Pita pita zangu humu nimekutana na huu uzi na nimesoma mchango wako kuhusu zao la korosho ushahuri wako ni wa ujenzi.
Mimi napita naenda kunywa kahawa na kashata za karanga.
Ahsanta...
Hilo naunga mkono unakuta kiongozi ana ngangani kushindana na wafanyabiashara kujenga vitega uchumi badala ya kukusanya ushuru Mkurugenzi ana waza kujenga hoteli ya 5 Star mjini katikati Paradise cinema Dodoma wananchi wanampigia makofi hiyo hotel ikifilisika na helazetu zimekwenda umiliki usimamizi waachiwe wenye taaluma serikali fuatilia tozo kodiFaiza nakubaliana na ushauri wako. Pengine kuboresha huo ushauri Serikali ijikite zaidi kwenye kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na kuwekeza. Utoaji wa mikopo ya kuwekeza na kuendesha hizo biashara liwe jukumu la mabenki na taasisi nyingine za fedha. Kutokana na data zilizopo mabenki nchini yan
Mku kwa hali ilivyo hatawakitokea ikaisaidi sects binafsi hakuna unafuu wowote kwani RAIA fedha za kununua hizi bidhaa zitakazozalishwa.Mtoa mada upo sawa, serikali inabidi itoe support sector binafsi. Risk ni nyingi katika Biashara. Ilifanyika dhambi kuwabeza sector binafsi sakata la Korosho. Waombwe radhi tufungue ukurasa mpya. Wengi wenu kijani mlifisia sana maamuzi yale ya dharula yasiyo na tija.
SUKITA ifufuliwe ijenge viwandaUna fikra zozote za utatuzi au ushauri au wewe ni Kama mke mwenza, unayoyafahamu ni matatizo tu bila kuwa na ufumbuzi?
Kama unaziona fursa kelele za nini? Nenda kafunguwe kiwanda ubangue korosho uuze Saudia. Shida za hii nchi zinaletwa na wazee wa itikadi. Sioni KIPYA kwenye mada yako cha kukiita ushauri.Usemayo ni mawazo duni sana. Mbona kuna Watanzania wengi sana wamefanikiwa? Bakhresa ni mfano mzuri sana, alikuwa ana kiduka tu cha kushona makubadhi pale mtaa wa Uhuru.
Kila unapoona matatizo ufahamu kuwa kuna fursa, nnakushangaa sana wewe unashindwa kuziona fursa na unayaona makaburi tu.
Ni ushauri (wazo) ambalo bila shaka hao hao wafanya biashara wangekuwa na nia ya kuifanya biashara hiyo wasingekuwa wamesita kukopa kwenye mabenki na kwingineko, kama mashirika ya fedha duniani yanayokopesha na hata kuingia ushirika na wafanya biashara, kama International Finance Corp.(IFC) sehemu ya WB.Ushauri: Serikali ijitowe kimasomaso kuwakopesha bila riba wafanya biashara wakubwa wenye uzoefu wa viwanda kama vile akina Bakhresa na Mo kufunguwa viwanda vikubwa vya kisasa vya kubangua, kusindika na kufungasha korosho kwa kiwango cha Kimataifa na kuwasaidia kushindana na masoko ya Kimataifa.
Aiseee, wewe una lako jambo. Mbona huu ni mjadala mzuri tu wa kupeana mbinu?Kama unaziona fursa kelele za nini? Nenda kafunguwe kiwanda ubangue korosho uuze Saudia. Shida za hii nchi zinaletwa na wazee wa itikadi. Sioni KIPYA kwenye mada yako cha kukiita ushauri.
Matatizo ya nchi hii hayako kwenye mitaji, yapo kwenye sera. Post yangu ilikuwa inajibu post yake ambayo ilikuwa inajibu post ya member mwingine kwa kuyaita mawazo yake ni mawazo duni.Aiseee, wewe una lako jambo. Mbona huu ni mjadala mzuri tu wa kupeana mbinu?
Kwanza kumbuka kuwa kwenye mazao yapo aina mbili kuu, mazao ya chakula na mazao ya biashara.Mku kwa hali ilivyo hatawakitokea ikaisaidi sects binafsi hakuna unafuu wowote kwani RAIA fedha za kununua hizi bidhaa zitakazozalishwa.
Watazalisha then watabaki na bidhaa kwenye mastoo mpaka muda wa matumizi utaisha mwisho wanapeka dampo baada ya kukosa wanunuzi.
Mzunguko ukirudi kila kitu kitawezekana kabisa shida fedha hakuna
Tanzania tumezoweshwa mambo "complicated" ndiyo eti mazuri. Binafsi naamini the "simpler the best".Wazo Murua (Kiswahili fasaha?) kuhusu kukopesha wakulima wa korosho bila riba, nashauri pia hata mazao mengine ya biashara, wakulima wawezeshwe. Ingawa nilipoona kuhusu "tafakuri", nilitarajia kusoma andiko pana na lenye kila aina ya uchambuzi na udadavuaji, ajenda ikiwa zao la korosho. Unfortunately, mwandishi ametoa suruhisho rahisi kwa maada ngumu na pana. chonde chonde Madam Faiza..you're better than this....@FaizaFoxy
Nikidhani tafakuri "WANALIPWAJE"?
Tuangalie tumejikwaa wapi kabla ya kuangalia tulipoangukia...
Ni wazo jema "kuwakopesha hao wafanyibiashara" lakini kila mfanyibiashara ana soko na malengo yake "KWANINI HAWATAKI KUJENGA WALA KUJIHUSISHA NA UBANGUAJI KOROSHO?" "KWANINI WANAONUNUA KOROSHO GHAFI ZINAPELEKWA INDIA KUBANGULIWA?" Tukipata jawabu kwa maswali hayo tutapata mwanga...
Cha msingi TUACHE POROJO NA SIASA WAKULIMA WALIPWE ILI WASIJE KUSUSA AMA KUCHUKIA ZAO HILO.