Tatizo la ukosefu wa haja kubwa kwa watoto wadogo na Vichanga. Fahamu chanzo chake na namna ya kutibu

omben

JF-Expert Member
May 30, 2012
812
449
1588596721784.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Nina mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 ana tatizo la kutokupata haja kubwa. Tatizo hilo limeanza juzi, leo ni siku ya pili bila kupata haja. Ana joto la kawaida ila leo amebaki analialia tu.

Nimekwenda zahanati wananiambia hana tatizo lolote.

Please naomba msaada wenu.
---

Habarini wana jf kuna tatizo la mtoto mchanga anakosa kwenda haja kubwa.Yeye anaweza kupitisha hata siku tatu lakini utamsikia analialia na kutoa gesi/hewa chafu.Wajuzi wa mambo naomba ushauri au tiba kwa haka kabinti ili kapate haja kama inavyopaswa kwa mwili wa binadamu.Natanguliza shukrani zangu.
---
Asalaam wadau natumaini nyote tumeamka salama!

Ni tatizo moja mwanangu ana umri miezi 4 na nusu. Ila ana changamoto ya kutopata choo(haja kubwa) na leo inaenda siku ya 3. Je shida inaweza kuwa nini? Na natakiwa nifanye nini ili apata choo kila siku? Na tumaini nitapa majibu ya kusaidia tatizo hili.

Asanteni 🙏🏿🙏🏿
---
Habari wakuu.
Kama nilivyoweka wazi hapo juu. Mwanangu wa miaka 5 hapati haja kubwa sawasawa.

Akienda haja kubwa anajisaidia kwa shida sana mpaka analia kama anapigwa.

Wakati mwingine inashindikana maana haja haitoki. Kuna wakati anapitisha siku nzima mpaka siku ya pili.

Nimempeleka hospitali nikashauriwa nimpatie vitu ambavyo kimsingi huwa nampatia mara kwa mara lakini mafanikio hakuna.

Anakula sana matunda, maji mengi, anacheza, mbogamboga sana lakini bado sioni mwanga.

Juzi juzi nilishauriwa nimpatie mafuta ya mlonge, nikampatia kiasi fulani kwa siku mbili tatizo lilipungua ila badae limerejea tena japo bado anaendelea kutumia mafuta hayo.

Naomba anaefahamu dr bingwa wa watoto na mambo kama hayo ama tiba mbadala anisaidie nimwokoe mwanangu.

Natanguliza shukrani kwenu na Mungu atawabariki.
---
Jamani naomba mnisaidie naamini hapa kuna wazoefu juu ya ulezi

Mwanangu (kiume) umri siku 27, analia sana hasa usiku hatulali... Pia ana siku ya nne hajapata haja kubwa, anaishia kujamba. Jumatatu tulimuona dokta, akamcheki tu akasema hana tatizo.

Mama ana maziwa ya kutosha na mtoto ananyonya vizuri tu ila shida ndo hiyo nilowaambia

Note:tulijaribu kumnywesha Gripewater lakini hakupoa.... na leo tumeanza kumpa INFACOL lakini bado tatizo halipoi.

msaada wa mawazo ndugu zangu

Sent using Jamii Forums mobile app

===
UFAFANUZI WA WATAALAMU KUHUSU TATIZO HILI
KUKOSA CHOO KWA WATOTO WADOGO.

kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation.

Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza

kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.

Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.

Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji ya Uvuguvugu safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.

2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.

3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.

4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.

5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.

6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.

7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng'ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng'ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng'ombe.

8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.

N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.

Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.
===

USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
Danny Job,
Hiyo tiba inaitwa kwa kitaalam 'ENEMA', unatumia kitu kinaitwa 'rectal bulb syringe'. Ni common practice katika jamii nyingi vijijini tulikokulia ambapo kwa wale waliokuwa hawajapata uwezo wa kununua hizo rectal bulbs walikuwa wanajaza dawa mdomoni kisha wanaipuliza kwenye 'lower bowel' ya mtoto kupitia 'rectum' kwa kutumia mrija (wa matete).

