangazo Kagera wakati sehemu yenye mabango mengi ni Dar es Salaam?

Hili swala lilijadiliwa sana humu jaribu kutafuta hiyo thread usome Mkuu inamaelezo mengi muhimu sana kwa watu mnapenda kuongelea watu badala ya mambo! Pale Magufuri alichemsha najuwa inawasumbuwa sana wafuasi wake lakini huo ndio ukweli.
 
Yaani hapa siajona Mh.sitta kama kamlipua Lowassa ila kaelezea na kujenga hoja ya Lowassa kama serikali inajua kuna mikataba mibovu ambayo imesainiwa katika mianya ya rushwa kwanini isiwachukulie hatua wale waliohusika?
Pili,Lowasa na wenzake ndio wajulikana ni miungu ya dili chafu na rushwa kwanini hawashtakiwi maana maamuzi magumu nipale watu watakaposhikilia sheria na haki ili kuiongoza Tanzania,Viongozi wafanye hivyo kama wanataka kushindana na Lowassa.
Inaonekana Lowassa na wenzake waogopwa na serikali ya CCM wakiongozwa na Mkulu mwenyewe,Je Lowassa anakitu gani dhidi ya viongozi kiasi cha kuogopwa namna hiyo ........................
 
Itatusaidia sana tukijenga utamaduni wa kuchunguza systemic flaws za mfumo mzima wa uendeshaji mambo badala ya kuangalia symptoms za tatizo tu.

Sitta hana password ya safe box la Hazina, kuna mtu alimpa hizo hela, nani huyo, kwa nini hakuuliza kama makao makuu ya kudumu ya Spika yanahamia Urambo, kiasi gani alimpa, kwa nini, kabla ya kutoka zilikuwa earmarked kwa bajeti gani, Sitta alisema anaenda kufanyia nini, sheria inasemaje, makaratasi yako wapi, mfumo mzima ukoje? Ultimately, si kosa la Sitta kuomba hela na kupewa.

Achana na mpuuzi huyo hata hajui nyumba za Serikali zinajengwa na nani hana faida yoyote kuzaliwa Dunia huyo!
 
Season 3:
Episode 5:
To be continued ..................................
 
Hili swala lilijadiliwa sana humu jaribu kutafuta hiyo thread usome Mkuu inamaelezo mengi muhimu sana kwa watu mnapenda kuongelea watu badala ya mambo! Pale Magufuri alichemsha najuwa inawasumbuwa sana wafuasi wake lakini huo ndio ukweli.
kumbe kusimamia sheria ni kuchemsha! Ndio maana wanamagamba wengi hawapendi kufuata sheria bali "mapokeo" ! Ukweli nikwamba vita vinavyo endelea sasa faida kubwa ni kwa wanamageuzi haijalishi nani ndani ya ccm yuko sawa bado mnufaikaji mkubwa ni mwanamageuzi ningefarijika sana kama angeibuka mwingine na mwingine zaidi kupambana na hoja ya EL
 
Hakuna Rais wa Tanzania kwenye hiyo list yako hapo kwa sababu zifuatazo;

1.Lowassa-Richmond, Dowans,Kaskazini hatoki Rais(Tamko CCM Pwani) na Makundi yake(Atamwaga Ugali)
2.Samuel Sitta-Visa na mikasa ya kukiaibisha chama Bunge la Tisa na makundi yake vs Lowassa(Atamwaga Mboga)
3.Mwandosya -Hana nguvu yoyote ndani ya CCM na hawamuelewi kama Atawalinda au Atawatosa mafisadi wenye CCM
4.Frederick Sumaye-Kaskazini Haitoi Rais,JK analo jina la mgombea(Tamko CCM Pwani) na uozo wake na Mkapa 1995-2005
4.Hussein Mwinyi- Kashfa za mabomu na changamoto za muungano kama uwepo usiwepo zinamnyima nafasi
5.Benard K. Membe- Aaaah!Nani anataka Rais mwingine mswahili na sharobaro muuza sura,Haturudii makosa ya 2005 na 2010.

CCM labda wajaribu J.P Magufuli angalau anaweza kupunguza kura za Rais Mtarajiwa His Excelence Dr.Wilbrod Peter Slaa

hili saga mweisho wake ni 2015 kunye kura za maoni ya kupendekeza jina la urai kupitia ccm, lowasa Vs sita bado wapo wakina mwandosya sumaye mwinyi mdogo na membe kazi ipo
 
Back
Top Bottom