TAFAKARI: Hivi kweli Mzee Makamba alifika mbele ya kamati ya nidhamu ya CCM na kuhojiwa?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
9,995
34,607
Ni swali lililoanza kurindima ndani ya vilinge vya siasa za wanaCCM kuhusu kuitikia au kuukacha wito wa kufika kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu ya CCM kwa wanasiasa wawili ndani ya CCM, yaani Yusuph Makamba na Mzee Kinana.

Taarifa ya kufika kuhojiwa kwa wanasiasa hao iliyoambatana video na picha ilitolewa na CCM yenyewe na vyombo vyote vya habari vikaitoa kwa umma kama ilivyo.

Hapo kabla kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya CCM zilizosema wanasiasa hao waligoma kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu kwa misingi kuwa hakuna kitu wataweza kubadilisha (maana maamuzi ya kuwafukuza ndani ya CCM yalishafanyika kitambo na kilichokuwa kinafanyika ni kuhalalisha tu) na hawana tena cha kupoteza au kupata kwa wao kuendelea kuwepo ndani ya CCM.

Lakini wakalazimishwa (chini ya ulinzi wa TISS?) kufika ofisi za Lumumba ili 'scene' ya kurekodi hilo tukio iweze kufanyika na vyombo vya habari vipate habari za kuandika kabla ya Mwenyekiti kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu leo. Lengo hasa likiwa ni kulinda heshima ya Mwenyekiti (maana anapenda kuonekana anaogopewa na kuheshimiwa na kila mtu)

Hapa ni baadhi ya dhana tafakarishi.

1. Kwanini Makamba na Kinana pasipo taarifa yoyote hawakufika Dodoma siku rasmi waliopaswa kufika na badala yake walifika Dar siku isiyo rasmi?

2. Kwanini mzee Makamba aliishia kupita na gari tu nje ya ofisi za CCM Lumumba huku akigoma kata kata kushuka na kuingia ndani ya ofisi?

3. Kwanini mzee Makamba na Kinana wafike ofisi za CCM wakitumia magari, madereva na wasaidizi kutoka idara ya...?

4. Kwanini wahusika wenyewe (Makamba na Kinana) wagome kusema kama wamehojiwa ama la, badala yake taarifa ya kuhojiwa kwao itolewe na CCM wenyewe?

5. Kwanini tukio la kudaiwa kufika na kuhojiwa kwa Makamba na Kinana lifanyiwe media coverage na ofisi ya CCM yenyewe badala wahusika wenyewe au vyombo huru tofauti kabisa na tukio la Benard Membe?
 
Wazee hawapaswi kusumbuka sumbuka kusafiri kwanza hawana nauli.
Kilichofanywa na CCM ni kusaidia namna ya wao kuitikia wito wa chama chao.
Hakuna maswali hapo,cha muhimu walifika na kufanyiwa walichoitiwa full stop.
 
Usanii mtupu.....

Hao CCM ni mabingwa wa maigizo yanayofanyika katika "location" mbalimbali
 
Hayo ni mambo binafsi ya kifamilia na watamalizana wenyewe kwa wenyewe...wewe usiumize kichwa jiulize tu kwanini Dula mdogo wake Chid hakufika kwenye kikao cha usuluhishi baada ya kumpachika mimba chausiku mdogo wake uchebe
 
Haya tena nyie fisadi mnaoamini ccm haipendwi endeleeni na njozi zenu. Kama sio nyie basi mikakati ya upinzani kutunga uongo kuwatia moyo mashabiki wao ni hatari. Hii inapelekea kutoamini pale wanaposhindwa na ccm kwa kua wanaaminishwa ccm imekwisha na kwa ujinga wanaamini😝😝😝😝😝
 
Anzia hapa:

"Kamati ndogo imepewa siku saba..."

Siku saba za nini...? Kuna kazi kubwa kiasi gani cha kuandika ripoti ya mahojiano na watu watatu tu?

Humo humo, kuna 'damage control'; 'buying time'..., na makorokocho mengi mengine ya kuwahadaa maamuma.
 
Hahahaha jomba nashangaa unahangaikia mambo ya hawa wazee wa ccm wakati chama chenu kimewashinda..mwenyekiti wenu.anaendelea ma udikteta wake wa hakuna hukoji kitu, nyie mmekaa kimya tu..hamuwez mambo ya wazee hawa magwiji wa siasa..jifunzeni tu kutoka kwao lakini mkiwafuatilia mtaangukia pua
 
Anzia hapa:

"Kamati ndogo imepewa siku saba..."

