TAFADHALI piga picha na wazazi wako

TAFADHALI piga picha na wazazi wako

R.i.p prof. Y. Bwatwa nilikua karibu yake miaka mingi iliyo pita alipenda kututania kuhusu kuongea kusalimiana na wazazi Kila asubuh japo hata kwa simu.

Prof Bwatwa ndie mwalimu wake na prof ndalichako.. mzee alikua mnyoofu kama rula

Alikuwa rafiki wa prof sarungi ni mtu wa mara pale bunda kwa wassira ni mzee alie ni shepu sanaaaaaa

Pumzika kwa amani profesa.
Nakumbuka kabla ya wazazi hawajaondoka duniani nilijiwekea ratiba ya kukaa nao siku nzima kila jumatano, jioni nawaacha narudi kwangu.

Hiyo kumbukumbu inanipa amani sana, bila kutenga mda kwa maksudi, hakuna namna itawezekana, mambo bado ni mengi.
 
Daah walishatengana ila ntafanya juu chini cku tukikutana pamoja ntachukua picha nao
 
Hiyo kitu imenishinsa aisee, kijiposition eti nipige picha dahhh🤣🤣🤣 kwanza sura yenyewe ya kupiga picha ninayo🏃🏃🏃. Sina picha hata moja na mamaangu just incase mmoja anakata moto right now inabaki story tu.
 
Gen Z chukueni huu ushauri. Kama una baba au mama hakikisha umepiga nao picha.
 
Kuna picha 3 ambazo hizi nimeziwekea frem kabisa,.

1, nilipiga na wazazi siku yangu ya kipamaira.
2. Nilipiga na wazazi siku ya graduation ya 4m 6.
3. Nilipiga na wazazi siku ya jubilee ya miaka 25 ya ndoa yao.

Kila nikiziangalia, Moyo wangu unasuuzika na kuwa mwepesi, nawapenda sana wazazi wangu.
 
Katika vitu ambavyo nimeshindwa ni kupiga picha zangu au na watu na nina simu yenye ubora mkubwa tu wa camera na siku niki kata kamba wadau wata hangaika sana kutafuta picha za kunipost kwamba rip.
Duh! Aisee 🤔
 
Back
Top Bottom