Tafadhali nisaidieni hesabu hii

Wageni watatu walikwenda kupanga chumba kwenye hoteli kilichokuwa kikipangishwa kwa Tshs 30,000. Kila mmoja alichanga shs 10,000 na kumkabidhi mhudumu. Bosi w ile hoteli alipoletewa zile pesa alimweleza mhudumu kuwa chumba kile bei yake ilikuwa ni Tshs 25,000 na sio 30,000, hivyo akamwamuru yule mhudumu awarudishie wale wageni watatu shs 5,000. Yule mhudumu alirudi na kuwakabidhi kila mmoja sh 1,000 kwani hakuwa na chenji kamili ( hivyo jumla Tshs 3,000) kisha yeye akabakiwa na shs 2,000. Hivyo ukiangalia ndio kusema kila mgeni alikuwa amechangia sh 9,000 kwenye kile chumba, hivyo jumla ni Tshs 27,000. na mhudumu alikuwa amebakiwa na shs 2,000, hivyo jumla tshs 29,000. Je shs 1,000 ilipotelea wapi?

Dear Afternoon, ooh samahani....., Dear Mchana;
(1) Wageni walitakiwa kutoa shs 8,333.33 kwa kila mmoja katika hali ya kawaida
(2) Wakafisadiwa na mhudumu na wakajikuta wametoa shs 9,000/= kila mmoja badala ya 8,333.33
(3) Assuming kwamba 2,000/= iliyobaki na mhudumu baada ya kurudisha chenji si ufisadi:
Hivyo NET UFISADI=(9,000-8,333.33)X3=1,000/=
Kwa kifupi tu ni kwamba the missing KILO ilibaki kwa mwenye Mali, na si kwa mhudumu.
Tunaomba tena nyingine of this kind!
 
Kama walirudishishiwa 1000 kila mmoja basi ndani ya hiyo 1000 kuna shs 333.3 kwa kila mmoja hivyo walilipa gharama za chumba shs 9333.3 kila mmoja.yani (9333.3x3)+2000=30,000/=.
 
Naona bado hamjamuelewa mchiziz hapo juu, swali liko hivi, kila mtu alitoa buku 10, na yule muhudumu aliwarudishia kila mtu buku (Zile buku 3), hii inaleta maana kuwa kila mtu alitoa buku 9, na 9 mara 3 ni elfu 27,000 na yule muhudumu alibaki na buku 2 hivo inakuwa jumla 29000, buku iko wapi?
 
Wageni watatu walikwenda kupanga chumba kwenye hoteli kilichokuwa kikipangishwa kwa Tshs 30,000. Kila mmoja alichanga shs 10,000 na kumkabidhi mhudumu. Bosi w ile hoteli alipoletewa zile pesa alimweleza mhudumu kuwa chumba kile bei yake ilikuwa ni Tshs 25,000 na sio 30,000, hivyo akamwamuru yule mhudumu awarudishie wale wageni watatu shs 5,000. Yule mhudumu alirudi na kuwakabidhi kila mmoja sh 1,000 kwani hakuwa na chenji kamili ( hivyo jumla Tshs 3,000) kisha yeye akabakiwa na shs 2,000. Hivyo ukiangalia ndio kusema kila mgeni alikuwa amechangia sh 9,000 kwenye kile chumba, hivyo jumla ni Tshs 27,000. na mhudumu alikuwa amebakiwa na shs 2,000, hivyo jumla tshs 29,000. Je shs 1,000 ilipotelea wapi?

Kama kila mgeni alichangia 9000 then hesabu inakuwa hivi
wageni 3 x 9000 = 27,000/=
Change kwa wageni ni 1000 @ kwa hiyo inakuwa 3000/=
Total iz 30,000/=

Kumbuka kwamba 9000/= is inclusive of what the waiter/waitress remained with i.e 2000/=

Hizi hesabu sio ngumu kihivyo, its just a brain teaser (chemsha bongo).
 
Kiufupi walitakiwa kulipa 30,000/- lakini bei ya chumba ikawa 25000/-, zikarejeshwa 5,000/- wakapewa 1,000/- kila mmoja so jumla ya pesa iliyorudi ni 3,000/-.

Muhudumu kachikichia 2,000/-...

so kwa hali hiyo hao jamaa watakuwa wamelipia chumba 27,000/- badala ya 25,000/- kumbuka 2,000/- aliyochukuwa muhudumu.

