tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,838
- 18,250
Heri ya mwaka mpya watu wangu wa nguvu. Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi. Naomba niseme kuwa huu ndio uzi wangu wa kwanza kwa mwaka huu wa 2024. Sikuwa nimepanga kuweka uzi hapa JF mapema hivi ila imenibidi nifanye hivyo baada ya kupokea ujumbe huu wa onyo kwa njia ya WhatsApp unaolenga kuwatapeli walimu.
Ujumbe huu umeambatana na audio ya tapeli maarufu wa mtandao ambaye amekuwa akiwasumbua sio tu walimu bali watanzania wengi, hasa watumishi wa umma. Sauti ya mtu huyu sio ngeni. Amekuwa akiwatapeli watanzania kwa muda mrefu sasa. Huenda hata wewe mwanaJF unayepitia uzi huu ulishawahi kukumbwa na dhoruba ya huyu bwana, ama akakutapeli au ukaponea chupuchupu. Sikiliza audio yake kwenye attachment hapo chini.
Kinachonisikitisha ni kuwa huyu jamaa amekuwa akiwatapeli watanzania kwa miaka mingi sasa bila kukamatwa na vyombo vya serikali. Hata TISS nao eti wameshindwa kumtia nguvuni pamoja na vifaa vyote vya kiintelejensia walivyo navyo. Ikiwa tapeli mdogo kama huyu amewashinda, je tuwaamini kulinda usalama wa nchi?
Tunaweza kusema labda polisi wa kawaida wanaodili na cybercrime hawana vifaa vya kumtafuta na kumpata. Hata TISS nao wameshindwa kweli kumtia mikononi huyu mshenzi na kumchukulia hatua za kisheria?
MAONI YANGU
Visa vingi vya utapeli wa rejareja mara nyingi vinalengwa kwa walimu. Hivi walimu wana uwezo mdogo wa kufikiri kiasi hiki hadi kila siku walengwe wao tu? Ikiwa sisi tunawategemea walimu kutufundishia watoto wetu halafu wao wanakuwa na akili ndogo ya kutapeliwa kirahisi tutarajie nini?
Ndio maana ubora wa elimu unazidi kushuka mwaka hadi mwaka kumbe ni kwa sababu elimu inatolewa na watu wenye upeo mdogo wa kufikiri. Mkuu Mpwayungu Village hawa walimu wenzako wanatuangusha sana. Nadhani baada ya kazi ya upolisi, kazi ambayo inasomba watu wasiokuwa na wito ni kazi ya ualimu. Tuna safari ndefu sana ya kufikia maendeleo ya kweli ikiwa think-tank yenyewe tunayotegemea ni ya aina hii ya walimu. Inasikitisha sana.