'Constipation' inaweza kumsababishia mtoto discomfort nadhani ndiyo maana analialia. Pia nadhani ikiendelea sana inaweza kusababisha matatizo mengine pia.

Ila mara nyingi hata bila 'intervention' inaweza kuisha baada ya siku kadhaa kwa mtoto kuachia 'mzigo mkubwa' sana hadi mkaukimbia kwanza!

220px-Rectal_bulb_syringe.jpg
Rectal bulb syringe
---
TATIZO LA MTOTO KUKOSA CHOO

Watoto wadogo hususani wale ambao bado wananyonya na wale ambao ndio wameanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na tatizo hili la kuwa na choo kigumu na hata kukosa choo kabisa.

Hali hiyo kitaalam huitwa ‘constipation’ mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa sana na tatizo hilo, lakini tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Mzazi unashauriwa kumuona daktari pindi unapogundua mtoto wako anasumbuliwa na tatizo hili, lakini pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

Kwanza hakikisha unampatia mtoto maji safi na salama ya kutosha na utakuwa ukipunguza au kuongeza kiasi cha maji kulingana na hali ya mtoto inavyoendelea. Hali kadhalika unaweza kumpatia mtoto juisi za matunda pia .

Pia ni vyema kujitahidi kumpa mtoto vyakula vyenye nyuzi nyuzi endapo mtoto atakuwa ameshaanza kula vyakula vigumu.

Mbali na hayo pia unaweza kumpaka mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Hakikisha mafuta unayotumia si yale yenye madini (mineral oil.)

Hata hivyo kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Jaribu kukatisha kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo bado endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe. Source.DK MANDAI: TATIZO LA MTOTO KUKOSA CHOO
---
Mtoto wa miezi miwili anapata shida kupata choo unamlisha nini zaidi ya maziwa ya mama? Au unampa maziwa ya kopo?

Na pia kabla ya tatizo kuanza alikuwa anapata choo mara ngapi kwa siku ? Mara ya mwisho kupata choo lini? Ni vizuri kujua tabia ya mtoto kupata choo aja kubwa na ndogo hili mabadiliko ys kitokea huweze kutatua mapema.

Kwa sasa ushauri wangu ni huu:
Mtoto anapozaliwa ni vizuri kumpa maziwa ya mama mpaka miezi sita japo ni vizuri zaidi kumnyonyesha mpaka mwaka mmoja. Maziwa ya mama nirahisi kwa mtoto kusaga tumboni kuliko maziwa ya kopo(formula).

Formula si nzuri kwa watoto wote na ziko haina tofauti. Mara nyingi inawajaza gesi watoto na kuwaletea maumivu na pia kukosa choo.

Wakina dada wengi siku hizi hampendi kunyonyesha mnaogopa maziwa yenu kulala na matokeo yake mnawapa watoto maziwa ya kopo. Maziwa ya mama muhimu sana kwa mtoto na humsaidia mtoto kujenga kinga nyingi mwilini.

Kama unatumia maziwa ya kopo, acha , anza kumyonyesha mwanao na kama ni lazima kumpa maziwa ya kopo mpe yalioandikwa "sensitive". Kama bado tatizo linaendelea mpeleke kwa daktari.
---
mathabane,
Ndg mpendwa.. nimeongea na wife Sasa hivi.. kani shauri uanze na dose ya Asali (pure honey) vijiko bow ili hadi tatu :-
1 unachanganya na maji ya moto (dafidafi siyo makali) acha Anywe Mara tatu kwa siku!! Kwani asali husafisha tumbo na huwa haikaai pamoja na any uchafu or bacteria.

2. Asema mmoja Wa mtoto wetu alikuwa hivo hivo!

3. Ile dose ya maramia ni baadae kabisa.

All the best and God bless you and our children's.. Ameen
---
Unaweza muongezea juisi ya ukwaju ni nzuri pia. Tafuta ukwaju safisha vizuri kisha loweka au chemsha, unaweza kamua kwa mikono Safi, kisha chuja, unaweza changanya na sukari au asali au tende ili kupunguza ule uchachu kisha mpatie anywe glass moja utapata matokeo.

Tumia ukwaju mara kwa mara kwa tatizo la digestion. Ilinisaidia Sana baada ya kukaa wiki mbili mwaka 2010 bila kupata Choo nilitumia papai kama mlo, dawa za hospital mafuta nk. Glass mbili za ukwaju zilinipa matokeo ndani ya dakika 15.

Mpaka sasa ukwaju juisi mixer tende ndio juisi yangu maarufu sana. Au ukwaju mix na papai pia ni haraka Sana inaleta matokeo.
---
mathabane,
Kwanza pole sana mkuu. Watoto huwa wanapitia changamoto nyingi. Hili la haja kubwa lisikupatie shida sana.

Mara nyingi watoto huwa wakipata choo kigumu hukwama sehemu za ndani za unyeo hivyo kushindwa kukisumuma vizuri.

Cha kufanya mwambie mama yake apake jelly/KY/mate kwenye kidole kidogo afu amusafishe ndani ya unyeo.

Unaweza kuta kunakinyesi kigumu kimekwama muda mmrefu - Akikikuta akitoe kwa uangalifu. Baada ya hapo ataendelea kama kawaida.

Ukimaliza leta mlejesho na pole sana kwa maswaibu hayo.
---
MREJESHO:
Napenda kuwashukuru wakuu wote kwa mioyo ya kujali na uungwana wa hali ya juu.

Nimeanza hatua za awali katika kufanyia kazi ushauri wenu. Hivyo nikaamua leo nisiende kazini ili nishugulike na afya ya binti yangu.

Kuanzia jana usiku nilianza kumpatia asali vijiko 3 kabla ya kulala.

Asubuhi nikampatia asali tena, saa 4 juice ya ukwaju kwa kuchanganya na asali .

Nimeendelea kumpatia dozi ya juice ya ukwaju na asali kila baada ya saa 1.

MATOKEO
Amepata choo laini bila ya maumivu mara mbili leo majira ya sa 4 na sa 10 jioni jambo ambalo sio kawaida kutokea kwake.

Mungu awabariki sana ndugu wote mliochangia kuleta furaha yangu na familia yangu.

Sina neno zuri na la pekee la shukrani zangu kwenu ila Mungu anajua kuliko mimi,naye atawatendea neno lililo jema kwenu.
---
Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua

Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation. Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.

Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.

Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.

2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.

3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.

4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.

5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.

6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.

7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng?ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng?ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng?ombe.

8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.

N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.

Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.

KWA USHAURI KUHUSU TATIZO HILI KWA WATU WAZIMA SOMA HAPA:
- Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake - JamiiForums
 
Muinike(sijui tafsiri nyingine ya hili neno) ila kuna kifaa kipo kana droppers,unakiminya unaingiza kwenye maji ya vuguvugu halafu unakiruhusu kifyonze maji.

kisha unaingiza mrija wake sehemu ya mtoto ya kutolea haja kubwa taratibu kwa uangalifu, unakiminya na kuachia mara kadhaa halafu unamwacha mtoto apumzike.

Hapo atapata choo tu vinginevyo waone madaktari wengine watakusaidia.
 
Danny Job,

Hiyo tiba inaitwa kwa kitaalam 'ENEMA', unatumia kitu kinaitwa 'rectal bulb syringe'. Ni common practice katika jamii nyingi vijijini tulikokulia ambapo kwa wale waliokuwa hawajapata uwezo wa kununua hizo rectal bulbs walikuwa wanajaza dawa mdomoni kisha wanaipuliza kwenye 'lower bowel' ya mtoto kupitia 'rectum' kwa kutumia mrija (wa matete).

'Constipation' inaweza kumsababishia mtoto discomfort nadhani ndiyo maana analialia. Pia nadhani ikiendelea sana inaweza kusababisha matatizo mengine pia.

Ila mara nyingi hata bila 'intervention' inaweza kuisha baada ya siku kadhaa kwa mtoto kuachia 'mzigo mkubwa' sana hadi mkaukimbia kwanza!

220px-Rectal_bulb_syringe.jpg
Rectal bulb syringe
 
Mtoto mchanga kupata tatizo hilo yakubidi kuwa makin zaid. Nakuomba mpatie vitamin B ya maji 5mls anza safari kwenda hosptal hasa hospitali ya wilaya atachunguzwa na tiba itaendelea.
 
Hiyo tiba inaitwa kwa kitaalam 'ENEMA', unatumia kitu kinaitwa 'rectal bulb syringe'.....

vyema sana mkuu kwa kuweka picha nazani ataelewa vizuri..
niliogopa kukianfika kwa kiingereza maana hakifahamiki sana na pia kwa kiswahili sikijui kabisa kinaitwaje..
ya hii ni njia nzuri sana na rahisi.
 
Habarini wana jf kuna tatizo la mtoto mchanga anakosa kwenda haja kubwa.Yeye anaweza kupitisha hata siku tatu lakini utamsikia analialia na kutoa gesi/hewa chafu.Wajuzi wa mambo naomba ushauri au tiba kwa haka kabinti ili kapate haja kama inavyopaswa kwa mwili wa binadamu.Natanguliza shukrani zangu.
 
Habarini wana jf kuna tatizo la mtoto mchanga anakosa kwenda haja kubwa.Yeye anaweza kupitisha hata siku tatu lakini utamsikia analialia na kutoa gesi/hewa chafu.Wajuzi wa mambo naomba ushauri au tiba kwa haka kabinti ili kapate haja kama inavyopaswa kwa mwili wa binadamu.Natanguliza shukrani zangu.

Mpeleke hospitali huyo mtoto wewe mbona unakuwa kama sio mzazi makini. Kamuone daktari wa watoto, na wale manesi wa kliniki watakusaidia kwani msaada unatokana na maelezo yako ya kina. Hamjampa kweli chakula kisichotakiwa kwa watoto, kwani ndani ya miezi sita anatakiwa kunyonya maziwa ya mama tu, hakuna cha maji ya kunywa wala nini.

Dalili kubwa ni kwamba mmeanza kumpa maziwa ya formula/ kopo. Vyombo vyake vinatakiwa kuwa visafi - vya chakula mpaka kuoga, anatakiwa kuoga maji yaliyochemshwa, na wala sabuni isiingie mdomoni. Ila sasa hivi funga safari ya kwenda kumuona daktari.
 
Thas normal..nothing to worry about..a baby can go upto 7 days without passing! Pia
jenga utaratibu wa kumfanyia massage tumboni na pia mfanyishe miguu in a movemnt ya kama anaendesha baiskeli.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu ambao umenifumbua maana nilikuwa gizani kwa hili.Hapo ndipo naipendea jf ya GreatThinkers.Keep blessed
 
Mpeleke hospitali huyo mtoto wewe mbona unakuwa kama sio mzazi makini. Kamuone daktari wa watoto, na wale manesi wa kliniki watakusaidia kwani msaada unatokana na maelezo yako ya kina...

miezi 6 mtoto bila kunywa hata maji!? not applicable kwa Tanzania hasa maeneo yenye joto, kwangu mimi wakati namlea mwanangu nilishindwa kufuata formula hzo kwenye vitabu vya madaktari
 
Ni hali ya kawaida kama ni mtoto chini ya miezi sita,anaweza fikisha hata siku tano hajapata,jitahidi kumnyonyesha kwa sana
 
Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua

Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa hali tunayoiita kimombo, constipation.

Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au mengineyo au pia anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa.

Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.

Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso. Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.

Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwa vyema.

2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa.

3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele au fiber. Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwa pondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.

4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.

5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumia mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharishwa katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.

6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirschsprung ugonjwa wa kumee neva katika utumbo, au Cystic Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.

7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng?ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya ng?ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng?ombe.

8. Mwogeshe au mweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwa majini na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata chook wa urahisi.

N.B Ukosefu wa choo kwa watu wazima baadhi ya wakati huandamana na magonjwa kama vile Arthritis, Appendicitis, Cataract, saratani, shinikizo la damu, Rheumatism na kadhalika lakini kwa watoto huenda tatizo hilo likawa halisababishwi na maradhi hayo.

Utafiti unaonyesha kuwa hakuna uhusiano wowote kuhusu kukosa choo mtoto na kupewa nyongeza ya chuma au Iron Supplement. Hivyo usimkatishe kumpa mwanao chuma iwapo anakosa choo. Kwani chum ni muhimu sana katika kuzuia upungufu wa damu mwilini kwa mtoto wako mdogo.
 
Hizo njia zooooote hapo juu ni too complicated, gharama,n.k. japo ni nzuri!
Kabari ya tatizo hilo ni;

Mtoto akikosa choo, muweke kakipande cha sabuni ya kufulia hasa hasa "Jamaa" au "Lyang'ombe"
Unamchukua,unapanua kidogo sehemu yake ya haja kubwa unakapichika hako ka soap,kidogo tuu! Hachukui round, atayanya yoote tena kama sabuni ni kali ataharisha kabisa.

Na hakuna madhara, ni njia nzuri ya asili fulani hivi, halafu affordable.
Hata kwa mtu mzima ukiona gogo ni gumu mno,weka ki piece cha soap huko kunako,halafu chezea maeneo ya chooni, utashusha mzigo smoothly kabisa.

NINA mtoto,ana mwaka mmoja na miezi 6 sasa, amefanyiwa hivyo, majirani waliolea nao vile vile na ndo walishauri. Ila hayo sijui Juice ya Apple,Pera, n.k. waachie familia za Dadiii na Mamiii, hapa nawashauri kina sie mboga moja!
Ni njia nzuri na salama.

Ni dizaini kama mtu aliyekula ugoro,jinsi gogo linavyoshukaga haraka na kwa spidi ya 120km/sec
 
Hizo njia zooooote hapo juu ni too complicated, gharama,n.k.? japo ni nzuri!
Kabari ya tatizo hilo ni;
Mtoto akikosa choo, muweke kakipande cha sabuni ya kufulia hasa hasa "Jamaa"?
Unamchukua,unapanua kidogo sehemu yake ya haja kubwa unakapichika hako ka soap,kidogo tuu! Hachukui round, atayanya yoote tena kama sabuni ni kali ataharisha kabisa?
Na hakuna madhara, ni njia nzuri ya asili fulani hivi, halafu affordable.
Hata kwa mtu mzima ukiona gogo ni gumu mno,weka ki piece cha soap huko kunako,halafu chezea maeneo ya chooni, utashusha mzigo smoothly kabisa?
NINA mtoto,ana mwaka mmoja na miezi 6 sasa? amefanyiwa hivyo, majirani waliolea vile vile na ndo walishauri.

Ila hayo sijui Juice ya Apple,Pera, n.k.? waachie familia za Dadiii na Mamiii, hapa nawashauri kina sie mboga moja!
Ni njia nzuri na salama?

Ni dizaini kama mtu aliyekula ugoro,jinsi gogo linavyoshukaga haraka na kwa spidi ya 120km/sec

Mh! Mkuu
 
Back
Top Bottom