Kwa hicho chumba watakuwa wamelipia 27,000

3000 imerudishwa kila mmoja akapata 1,000.

So... 25,000 (bei halisi ya chumba)+ 2,000 (tip ya muhudumu) + 3,000 (waliyorejeshewa) = 30,000/-
 
Last edited:
Hivyo ukiangalia ndio kusema kila mgeni alikuwa amechangia sh 9,000 kwenye kile chumba, hivyo jumla ni Tshs 27,000. na mhudumu alikuwa amebakiwa na shs 2,000, hivyo jumla tshs 29,000. Je shs 1,000 ilipotelea wapi?

Mwenye hoteli wamempa shs 25,000, mhudumu wamempa shs 2,000 (jumla wametoa shs 27,000 = 9,000 x 3), shs 3,000 wanazo mfukoni :D.
 
Hesabu bado iko palepale chumba 25,000.wageni walirudishiwa sh 3,000 na muhudumu alibaki na sh 2,000 jumla 30,000
 
Wageni watatu walikwenda kupanga chumba kwenye hoteli kilichokuwa kikipangishwa kwa Tshs 30,000. Kila mmoja alichanga shs 10,000 na kumkabidhi mhudumu. Bosi w ile hoteli alipoletewa zile pesa alimweleza mhudumu kuwa chumba kile bei yake ilikuwa ni Tshs 25,000 na sio 30,000, hivyo akamwamuru yule mhudumu awarudishie wale wageni watatu shs 5,000. Yule mhudumu alirudi na kuwakabidhi kila mmoja sh 1,000 kwani hakuwa na chenji kamili ( hivyo jumla Tshs 3,000) kisha yeye akabakiwa na shs 2,000. Hivyo ukiangalia ndio kusema kila mgeni alikuwa amechangia sh 9,000 kwenye kile chumba, hivyo jumla ni Tshs 27,000. na mhudumu alikuwa amebakiwa na shs 2,000, hivyo jumla tshs 29,000. Je shs 1,000 ilipotelea wapi?

The PAYER (wageni) parted with Sh.27,000. The PAYEE (Hoteli + Mhudumu) received Sh. 27,000. (Hoteli ilipokea Sh. 25,000 na Mhudumu alipata Sh. 2,000). The books are balanced. Hakuna fedha iliyopotea. Huwezi kujumlisha kiasi alichopata Mhudumu (ambaye ni PAYEE) kwa kiasi walichotoa wageni (ambao ni PAYER).
 
Kama kila mgeni alichangia 9000 then hesabu inakuwa hivi
wageni 3 x 9000 = 27,000/=
Change kwa wageni ni 1000 @ kwa hiyo inakuwa 3000/=
Total iz 30,000/=

Kumbuka kwamba 9000/= is inclusive of what the waiter/waitress remained with i.e 2000/=

Hizi hesabu sio ngumu kihivyo, its just a brain teaser (chemsha bongo).

Kiufupi walitakiwa kulipa 30,000/- lakini bei ya chumba ikawa 25000/-, zikarejeshwa 5,000/- wakapewa 1,000/- kila mmoja so jumla ya pesa iliyorudi ni 3,000/-.

Muhudumu kachikichia 2,000/-...

so kwa hali hiyo hao jamaa watakuwa wamelipia chumba 27,000/- badala ya 25,000/- kumbuka 2,000/- aliyochukuwa muhudumu.

Kwa hicho chumba watakuwa wamelipia 27,000

3000 imerudishwa kila mmoja akapata 1,000.

So... 25,000 (bei halisi ya chumba)+ 2,000 (tip ya muhudumu) + 3,000 (waliyorejeshewa) = 30,000/-

Mwenye hoteli wamempa shs 25,000, mhudumu wamempa shs 2,000 (jumla wametoa shs 27,000 = 9,000 x 3), shs 3,000 wanazo mfukoni :D.

