AzamPesa nimejisali leo tayari napokea simu za matapeli

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Habari wana-JF imebidi niandike huu uzi maana nimepata mashaka na usalama wa taarifa zangu kwenye hii huduma ya AzamPesa.

Leo asubuhi nilijiunga na huduma ya AzamPesa kwa lengo la kuanza kutumia huduma hii ila simu ya tapeli niliyopokea imeniaminisha hii huduma bado siyo salama kwa Watanzania.

Usiku huu nimepokea simu kwa namba ngeni, kitu kilichonishtua kwasababu namba niliyojiungia AzamPesa wanaijua familia yangu tu na huwa naitumia kwenye huduma zote za kifedha. Namba mpya huwa sipokei kwasababu siyo namba ninayompa kila mtu ila nilikuwa na miadi ya kukutana na ndugu yangu na namba iliyopiga ilikuwa ikifanana hivyo nikahisi huenda ndiye labda sija-save (ana namba nyingi).

Nikapokea simu ila nikakaa kimya kwasababu hii ni namba binafsi yoyote tofauti na familia nitasikilizia aongee kwanza.

Tapeli: Habari, ndugu Forgotten.

Mimi: Salama, habari.

Tapeli: Leo ulijiunga na huduma ya AzamPesa.

Mimi: Ndiyo.

Tapeli: Vipi maeneo ulipo kuna mawakala wa kutosha?

Mimi: Ndiyo.

Tapeli: Upo mkoa gani?

Mimi: Nipo..........

Tapeli: Mjini?

Mimi: Ndiyo.

Tapeli: Kuna tarakimu nne za OTP zimeingia kwenye simu yako nitajie.

*Ni kweli nilipokea OTP kabla hajapiga simu, tena nikashangaa OTP za nini wakati hata app sijatumia toka mchana. Nikapata mashaka ila nikahisi huenda system yao ilituma meseji nyingi wakati wa usajili.

Mimi: Za nini?

Tapeli: Mimi ni wakala nahitaji ili nikamilishe usajili wako pia niweze kuona idadi ya mawakala waliopo eneo lako.

Mimi: Nimeshakamilisha usajili mwenyewe.

Tapeli: Ndiyo, ila ni lazima huku pia tukamilishe usajili.

*Nikakata simu.

Kiukweli nimejiuliza maswali mengi, huyu tapeli amepataje taarifa zangu? Jina na namba ya simu niliyojiungia AzamPesa. Kama ameweza ku-access taarifa hizi kwenye system ya AzamPesa maana yake taarifa zangu za NIDA zipo wazi tu pamoja na taarifa za watumiaji wengine.

Sijajua kama ali-reset PIN ili aweke OTP abadili PIN halafu akahamishe fedha au alifanyaje ila kwa watumiaji wa AzamPesa muwe makini sana.

Kwa hili tukio ni wazi AzamPesa haijaja kuwasaidia Watanzania kwasababu wameshindwa kuleta bidhaa inayotatua matatizo na mapungufu ya washindani wao.
 
Mimi naomba kuuliza, Azam wamefungua lini mtandao wa simu, line zao zinapatikana wapi?

Au ni huduma ya Pesa ya online tu kwamba lazima uwe na app inayofanya kazi via internet connection? Na je, kama ni hivyo, ina kipi cha ziada kuliko hizi huduma zinazotumia namba za line za simu?
 
Mimi naomba kuuliza, Azam wamefungua lini mtandao wa simu, line zao zinapatikana wapi?

Au ni huduma ya Pesa ya online tu kwamba lazima uwe na app inayofanya kazi via internet connection? Na je, kama ni hivyo, ina kipi cha ziada kuliko hizi huduma zinazotumia namba za line za simu?
1. Hawajafungua mtandao wa simu

2. Hawana laini kwa vile hawana mtandao wa simu.
Ila wana huduma ya pesa ambapo unapata huduma zote kama zilizopo MPESA, TIGOPESA au AIRTELMONEY.
Jinsi ya kujiunga, unajiunga kupitia smartphone kwa kupakua app yao na kujisajili.
Namba yako ya simu uliyojisajili ndio itakuwa namba ya azampesa ila 0 ya mwanzoni inabadilishwa kuwa 1.

3. Si lazima kutumia enternet, hiyo inatumika wakati wa kujiunga na unaweza kuamua kuendelea kutumia app au USSD.

4. Hawana cha zaidi kuliko mitandao ya simu sana sana wao kutuma pesa ni bure, ukijiunga pia unapata pesa kidogo.
 
Back
Top Bottom