Matamshi ya Mzee Yusufu Makamba yasiyo na busara, yameiadhiri CCM kwa kiasi fulani!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,315
24,177
Busara ni kitu cha bure.

Na kwa kawaida mtu akiwa mzee, kama alivyo Yusufu Makamba, inategemewa na jamii zote duniani kuwa atakuwa anaongea mambo ya busara na yenye maonyo, yatokanayo na uzoefu mkubwa kimaisha.

Mimi ni mwana CCM, kada, ila sijapenda rap rap ya Makamba.
Maneno ya mzee Yusufu Makamba yanakosa mizania ya busara.
Ati watu wazuri hawafi, ndio maana Kinana yupo na Kikwete yupo!

That is rubbish by all means.
Tunashukuru mama Samia alilisahihisha hilo kabla ya mkutano kumalizika

CCM wajifunze kuwa kuna wazee ndani ya CCM hawana busara ya kutosha, mmoja wao ni Yusufu Makamba, Luteni mstaafu.

Miaka ya nyuma niliwahi kuandika kuwa CCM inaweza kufa, chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo, Yusufu Makamba.

Kabla ya kuongea na kadamnasi hadharani maneno ya Makamba hayana budi kupimwa mapema.
 
Busara ni kitu cha bure.
Na kwa kawaida mtu akiwa mzee, kama alivyi Yusufu Makamba, inategemewa na jamii zote duniani kuwa atakuwa anaongea mambo ya busara na yenye mainyi, yatikanayo na uzoefu mkubwa kimaisha...
Jidu,
Lisemwalo kwa nanma hii husemwa uchochoroni wakikutana wao kwa wao; huyu mzee ni kibri yake tu; anapima maji. Ni kweli ametapika chumvi ambayo iko moyoni kwake. Kurudi kubisha si rahisi.

Wewe unafikiri Samia siyo accomplice; she is one of the culprits !!

Go tell it to birds​

Nashangaa kuna watu wanajaribu kumtetea Mzee Makamba kwa ile kauli yake aliyoitoa jana.

Ukweli ni kwamba, kwa ile kauli aliyoitoa ya "watu wazuri huwa hawafi" katikati ya uwepo wa wajane, alikosea, tena alikosea sana.

Ndio maana Samia kwa kutambua hilo, akaomba radhi kwa niaba ya Mzee Makamba, akitamka pale ukumbini anajua hakuna ambaye hajafiwa na ndugu yake.

Hapa hakuna habari ya kuleta siasa au vinginevyo, Makamba alikosea anastahili kuambiwa ukweli ili ajirekebishe, na asitetewe kwa sababu zozote zisizo na mashiko.
 
Naunga mkono hoja ukitaka kufanya utafiti juu ya familia fulani kusema familia nyingine uliza watoto,Makamba ni mtoto katka familia ya CCM mzee asamehewe yawezekana muda huu yuko juani anatafuta jotoridi la mwili wake naomba kuwasilisha
 
Nashangaa kuna watu wanajaribu kumtetea Mzee Makamba kwa ile kauli yake aliyoitoa jana.

Ukweli ni kwamba, kwa ile kauli aliyoitoa ya "watu wazuri huwa hawafi" katikati ya uwepo wa wajane, alikosea, tena alikosea sana.

Ndio maana Samia kwa kutambua hilo, akaomba radhi kwa niaba ya Mzee Makamba, akitamka pale ukumbini anajua hakuna ambaye hajafiwa na ndugu yake.

Hapa hakuna habari ya kuleta siasa au vinginevyo, Makamba alikosea anastahili kuambiwa ukweli ili ajirekebishe, na asitetewe kwa sababu zozote zisizo na mashiko.
Pia pamoja na kauli ya rais Samia kumuombea radhi haitoshi,watu mkutanoni wameondoka na donge kadhalika watanzania kwa ujumla wamehudhunika wapo ambao hawawezi samehe kauli hiyo.
Kifupi ujuaji mwingi mbele giza
 
Mbona wajumbe walishangilia kwa makofi hiyo kauli?. Donge limetoka wapi Tena.
 
JamiiForums428144445_680x453.jpg
 
Tulia kijana hutoamini kitatokea. Mzee amelitafuta asilo lijuwa nilidhani kwa kukaa kwake jeshini anajuwa silence war ila ametoka nje ya mstari.
Makamba kweli kalitifua.
Hana ulimi wa busara.
Lakini kimsingi kalinanga kundi ka Mwendazake.
Mimi simpendi wa sikumpenda sana Mwendazake lakini kumkebehi katika hadhira ya chama sikuona busara yake.
 
Busara ni kitu cha bure.

Na kwa kawaida mtu akiwa mzee, kama alivyi Yusufu Makamba, inategemewa na jamii zote duniani kuwa atakuwa anaongea mambo ya busara na yenye mainyi, yatikanayo na uzoefu mkubwa kimaisha.

Mimi ni mwana CCM, kada, ila sijapenda rap rap ya Makamba.
Maneno ya mzee Yusufu Makamba yanakosa mizania ya busara.
Ati watu wazuri hawafi, ndio maana Kinana yupo na Kikwete yupo!

That is rubbish by all means.
Tunashukuru mama Samia alilisahihisha hilo kabla ya mkutano kumalizika

CCM wajifunze kuwa kuna wazee ndani ya CCM hawana busara ya kutosha, mmoja wai ni Yusufu Makamba, Kapteni mstaafu.

Miaka ya nyuma niliwahi kuandika kuwa CCM inaweza kufa chini ya Ukatibu Mkuu wa Yusufu Makamba.

Kabla ya kuongea na kadamnasi hadharani maneno ya Makamba hayana budi kupimwa mapema.
Kweli hakutoa maneno ya busara lakini Rais Samia Suluhu alilekebisha kauli hiyo
 
Nadhani yamemuadhirisha yeye mwenyewe na wanae sio chama. Substance hana na yawezekana na vijana wake pia wako hivyo sema connection za mzee zimewafikisha hapo walipo.
 
Mzee Makamba kwenye INTERVIEW jana alimuuliza mwandishi "Kwani wewe hutaki kulamba Asali....??😂😂😂
 
... miaka yote Luteni (sio Kapteni) YM pamoja na quotes nyingi za vitabu vitakatifu haijawahi kuwa na busara kabisa. Hubwatukabwatuka ovyo kama mwendazake.
Mkuu, nashangaa eti watu wamemuona jana tu kuwa hana busara! Mikutano mingi tu ya uchaguzi, huwa anapangwa 'KUMPAMBA' mgombea, mara zote huwa PUMBA tu anatapika. Kishampamba KIKWETE, MAGU, hata SAMIA pale alipoukwaa URAIS. Kote huko, alikuwa anaongea pumba tu!
 
Back
Top Bottom