Nadhani maelezo yanaridhisha kiasi. Sasa tunaomba jibu la swali lililoulizwa :)
Hiyo 1,000 ambayo kwa haraka haraka ilionekana kana kwamba imepotea, iko kwa nani kati ya hao watu watano?
(Kuna Mhudumu, mmiliki, pamoja na wateja watatu)
 
kimsingi
walitoa 30,000
mwenye hotel achukua 25,000
baki 5000, halafu
wakarudishiwa chenji 3,000 (kila mmoja 1000 x 3)
mhudumu 2000

kimsingi hiyo 1000 iko mifukoni mwa hao wageni
 
Mwanzo walitoa 30,000. Hiyo ni hesabu tunaifanyia accounting kwanza.

Chumba 25,000/- Baki 5,000. Then wakarudishiwa alfu 3. Zikabaki alfu 2 kwa mhudumu. Jumla 30,000.

Accounting Na.2
Kila mmoja ametoa 9,000 x 3 = 27,000.
Chumba ni Tshs 25,000 + Mhudumu anayo 2,000 = Jumla ni 27,000.

Hakuna cha Alfu iliyopotea kwa sababu kilichofanyika ni transaction mbili tofauti. Huwezi kuunganisha transaction ya kwanza na ya pili na kupata balance. Maswala ya namna hii yapo kwenye fani ya benki pia. Ni mambo ya mzunguko wa pesa kwa hiyo transactions ni 2 sio moja
 
Wageni watatu walikwenda kupanga chumba kwenye hoteli kilichokuwa kikipangishwa kwa Tshs 30,000. Kila mmoja alichanga shs 10,000 na kumkabidhi mhudumu. Bosi w ile hoteli alipoletewa zile pesa alimweleza mhudumu kuwa chumba kile bei yake ilikuwa ni Tshs 25,000 na sio 30,000, hivyo akamwamuru yule mhudumu awarudishie wale wageni watatu shs 5,000. Yule mhudumu alirudi na kuwakabidhi kila mmoja sh 1,000 kwani hakuwa na chenji kamili ( hivyo jumla Tshs 3,000) kisha yeye akabakiwa na shs 2,000. Hivyo ukiangalia ndio kusema kila mgeni alikuwa amechangia sh 9,000 kwenye kile chumba, hivyo jumla ni Tshs 27,000. na mhudumu alikuwa amebakiwa na shs 2,000, hivyo jumla tshs 29,000. Je shs 1,000 ilipotelea wapi?

Wee Mchana, UMEDANGANYA!!!!!

Nashindwa kuamini kuwa watu wameamini kuwa WAGENI wakirudishiwa Elfu 1, basi watakuwa wametoa 27,000. Mambo yalikuwa hivi.
Walipotoa 10,000 na kurudishiwa elfu 5, ina maana kuwa karibu kila mtu alishapoteza tayari elfu 2. Hivyo ili uanzie kwenye 27,000, inabidi useme kuwa walitoa wote 24,000 (8,000x3). Zimebaki 6,000.
1,000 inaenda kwa mwenye hotel.
3,000 (3x1,000) wamerudishiwa.
2,000 zimechukuliwa na FISADI mhudumu.

YANGU INAFUATA:-
 
Mkuu Mchana, kwani ina maana 25,000 ukiigawa kwa 3 inakuja 8000? kwa maana 8000 ukiizidisha kwa 3 inakuja 24,000 kwahiyo unaona kabisa kwamba 1000 imekuwa fisadilized pale unaposema kwamba ukijumlisha na 1000 inakuwa 9000 baada ya hapo majibu yapo wazi
 
Train la umeme linatoka Berlin kwenda Bonn. Berlin iko mashariki ya Bonn. Upepo unavuma kutoka mashariki (Berlin) kwenda Magharibi (Bonn) kwa speed ya 50 km/hr. Hapa nina maswali mawili :-
1. Kwa nini Train linatumia saa moja na nusu kwenda Bonn na kurudi linatumia dakika tisini tu?

2. Je moshi wa train utapeperuka kwenda upande gani?
 
Train la umeme linatoka Berlin kwenda Bonn. Berlin iko mashariki ya Bonn. Upepo unavuma kutoka mashariki (Berlin) kwenda Magharibi (Bonn) kwa speed ya 50 km/hr. Hapa nina maswali mawili :-
1. Kwa nini Train linatumia saa moja na nusu kwenda Bonn na kurudi linatumia dakika tisini tu?

2. Je moshi wa train utapeperuka kwenda upande gani?[/QUOTE]

2. Train ni ya Umeme haiwezi toa moshi
 
Back
Top Bottom