Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,148
Ni swali lililoanza kurindima ndani ya vilinge vya siasa za wanaCCM kuhusu kuitikia au kuukacha wito wa kufika kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu ya CCM kwa wanasiasa wawili ndani ya CCM, yaani Yusuph Makamba na Mzee Kinana.
Taarifa ya kufika kuhojiwa kwa wanasiasa hao iliyoambatana video na picha ilitolewa na CCM yenyewe na vyombo vyote vya habari vikaitoa kwa umma kama ilivyo.
Hapo kabla kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya CCM zilizosema wanasiasa hao waligoma kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu kwa misingi kuwa hakuna kitu wataweza kubadilisha (maana maamuzi ya kuwafukuza ndani ya CCM yalishafanyika kitambo na kilichokuwa kinafanyika ni kuhalalisha tu) na hawana tena cha kupoteza au kupata kwa wao kuendelea kuwepo ndani ya CCM.
Lakini wakalazimishwa (chini ya ulinzi wa TISS?) kufika ofisi za Lumumba ili 'scene' ya kurekodi hilo tukio iweze kufanyika na vyombo vya habari vipate habari za kuandika kabla ya Mwenyekiti kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu leo. Lengo hasa likiwa ni kulinda heshima ya Mwenyekiti (maana anapenda kuonekana anaogopewa na kuheshimiwa na kila mtu)
Hapa ni baadhi ya dhana tafakarishi.
1. Kwanini Makamba na Kinana pasipo taarifa yoyote hawakufika Dodoma siku rasmi waliopaswa kufika na badala yake walifika Dar siku isiyo rasmi?
2. Kwanini mzee Makamba aliishia kupita na gari tu nje ya ofisi za CCM Lumumba huku akigoma kata kata kushuka na kuingia ndani ya ofisi?
3. Kwanini mzee Makamba na Kinana wafike ofisi za CCM wakitumia magari, madereva na wasaidizi kutoka idara ya...?
4. Kwanini wahusika wenyewe (Makamba na Kinana) wagome kusema kama wamehojiwa ama la, badala yake taarifa ya kuhojiwa kwao itolewe na CCM wenyewe?
5. Kwanini tukio la kudaiwa kufika na kuhojiwa kwa Makamba na Kinana lifanyiwe media coverage na ofisi ya CCM yenyewe badala wahusika wenyewe au vyombo huru tofauti kabisa na tukio la Benard Membe?