Tafrani Kimara: Msongamano kituo cha Mwendo kasi - Abiria wakiwemo wanafunzi wazimia!

serikali kwanini haipendi upinzani?
Kwani upinzani wanaipenda serikali?Toka lini wamekuwa na hayo mapenzi?Kuapishwa Magufuli walisusa wakasema hawamtambui,Bungeni wakasusa hotuba yake kuwa hawamtambui kama Raisi!!!Sasa yeye awatambue wakati hawajawahi tengua hiyo kauli ya kutomtambua kama Raisi?
 
Ni ngumu sana kupata hela za kulipia hayo magari in one instalment, waestablish liability waingie mkataba wa malipo kwa instalment, they need to be pro service, ubabe tu wa kutumia nguvu za sheria nao ni utumwa wa madaraka.
Sasa kwa nini walinunua mabasi 70 kwa one installment? Si wangenunua 35 halafu hela inayobaki iwe ya kulipia kodi?
 
Mabasi 70 si wanasema TRA wameyashikilia haya ndiyo madhara yake
Hii nchi ina watu wamejaa maofisini huko lakini uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana,wangeruhusu yaendelee kufanya biashara huku wanachukua kodi yao taratibu sasa miezi 6 wameambulia nn?
Lakini sishangai sana wengi wa watzn tuna upeo mfupi sana mfano huku Tunduma kila jumamosi biashara zinafunguliwa saa 4 kwa maelezo kuwa ni siku ya usafi,pesa kiasi gani inapotea ndani ya hayo masaa?
 
Mwendokasi waruhusu daladala kutumia barabara zao mida ya asubuhi na jioni kuwasaidia hawana uwezo WA kuhudumia mida hiyo.Abiria wanajaa vituoni masaa bila huduma
Ebu fuatilia majibizano kwenye twitter kuhusu ushauri kama wako na watu wanaohusika....

@DARTMwendokasi @WizaraUUM kutokana na elimu yetu ya kukariri kutokupenda ku-simply mambo, kutokuwa innovative/creative kila kitu kwetu ni kigumu, hatushangai barabara nzuri zajengwa huku mitaro ikiwa wazi ambayo ni hazard kwa binadamu, ila kwetu poa tu inasikitisha
jibu

[B]Tumaini Kilimba[/B]‏ @[B]Tumaini_Kilimba[/B] Sep 19
Replying :
Toa mfano ya nchi gani Ina ruhusu dala dala sambamba na BRT?

Replying to
Kwa waliobarikiwa kwenda nchi zilizoendelea wataelewa, mpaka taxi zinaruhusiwa kupita hapo, watatumia vituo hivyo hivyo, abiria atachaguwa basi lipi apande tu..sitaki kuamini hilo zoezi laonekana gumu..

[B]Tumaini Kilimba[/B]‏ @[B]Tumaini_Kilimba[/B] Sep 19
Replying to :
Toa mfano ya nchi gani Ina ruhusu dala dala sambamba na BRT?

Inasikitisha sana, kwamba ubabaishaji bado upo, na watu hawataki kuwa creative/innovative, wako rigid na mawazo yao ya mgando kama zama zile, ni shida
 
serikali ya TANZANIA. haiwezi kutatua hiyo kero " Mpaka pale Jamii ya watu wa taifa lake " itakapofikwa na Maafa "... (watu wapate ajali wafariki) ... kisha serikali isubiri kupokea rambi rambi " ikishapokea rambi rambi " watatangaza kuzitumia pesa hizo kujenga au kuimarisha miundombinu yoyote ...

hii ndio TZ Zaidi ya uijuavyo bwana ..hehee
 
Hujui mfumo wa elimu Tz
Mfumo wa elimu Tanzania mwisho ni chuo kikuu, by that time ushafikisha miaka sema 30 kwa kiwango cha juu. leo una miaka 40, miaka yote kumi haujajirekebisha tu.

ukifikisha miaka 50 bado una akili za hovyo huwezi laumu mfumo wa elimu, ni wewe mwenyewe ndio tatizo.
 
Bandarini kuna mabasi mapya 70 ya Mwendokasi zaidi ya miezi 6 sasa yamekaa tu kisa serikali inagombana na DART/UDA kuhusu kodi huku wananchi wakiumia!!
Mabasi hayo 70 yaliyopo bandarini ndiyo yamesababisha mabasi yaliyopo kazini kuzurua kwenye route bila kubeba abiria?

Gari zinashusha abiria na kuondoka bila abiria. Tunajua hii nitaifoward hujuma kwa serikali na wananchi.

Acha kutumika vibaya
 
Sasa kwa nini walinunua mabasi 70 kwa one installment? Si wangenunua 35 halafu hela inayobaki iwe ya kulipia kodi?

wewe unawazungumzia hao BRT, mimi nawazungumzia TRA. Kosa la kwanza halijustify kosa la pili.
 
Kitu najiuliza hizo bus 70 zingekua za kilimanjaro express wangeendelea kumbembeleza alipe kodi?
Jiulize, basically 70 zimezuia zilizopo zisitoe huduma?

Kama kwenye kituo cha mwendokasi uhesabu basi zinazipita tupu....
 
Mleta mada nimetumia zaidi ya masaa mawili kufuafuatilia utendaji wa Mabasi hasa masaa ya mchana nikaambiwa mchana pia ilikuwa kero kubwa mida ya kuanzia saa sita hadi nane Na nusu.Wakasema wanashangaa leo Mabasi ya kimara Na ubungo yako kibao
 
wewe unawazungumzia hao BRT, mimi nawazungumzia TRA. Kosa la kwanza halijustify kosa la pili.
Kwa miezi kumi hajapata hela ya kulipia kodi atoe Mabasi hata kumi tu? Miezi kumi hajapata hela ya kodi ya kutoa hata basi moja si tapeli huyo
 
Kwa miezi kumi hajapata hela ya kulipia kodi atoe Mabasi hata kumi tu? Miezi kumi hajapata hela ya kodi ya kutoa hata basi moja si tapeli huyo

Well, miezi kumi ni mingi.
Lakini unajua madhara ya kifedha kwa hujuma alizofanya magufuri kwa kusitisha huduma za maxcom? unajua pesa ngapi hupotea kila siku baada ya kupokelewa mannually? unajua pesa ngapi zinapotea kila siku kwa abiria kupanda hayo magari bure?

Una uhakika serikali haijaingilia mfumo wa usimamizi fedha wa shirika hilo? serikali hii isiyopenda kulipa madeni ya ndani?
 
Saa nane hii, hamna abiria, subiri ifike kumi na moja
Mchana kuanzia saa sita hadi nane Na nusu mchana walikuwa pia wana tabia mbaya mabasi yalikuwa hamna leo ghafla wamebadilika kuanzia mchana usafiri wa kimara kibao.Kitu ambacho ni cha ajabu hawako hivi siku zote.Shukrani kwa wote waliosaidia hili.Wanapiga mzigo hasa.Hebu Tusubiri jioni pia tuone
 
Mabasi 70 si wanasema TRA wameyashikilia haya ndiyo madhara yake
Hata wangepata hayo mabasi. Mradi huo ni management failure. Kwa sababu udart ndio wangekusanya hela za nauli hata kama wangelipa tozo kwa dart. Sasa mkusanyaji wa nauli s
Dart, waibe kidogo, ndio amlipe udart kuendesha magari. Wapi na wapi.
 
Back
Top Bottom