TAFAKURI: Mpiga dili anaonekana mjanja kuliko anayetetea maslai ya umma!

MWANAHARAKATI MWEMA

Senior Member
Dec 16, 2022
192
270
Nawasalimu Kwa Jina la mwenyezimungu mwingi wa kusamehe, najaribu kutafakali kuhusu tabia za watanzania najaribu kulinganisha na mataifa mengi ya wazungu au wachina au wajapani kuhusu uzalendo wao.

Katika nchi ya Tanzania wafanyakazi wa umma wanafanya mambo ya ovyo Kwa Tamaa zao au kushawishiwa na mara nyingi Ni kutokana na jamii husika kudhihaki maisha ya muhusika hivyo kumbadilisha tabia, Kuna mambo ambayo katika jamii yanashangaza sana na ni ya kutia kinyaa Kwa nchi Maskini kama yetu.

Katika mifumo mingi ya kiserikali unakuta Kuna mazingira ambayo mengi si rafiki kupata huduma Kwa uharaka kiasi Kuna wakati muhudumiwaji unahisi hapa Hawa wahudu wanaitaji pesa au wahudumu wanakutengenezea mazingira utoe pesa.

Shida sio hiyo Shida ni pale wananchi wanakuwa waoga kudai haki Yao Kwa kuungana kushinikiza Jambo wanaloona haliendi Sawa na badala yake wanakubaliana kwamba hapa Bila pesa hutoboi hivyo wanasambaza ujumbe kwamba pale nenda na pesa wakati huduma Ile ingetolewa bule endapo wangeungana na kushinikiza kwamba Hakuna atakae toa pesa.

Jamii ya watanzania Ni jamii ambayo haina tabia ya kuungana kupinga uovu, Ni jamii ya watu waoga na waliokosa elimu ya kujitambua, Mimi Kuna nyakati uwa najisemea kwamba elimu umkomboa mtu mwoga japo Kuna muda uwa najisemea kuwa labda ni nafsi za jamii husika.

Kwa nini uwa Nawaza haya Ni Kwa Sababu Kuna jamii ya wahaya hawa jamaa mpaka ule pesa yake ya RUSHWA uwe umepambana sana, pia si waoga hata kigogo lakini wengi wameelimika, wapo watu wa mara japo sio wote namaanisha wakulya Hawa jamaa elimu 50/50 lakini sio waoga hata kidogo kwenye( Lisk ishuu) Yuko tayari kufa akipambania Mali si yake au yake lakini si kudai haki mabigwa wa shortcut, wachaga pesa Yao rahisi ili mradi apate anachotaka na wanajua kucheza na dili Hawa wazoefu WA fulsa.

Sasa kinachonishangaza Ni kwamba katika haya makundi na jamii nyingi zilizopo Tanzania licha ya kila jamii ina hulka Zake lakini ikitokea ikampata mtumishi ambaye ni mpenda haki na muwajibikaji na sio mwizi wa Mali ya UMMA, wao ndio umbadilisha huyo mtu Kwa kumpachika majina ya mjinga,atakufa umaskini,hajitambui,anazani atadumu hapo milele kiasi muhusika akisikia anaona kumbe nachelewa na kuanzia kufuja Mali za UMMA.

Najua wapo viongozi wa zamani wanaonekana Ni wajinga kwenye jamii zetu Kwa Sababu TU hawakuiba enzi za utawala wao lakini ukweli ni kwamba walifanya Kwa upendo lakini jamii Leo inawabeza, naitimisha Kwa kusema UFISADI,RUSHWA Ni zao la jamii husika kulea licha ya kwamba uwezo WA kuikataa IPO mikononi mwao.
Asante.
 
Siungi mkono hao watu, ila wasikilizwe wana hoja. Mtetea maslahi anakufa masikini, mpigaji ana uhakika wa maisha na kuongezewa. A case study of Paul Makonda and CCM at large
 
About heading.
Omba Moderator Wakufanyie uhariri. Neno TAFAKULI ni tusi
 
Usitegemee lolote katika nchi ya wapumbavu wanaowaza ngono, uchawi majungu na simba na yanga pekee.
 
Mtu mmoja anakula pesa ya hospital ambayo ingetibia watu laki na nusu anaweka kwa akaunti yake ale, huyo ji chizi kama machizi wengine mwisho anakufa anaiacha bank, mwingine anaitumbua kwa starehe anashindwa hata kuchonga dawati watoto wanakaa chini huku wamezungukwa na misitu kila kona, sasa hapo Ana raha gani ktk kuongoza? Anajivunia nn kwenye hiyo nafasi? Kuiba nacho kitu cha kujivunia?
 
Back
Top Bottom