Siku saba za nini...? Kuna kazi kubwa kiasi gani cha kuandika ripoti ya mahojiano na watu watatu tu?

Humo humo, kuna 'damage control'; 'buying time'..., na makorokocho mengi mengine ya kuwahadaa maamuma.
we unajua taratibu za ccm zikoje..usituchose na maswali yako。nenda kwanza kaulize matumizi ya fedha yaliyofisadiwa chama chenu kule na mwenyekiti wenu kwanza msijifanye kufumbia macho..haya ni mazito na ya msingi sana.kuliko hayo unayofuatilia sijui habari za siku ngapi...st..u.ppi.d. au mnataka kufanya kama kwa Lowasaa mnavizia wakitoka mje muwape wagombee urais halafu baadae wanarudi nyumbani kwao.ccm...hahahhaha...naona.hamjakoma.kuvizia.vizia makada wa ccm
 
Aisee kumbe wengi tunaojiuliza maswali kama hayo mojawapo ni kwanini Bashiru & Co. wazungumze na waandishi bila ya wahusika kuwepo? Ngoja tusubiri.
 
Niliogopa pale ambapo huyu Bash alipotaka kumfungulia mlango Maka halafu mzee akamwambia; Usiufungue mlango, sishuki... Ikabidi jamaa auegemee tu mlango kwa hisani ya mzee.
Kuna jambo linachemshwa hapo. Naona ka supu ya mawe
 
we unajua taratibu za ccm zikoje..usituchose na maswali yako。nenda kwanza kaulize matumizi ya fedha yaliyofisadiwa chama chenu kule na mwenyekiti wenu kwanza msijifanye kufumbia macho..haya ni mazito na ya msingi sana.kuliko hayo unayofuatilia sijui habari za siku ngapi...st..u.ppi.d. au mnataka kufanya kama kwa Lowasaa mnavizia wakitoka mje muwape wagombee urais halafu baadae wanarudi nyumbani kwao.ccm...hahahhaha...naona.hamjakoma.kuvizia.vizia makada wa ccm
Naona maoni yangu hayo yamekuumiza sana moyo.
 
Utachosha akili yako kisoda bure tu,kauze ndizi mbivu tu
Ni swali lililoanza kurindima ndani ya vilinge vya siasa za wanaCCM kuhusu kuitikia au kuukacha wito wa kufika kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu ya CCM kwa wanasiasa wawili ndani ya CCM, yaani Yusuph Makamba na Mzee Kinana.

Taarifa ya kufika kuhojiwa kwa wanasiasa hao iliyoambatana video na picha ilitolewa na CCM yenyewe na vyombo vyote vya habari vikaitoa kwa umma kama ilivyo.

Hapo kabla kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya CCM zilizosema wanasiasa hao waligoma kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu kwa misingi kuwa hakuna kitu wataweza kubadilisha (maana maamuzi ya kuwafukuza ndani ya CCM yalishafanyika kitambo na kilichokuwa kinafanyika ni kuhalalisha tu) na hawana tena cha kupoteza au kupata kwa wao kuendelea kuwepo ndani ya CCM.

Lakini wakalazimishwa (chini ya ulinzi wa TISS?) kufika ofisi za Lumumba ili 'scene' ya kurekodi hilo tukio iweze kufanyika na vyombo vya habari vipate habari za kuandika kabla ya Mwenyekiti kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu leo. Lengo hasa likiwa ni kulinda heshima ya Mwenyekiti (maana anapenda kuonekana anaogopewa na kuheshimiwa na kila mtu)

Hapa ni baadhi ya dhana tafakarishi.

1. Kwanini Makamba na Kinana pasipo taarifa yoyote hawakufika Dodoma siku rasmi waliopaswa kufika na badala yake walifika Dar siku isiyo rasmi?

2. Kwanini mzee Makamba aliishia kupita na gari tu nje ya ofisi za CCM Lumumba huku akigoma kata kata kushuka na kuingia ndani ya ofisi?

3. Kwanini mzee Makamba na Kinana wafike ofisi za CCM wakitumia magari, madereva na wasaidizi kutoka idara ya...?

4. Kwanini wahusika wenyewe (Makamba na Kinana) wagome kusema kama wamehojiwa ama la, badala yake taarifa ya kuhojiwa kwao itolewe na CCM wenyewe?

5. Kwanini tukio la kudaiwa kufika na kuhojiwa kwa Makamba na Kinana lifanyiwe media coverage na ofisi ya CCM yenyewe badala wahusika wenyewe au vyombo huru tofauti kabisa na tukio la Benard Membe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom