Tahadhari ili kuepuka gharama uji wa ulezi huchanganywa na unga wa mchele

Nashukuru hatimaye umenielewa.
Basi usiishie kucheka tu, toa mrejesho kuwa sasa uko vizuri juu ya hili.
Mimi ni waliperson!yaani kwangu mchele ndio best wanga ukifuatiwa na ngano...huo ulezi ukipikwa bila kuchanganya ndio sili kabisaaaa
 
😁😁 Nimependa ulivyoanza maelezo,yaani ni kama nakuchosha....Ukisema ulezi upo juu kuliko mahindi unakosea,bei ya soko inayotambulika na wizara ya viwanda na biashara mchele ndio uko juu,mchele min ni sh 2000-max3000,na wakati ulezi ni min1800-max1900..Sasa Ukiona mama kakuchanganyia na mchele ujue wewe ndio mnyonyaji........ila inaonekana wewe ni mpenzi wa uji wa ulezi.
Sasa unataka kunidanganya huku nikiwa macho kabisa!
Huyo mfanya biashara anayenunua ulezi kwa bei ndogo, huku akijua mcele ni ghali; halafu aamue kuchanganya na ulezi, ili apate hasara ya bei aliyonunulia mchele; biashara ya namna hii sijawahi kuisikia. Pengine ndiyo sababu biashara zetu nyingi ndogo ndogo huwa hazifanikiwi, kwa sababu hatufuati kanuni za biashara.

Labda nikuombe unifahamishe hili: ni sababu gani zinazofanya ulezi uchanganywe na unga wa mchele? Inawezekana hilo ndilo silijui.
 
Mimi ni waliperson!yaani kwangu mchele ndio best wanga ukifuatiwa na ngano...huo ulezi ukipikwa bila kuchanganya ndio sili kabisaaaa
Sawa, sina la ziada juu ya hilo, ila kusema tu kuwa kuna wengine wasiosikia la mtu inapokuja katika uji wa Ulezi. Hawataki kabisa kuchanganyiwa na unga wa mchele. Kwa hiyo ni bora kuwa muwazi kabisa unapofanya biashara hiyo. Sema unauza uji uliochanganywa ulezi na mchele; usiishie tu kuwadanganya kuwa uji ni wa ulezi.

Hebu ngoja kwanza: umesema "ngano". Sijawahi/sijapata kuonja uji uliotengenezwa kwa kutumia unga wa ngano. Hivi nao upo sokoni?
 
Sasa unataka kunidanganya huku nikiwa macho kabisa!
Huyo mfanya biashara anayenunua ulezi kwa bei ndogo, huku akijua mcele ni ghali; halafu aamue kuchanganya na ulezi, ili apate hasara ya bei aliyonunulia mchele; biashara ya namna hii sijawahi kuisikia. Pengine ndiyo sababu biashara zetu nyingi ndogo ndogo huwa hazifanikiwi, kwa sababu hatufuati kanuni za biashara.

Labda nikuombe unifahamishe hili: ni sababu gani zinazofanya ulezi uchanganywe na unga wa mchele? Inawezekana hilo ndilo silijui.
Ndio hivyo,we tafuta hata takwimu za bei ya nafaka utaona mchele juu ulezi chini....labda tu nikuume sikio,,,wanatumia chenga,ambazo bei yake ni 800-1000😁😁
 
Wadau hamjamboni nyote?

Nimeona niwape tahadhari kabla ya kuwatakia usiku mwema

Ni kwa wale Ndugu zangu wanaopenda kunywa uji wa ulezi kama mimi hapa.

Huu ni utafiti usio na chembe ya uongo kuhusu uji wa ulezi unaouzwa kwa kutembezwa barabarani na Wamama hususani hapa Dar es salaam

Inadaiwa kuwa uji huo huwa unachanganywa kwa ufundi mkubwa na mchele uliosagwa.

Sababu ni gharama kubwa za unga wa Ulezi hivyo wauzaji huchanganya na mchele ili kuufanya uji huo uwe mzito na hivyo kumpatia muuzaji faida huku mnywaji akikosa virutubisho muhimu

Unashauriwa kuwa makini na matumizi ya uji huo unaotembezwa barabarani vinginevyo nenda sokoni nunua unga kisha mpatie mkeo akuandalie

Njia rahisi kugundua mchanganyo huo haramu kwa wazoefu ni ladha tu ya uji kuwa siyo ya kawaida

Ucku mwema

View attachment 2968677
Sawa mkuu. Nashukuru kwa ushauri. Lakini ulezi na mchele vyote ni carbohydrates. Sioni kama kuna virutubisho utavikosa hata ukinywa uji wa mchele peke yake ukilinganisha na uji wa ulezi peke yake. Tofauti ipo tu kwenye ladha lakini matumizi mwilini ni sawa....they all energy-giving foods and have the same chemical contents and composition.

Labda kama umefanya utafiti wa chemical analysis hebu tuambie contents za ulezi zinavyotofautiana na contents za mchele ili tukuelewe mkuu. Otherwise, hii ni kama hadithi tu unayotuletea hapa.

Hebu tazama hapa mkuu mtoa mada:
1715357728962.png

NUTRITIVE VALUE OF FINGER MILLET
1715357805034.png

Umeona kuwa hakuna tofauti mkuu? kwa hiyo kama wanachanganya waache waendelee kuchanganya ili kuboresha ladha kwa kuwa thamani za kilishe zinafanana.
 
Ndio hivyo,we tafuta hata takwimu za bei ya nafaka utaona mchele juu ulezi chini....labda tu nikuume sikio,,,wanatumia chenga,ambazo bei yake ni 800-1000😁😁
Unaona sasa, kumbe jibu ulikuwa nalo, lakini hukutaka kulitumia hadi mwisho! Tabia hii inaturudisha nyuma sana waTanzania. Hapo kutumia chenga za mchele kupata unga, inakuwa siri, kana kwamba ni 'patent ya jambo jipya kabisa lililogunduliwa karibuni!. Chenga za mchele inakuwa ni siri kubwa ya kibiashara!
Hujaeleza kuhusu ngano na uji.
 
Back
Top Bottom