Tahadhari: Msilipue ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mbezi Louis

luirhu

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
800
412
Baada ya muda mliopewa kwisha jana tarehe 30/11/2020, na ujenzi kutokukamilika bado unaendelea japo kuwa nje ya agizo la Mh. Rais.

Ushauri wangu ni kuwa msilipue kazi bora kuomba muongezwe muda kuliko ku-force halafu mwishowe mkaharibu au ubora ukapotea.

Hiyo ni stendi ya kimataifa ni sawa tu na uwanja wa ndege wa kimataifa maaana ni stendi inayo hudumia mataifa mbalimbali hivyo umakini an ubora ni jambo la kuzingatia, isiwe bora tu kumaliza bali tuone thamani ya fedha zilizotolewa.

KAZI inaendelea.
 
Hivi daladala za Tabata Segerea to Mbezi stend zitakuwepo?

Na

Kivule to Mbezi stend je?
 
TANROAD walisha fungua njia zote kutoka pembe zote za Jiji ni lazima daladala zote zifike Mbezi mwisho, Kwa kifupi Kwa sasa Mbezi itakuwa K/koo no.2 kila kitu sasa unaweza kukamilisha ukifika tu MBEZI
 
Watendaji wote mnao husika na mradi huo nawakumbusha tu mliambiwa msikae maofisini, pigeni kambi hapo hadi kieleweke.
 
Umenena, ni kweli hiyo ni stendi ya mfano Afrika mashariki na kati.

na hakika mapato yataongezeka maradufu na itachochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja moja na nchi kwa ujumla.
 
Baada ya muda mliopewa kwisha jana tarehe 30/11/2020, na ujenzi kutokukamilika bado unaendelea japo kuwa nje ya agizo la Mh. Rais.

Ushauri wangu ni kuwa msilipue kazi bora kuomba muongezwe muda kuliko ku-force halafu mwishowe mkaharibu au ubora ukapotea.

Hiyo ni stendi ya kimataifa ni sawa tu na uwanja wa ndege wa kimataifa maaana ni stendi inayo hudumia mataifa mbalimbali hivyo umakini an ubora ni jambo la kuzingatia, isiwe bora tu kumaliza bali tuone thamani ya fedha zilizotolewa.

KAZI inaendelea.
Yaani ukiangalia Raman ya hiyo stand kwakweli nibongee la stand likikamilik vizuri labda tumuombe
hwmheshimiwa rais awape muda waombe radhi kwa kuxhelewesha mradi ili wamalize kwa kiwango cha Raman yake
 
Back
Top Bottom