Stories of Change - 2023 Competition
Jun 25, 2023
23
21
Miongoni mwa Mikoa ambayo nimewahi kutembelea nchini Tanzania ni Mkoa wa Mwanza 'rock city' ambao umebarikiwa vitu vingi vizuri; Ziwa Victoria lenye samaki pendwa na watamu aina ya Sato na Sangara lakini mbali na Ziwa Victoria, Mkoa wa Mwanza pia umebarikiwa miamba na mawe makubwa (rocks) yenye kulifanya Jiji hili liwe la kuvutia.

Moja kati ya mambo ambayo BWANA YESU KRISTO Ametufundisha ni tofauti kati ya kujenga nyumba juu ya mwamba na juu ya mchanga, ambapo nyumba ijengwayo juu ya mwamba inakuwa imara sana isiyoweza kuanguka kwa mvua, mafuriko wala upepo tofauti na nyumba ijengwayo juu ya mchanga.

"Basi kila asikiaye hayo MANENO YANGU, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo MANENO YANGU asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa." (Mathayo Mtakatifu 7:24-27)

Watu wa Jiji la Mwanza wameamua kutumia NENO HILI kwa kujenga nyumba zao juu ya miamba, lakini swali ni je! Wakati wanajenga nyumba hizi walizingatia suala la UFUNDI, SANAA, UBUNIFU NA TEKNOLOJIA ili wasihatarishe usalama wao?

Tukumbuke Kuwa BWANA YESU KRISTO NI FUNDI, MWANASANAA, MWANATEKNOLOJIA NA MBUNIFU Aliyeshiriki pamoja na MUNGU BABA katika UUMBAJI wa ulimwengu huu tunaoishi. (Mwanzo 1 na Mwanzo 2) (Mithali 8:23-31) (Yohana Mtakatifu 1:1-5) (Marko Mtakatifu 6:2-3)

Tafsiri yake ni kuwa, BWANA YESU KRISTO Aliposema "Basi kila asikiaye hayo MANENO YANGU, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba." (Mathayo Mtakatifu 7:24-25);

Hakumaanisha kuwa ukipata eneo tu lililo juu ya mwamba wewe jenga hata kama kuna pango la wanyama wakali hapana, bali Amemaanisha kuwa ni KWELI eneo zuri la kujenga ni juu ya mwamba, lakini pia kabla ya kujenga itumike HEKIMA YA MUNGU kwa ajili ya usalama wa watu na jamii kwa ujumla.

Kwa namna baadhi ya nyumba za Jiji la Mwanza zilivyojengwa juu ya miamba ni kweli hazitaweza kuangushwa na mvua, mafuriko wala upepo lakini zinaweza kuangushwa na mawe makubwa ambayo yapo maeneo mengi karibu na nyumba hizo pasipo wenyewe kuchukua tahadhari wala kuwaza kuwa mawe hayo hayana mizizi chini ya ardhi hivyo siku yoyote yanaweza kudondoka; hususan mawe makubwa yaliyo juu ya mawe mengine au mawe makubwa yaliyoingia kwa kiasi kidogo ardhini.
IMG_20230710_111204.jpg

Picha kutoka Mtandaoni

Mbali na hatari ya kuangukiwa na mawe, wakazi wa maeneo haya wamezuiwa na mawe haya kupata huduma za miundombinu ya barabara, kwani wanaoishi kwenye hii miamba pia ni wanadamu ambao wana watoto na wana wajawazito lakini pia wana familia zinazohitaji huduma za usafiri ili kufikia huduma za Elimu na Afya pamoja na huduma nyinginezo za kijamii kwa wakati sahihi.

Hatari nyingine ni kutokana na miamba iliyoinuka mpaka kufikia usawa wa ardhi pamoja na uchongaji holela wa miamba kupelekea ngema ndefu nyingi mfano kutoka nyumba ya juu mpaka ya chini au eneo la juu mpaka la chini; hivyo kupelekea hatari kwa watoto wadogo ambao wanaweza kuanguka kwenye ngema hizi pale wanapocheza au kufanya chochote kwenye maisha ya kila siku.
IMG_20230710_111237.jpg

IMG_20230710_111601.jpg

Picha kutoka mtandaoni


Suluhisho

Serikali, Wizara Husika, Wadau wa Maendeleo, Watanzania, Makampuni, Mashirika, Taasisi Mbalimbali, Huduma Mbalimbali na Mtu Mmojammoja tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kuwasaidia kuwaondolea mawe haya ili yakatumike kwenye shughuli nyingine za maendeleo, kisha kuwachongea njia kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kati ya nyumba na nyumba ambapo njia hizo zitaunganishwa pamoja na barabara mojamoja kutoka kule waliko mpaka barabara kubwa za Jijini Mwanza au Kivukoni kwa walio karibu na Ziwa Victoria.

Hii yote ni kwa sababu UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI unahitaji NGUVUKAZI, na siku zote NGUVUKAZI ni wanadamu hivyo KWA UPENDO TU hatutakiwi kusubiri mpaka mawe haya yafanye uharamia kwa wanadamu wenzetu, kwani na wao pia wana nafasi yao na wana sehemu yao katika kulijenga Taifa la Tanzania, Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

Kwa maeneo ya aina hii iwe Mwanza au mkoa wowote mwingine ambayo bado hayajajengwa, unahitajika usimamizi mkubwa, na matumizi ya TEKNOLOJIA, SANAA, UBUNIFU NA UFUNDI WA HALI YA JUU ili kujenga juu ya miamba na maeneo yaliyoinuka kusiwe shubiri kwa wamiliki wa majengo hayo hata kupelekea wengine kukimbia kujenga kwenye maeneo yaliyoinuka na kwenda kujenga mabondeni; bali kujenga kwenye miinuko na miamba kunatakiwa kuwe kivutio kwa watu wengi zaidi kujenga kwenye maeneo hayo ili kuepuka mvua, mafuriko na upepo kuangusha nyumba zao taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa sana na vyombo vyetu vya habari hususan nyakati za masika wakati tuna maeneo mazuri yenye miamba na yaliyoinuka kwa ajili ya shughuli za ujenzi kama vile ambavyo maeneo mbalimbali duniani yameweza kutumia TEKNOLOJIA, SANAA, UBUNIFU NA UFUNDI MZURI kujenga nyumba na majengo mengine mahali penye miamba na miinuko kwa utaratibu mzuri usiowanyima haki zao za msingi za kijamii wamiliki na wakazi wa kwenye nyumba hizo, wala usiotishia na kuhatarisha Usalama wao.

IMG_20230710_111141.jpg

IMG_20230710_111341.jpg
IMG_20230710_111316.jpg

IMG_20230710_111422.jpg

Picha kutoka mtandaoni

Usalama wa watu na jamii zetu ni jukumu letu sote.
 
Back
Top Bottom