Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

. Vamos de puta Madre
 
Unatumia kinywaji gani mkuu wakuongezee hapo round mbili kwa Bill yangu.
 
Kama unaziona fursa kelele za nini? Nenda kafunguwe kiwanda ubangue korosho uuze Saudia. Shida za hii nchi zinaletwa na wazee wa itikadi. Sioni KIPYA kwenye mada yako cha kukiita ushauri.
Hapo ulipoandika "Sioni kipya" umepatia kwa asilimia mia. Sijawahi kutegemea mwenye macho yasiyoona akaona.
 
Inawezekana sio issue kwa sababu ufafanuzi umetolewa lakini ni issue kwa maskini wale kama hawalipwi kwa wakati... ilhali wana mahitaji ya kielimu, afya, makazi nk. "...aaah HAYATUKHUSU!!!"
Hivi kwanini wanaopewa nafasi "HATUJIFUNZI?"
Korosho zitaendelea kuwa korosho na si korosho hata kahawa tunarudi nyuma... achilia mbali cash crop zingine!!!
China leo wanaleta samaki wanaowafuga hapa kwetu ilhali wao wakiagiza kwetu hapo awali...
Kuna tatizo mahala...
 
Kama umeona fursa ya dengu na mbaazi kwanini usiitumie umngoje balozi?

Huo ndiyo muono wako ulipoishia kungoja kufanyiwa.
 
Ongeza mbili mkuu
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hilo ni tatizo lililokuja ghafla na kwa muda tu, mada yangu imelenga suluhisho la muda mrefu kuepukana na matatizo ya kupangiwa bei na wabangua korosho wa India. Tutoke huko tukapambane na wapanga bei za walaji wa korosho.

Mfano, India wanalima aina nzuri ya mchele wa Basmati lakini nenda India kanunuwe mpunga kama utaupata. At the same time, nenda kanunuwe mchele, watakuuzia hata kwa brand yako na namna ya vifungashio uvitakavyo. Huko ndiyo ku add value ya mazao nilipopalenga mimi.
 
Hayo utayaona kwenye Mazao yote hapa kwetu Tanzania
AISEEEE, nimekusoma sana mkuu.
Jambo la ziada kidogo: hivi inakuwaje tunao wataalam chungu nzima wizarani (kilimo na kwingineko); hivi hawa wastu wanafanya kazi gani huko?

Baada ya kuweka bandiko langu la mwanzo katika mada hii, likaniijia swali: hivi nchi kama Vietnam ambao ndio wanaoongoza katika zao hili wao wakoje? Nika-'google' "Vietnam Cashewnut Processing Industry" Nikakuta taarifa nyingi tu, na hata wao wanavyohangaikia kupata mali ghafi za kulisha viwanda vyao, na jinsi wanavyolinda 'technology' yao ili waendelee kuwa vinara. Waliwanyima Nigeria teknologia hiyo walipoiomba 2007 kwa sababu za ushindani huo.

Nimesoma dakika chache tu na kupata picha ya yanayotusumbua sisi, moja wapo likiwa hilo la kukosa teknologia sahihi. Sasa najiuliza, pamoja na kuwa na wasomi wote hawa tulionao sasa tunashindwa kabisa angalao kujua matatizo yetu yanatokana na nini, tunabaki kuwa watu wa kubahatisha tu? Juzi Rais Magufuli akadhani Jeshi litatumia vile viwanda kuuku tulivyokuwa navyo, jamaa (wataalam wetu) wanamwangalia tu, pengine wakichekelea! Nilliona picha ya wanajeshi wamepinda migongo wakibeba mashine, sijui walikuwa wanaipeleka wapi!

Magufuli angependa kuwa Dikteta wa ukweli, udikteta wake ulitakiwa ufanyike huko huko kwa watu wake huko serikalini, na sio huku uraiani. Hata mimi ningemuunga mkono. Hawa wasomi tulionao ni lazima wafanye kazi kama punda kama hawawezi kujituma wenyewe.

Kwa hiyo inawezekana sana kwa hawa wafanya biashara wetu hapa wanasita kuingia katika biashara hiyo kwa kujua ugumu huo. We have no technology needed to process the damn thing efficiently, and those who have the technology are reluctant to share!
No wonder, we hardly see any of those companies willing to set up here, even with the available incentives.

Narudi huko huko nilikoanzia. Suluhisho la matatizo yetu haya ni kuwapa wakulima uwezo. Acha waunde Ushirika wao na wawe na uwezo wa kila namna katika shughuli za mazao wanayoyalima.
 
Mengine yote nakubaliana na wewe lakini Ushirika kwa maana ya vyama vya ushirika siyo suluhisho. Vyama vya ushirika ndiyo chanzo kikuu kilichoitoa nchi hii kutoka msafirishaji wa kwanza wa mazao nje wa Afrika hadi kufikia omba omba wa kwanza.

Ushirika kama kampuni, Bakhresa na MO ni mfano mzuri nimeweka juu hapo. Hiyo ndiyo solution.

Kuhusu teknolojia, hilo si tatizo kubwa sana ingawa tunalo. Makampuni binafsi yana njia zao za ki intelijensia binafsi za kutatua hayo, yatapopewa fursa yataweza tu.
 
Una fikra zozote za utatuzi au ushauri au wewe ni Kama mke mwenza, unayoyafahamu ni matatizo tu bila kuwa na ufumbuzi?
Wewe Faiza umegundua tatizo... Asante sana sasa umeeweza kufikiria utatuzi bora ninini?
 
Kuna swali hujajiuliza, ni kwa vipi hao Wafanyabiashara hawajaiona hiyo fursa hiyo kwa miaka yote. Unadhani ni kwa sababu ya kutokuwa na fedha?
Swali zuri. Jibu ni rahisi; vyama vya msingi na vile vikuu pamoja na ushirika viliaminika na kuopewa chapuo zaidi na serikali. Kuwa, vingeweza kusimamia biashara hiyo jambo linaloonekana wazi kushindwa.
 
Ma shaa Allah, kaolewa yupo kwa mumewe.

Jikumbushe: https://www.jamiiforums.com/threads/bibi-nisamehe-najuta.971224/
 
Faiza, usisahau kale kakero ka slogan za Kijamaa bado kapo! Kuwa mnunuzi binafsi wa mazao huitwa " mlanguzi". Hadi wakulima husikika wakisema "tumelanguliwa" mazao yetu na mnunuzi fulani.
Bado kuna imani ndani ya serikali kuwa ushirika ndo kilakitu. Ushauri wako ni mzuri.
 
Hajweka pembeni hapo... We hauon kila dakika mbili bakhresa..

Utadhan mfanya biashara yuko mwenyewe.
Nitajie basi wafanya biashara wa kutukuka wa "food processing" Tanzania hii niwaweke.

Tatizo nini?
 
Hajweka pembeni hapo... We hauon kila dakika mbili bakhresa..

Utadhan mfanya biashara yuko mwenyewe.
Nitajie basi wafanya biashara wa kutukuka wa "food processing" Tanzania hii niwaweke.

Tatizo nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…