Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,144
- 162,542
Naomba nikwambie kuwa ukiendelea na hii tabia yako ya kupuuza maoni na matakwa ya wengi, kuna siku utakuja kupingwa kwa kuzomewa hadharani na heshima yako itashuka vibaya sana.
Mwaka 2015 ulipindua matakwa ya wanachama wenzako kwa kumpiga chini Marehemu Mzee wa watu na safari hii unafanya yale yale kwa kuwaletea wenzako mgombea wasie mtaka(asietakiwa na wengi) huku ukikiri wazi kuwa mnakosea(kumbuka kukosea ni kukosea tu na hakuna kukosea kidogo kama ulivyosema).
Mzee wangu, tambua unaheshimiwa kwa nafasi kubwa uliowahi kushika katika hii nchi na si vinginevyo. Hivyo, usipojirekebisha, watu hawataendelea kukuvumilia na kuna siku utazomewa iwe ni ukumbini au katika eneo la wazi.
Kwa nafasi yako, unapaswa kuwa mshauri bora kwa chama chako na kwa nchi yako kama alivyokuwa Hayati Mwalimu Nyerere baada ya kustaafu ambapo alikuwa anashauri na kukemea hata hadharani inapobidi.
Nimemaliza.