Tafrani Kimara: Msongamano kituo cha Mwendo kasi - Abiria wakiwemo wanafunzi wazimia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
45,246
2,000
Hali ni tete katika kituo cha kimara kama ilivyoripotiwa na Benjamin Mzinga wa ITV msongamano wa abiria ni mkubwa na watu wanaathirika kwa kuumizana na kukosa hewa.

Source: ITV mubashara!


=====

DpItNWrXUAAtJG9.jpg large.jpg

Katika hali ya kuonekana kuchoshwa na kutosikilizwa kwa malalamiko yao, abiria wanaotumia mradi wa Mabasi ya Mwendokasi waamua kuoandia dirishani

Kwa muda mrefu abiria hao wamekuwa wakilalamikia utaratibu wanaouita mbovu wa watoa huduma hiyo ya usafiri.

Mapema leo kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa madereva wa mabasi hayo wamegoma kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yao

UDART imesema katika hali isiyo ya kawaida madereva wawili wanadaiwa kutoa mabasi ndani ya kituo hicho kwa makusudi na kwenda kuziba milango mikubwa miwili ya kutokea mabasi hayo na hivyo kusababisha mabasi mengine kushindwa kutoka ikizingatiwa ilikuwa ni nyakati za asubuhi ambapo mabasi yote yanapaswa kuanza safari zake. Madereva nao wadai kutolipwa Mshahara kwa Wakati.
 

donbeny

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
3,578
2,000
Kuna upungufu wa mabasi ,serikali waangalie namna ya kutatua ikiwemo kumalizana na walioleta mabasi 70 bandarini.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,877
2,000
Unapandajepandaje kwenye daladala yenye mlango kushoto mwa dereva wakati abiria wa mwendokasi wanakaa kulia mwa davoo?
Wakifika Kituo cha mwendokasi wanashuka barabarani Milango ya dala dala kushuka ni kushoto hawaingii kwenye jengo unashuka kituoni unaendelea na safari Kama wanavyoshuka vituo vingine Na kupanda hivyo hivyo
 

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,385
2,000
Bandarini kuna mabasi mapya 70 ya Mwendokasi zaidi ya miezi 6 sasa yamekaa tu kisa serikali inagombana na DART/UDA kuhusu kodi huku wananchi wakiumia!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom