Dawa ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa!

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,126
22,617
INTRODUCTON.

Leo naongea na wote wenye uhitaji wa pesa, Kila mpango wako kupata pesa umekwama,

Naongea na wote wenye ukata wa pesa, walioajiriwa na Wana mishahara lakini wanadaiwa Kila Kona, mshahara hautoshi.

Naongea na wenye biashara ndogo na za kati ambao wanafanya juhudi zote kujitoa walipo kiuchumi lakini wanazidi kudidimia kwenye dimbwi la Umaskini.

Naongea na wote wenye madeni Sugu Kila Kona, wangependa kulipa madeni hayo Ili wawe huru lakini hawaoni njia ya Kupata kipato kulipia, ndo wanawaza kukopa tena.

MY LIFE EXPERIENCE.

Nilipokuwa kidato Cha SITA, jobless, wakati nikisubiri mchakato wa kujiunga na chuo kikuu, nilirudi nyumbani kwetu.

Nikiwa nyumbani, nilipata shida sana kuishi nyumbani bila KAZI yoyote Kwa kipindi kile.

Siku moja, nilipewa pocket money na Mzee ya Tshs 20,000, nilikuwa na mahitaji mengi zaidi ya pesa niliyopokea, nilishukuru kupokea pesa hiyo kidogo na kuondoka kwenda kununua mahitaji yangu binafsi,

Nilinunua mahitaji machache na nilibakiwa na 2,000 tu.

Jumatano siku iliyofuata ilikuwa siku ya maombi Kanisani kwetu, niliondoka nyumbani mdogo mdogo nikielekea Kanisani, njiani nilinunua vitu vingine vidogo vidogo na kubakia na shs 600.

Nilianza kupata mawazo sababu pesa imeisha na mahitaji yangu hayajaisha na sijui lini tena ntabahatisha kupata pesa ingine.

Nikiwa njiani kuelekea Kanisani, niliwaza nisitoe sadaka niitunze hiyo 600 Ili ilinde mfuko wangu maana sikujua lini tena ntapata pesa,

Nikiwa katika kuwaza huko, ndipo lilinijia wazo la kumjaribu Mungu kupitia matoleo.

Niliwahi soma BIBLIA (Malachi 3:10-12). Nikakutana na andiko linaloongelea jinsi ya kumjaribu Mungu Kwa matoleo.

Niliwaza kuwa, sh 600 niliyonayo ni ndogo, isingenifikisha popote, kwanini nisiitumie hiyo kumjaribu Mungu?

Niliongea na Mungu ndani ya NAFSI yangu na kumwambia Mungu, Ewe mwenyezi Mungu, umesema katika neno lako kuwa nikujaribu Kwa matoleo na ZAKA Ili nisipungukiwe, Nami Leo hii naitoa pesa hii yote,akiba pekee niliyonayo Ili nione ikiwa utanibariki au la, nililenga kumjaribu Mungu kupitia neno lake.

Nilitoa sadaka Ile na kuondoka kurudi nyumbani, wakati natoa sadaka Ile ilikuwa saa tisa jioni,

Ilipofikia saa mbili usiku, nilipigiwa simu na Rafiki yangu ambaye Yeye baada ya kumalisha masomo, alipata ajira ya mkataba Mahali Fulani. Aliniambia kuwa anajisikia kunitumia pesa kidogo Kwa ajili ya matumizi madogo muda huu nikiwa Sina KAZI.

Haukupita muda, message mbili za mpesa ziliingia Kwa kufuatana, Nilipoangalia, alikuwa amenitimia 30,000/=

Tangu hapo, maisha yangu ya utoaji yalibadilika, Kila kipato nilichokipata nilitenga sadaka kwanza na kuinenea nilichotaka sadaka hiyo ifanye.

Hadi sasa navyoongea nawe, ninaishi maisha yangu vizuri sana, sio tajiri sana, lakini sipingukiwi na chochote ninachohitaji.

Nikiona naeekea kuishiwa, huchukua akiba kidogo niliyonayo huenda kuitoa nikinuia mahitaji ambayo ningependa Mungu anisaidie kuyatimiza na hujibiwa Kwa haraka sana.

USHUHUDA WA MWL MWAKASEGE.

Akiwa kwenye semina mahala Fulani, alitoa ushuhuda akisema:

Alipokuwa nje ya nchi Mungu alimsemesha apeleke sadaka Kwa mama mjane aliyeko Arusha. Baada ya kurudi nchini, alisahau kupeleka sadaka hiyo, baada ya muda kupita, alikumbushwa kwenda Kutoa sadaka Ile.

Alipofika Kwa mama yule mjane, alimkuta na alipomweleza alichoambiwa na Mungu kufanya, mama yule alijibu akisema, ameugua Kwa muda mrefu, na alikuwa akiuza nyanya na mboga sokoni, alipougua akashindwa kulipa ada ya wajukuu wanaomtegemea na Hali ikazidi kuwa ngumu.

USHUHUDA huu utupe kujua kuwa IPO haja ya kupendana na kusaidia majirani na watu wenye uhitaji na hatutapungukiwa

JINSI ZAKA,SADAKA NA MATOLEO YANAVYOFANYA KAZI.

Huzuia majanga kukuandama.
Wapo watu akipata tu mshahara, huja taarifa za misiba, wagonjwa, HASARA, Ajali Ili pesa ziende huko, pesa zikikata, matatizo yanapungua, ukipata tena pesa majanga haya hapa,

Ukitoa sadaka, matoleo ZAKA Mungu huzuia majanga hayo kukujia, na utashangaa pesa kidogo upatayo inakidhi mahitaji Yako yote.

SOLUTION.

-Kwa wenye Madeni.
Chukua pesa yote kidogo uliyonayo, tafuta mtumishi wa Mungu anayeishi maisha magumu, mpe sadaka hiyo, inenee sadaka Yako Yale Mungu ungependa akutendee.

-Kwa wanaopokea mshahara na haufiki mwisho wa mwezi.

Chukua mshahara wako Tenga sadaka kabla ya kufanya matumizi yoyote, peleka sadaka Yako Kwa maskini au wahitaji maskini, au hospitalini Kwa walioshindwa kulipa gharama za matibabu, au peleka Kwa mtumishi wa Mungu inenee sadaka Yako na utanipa majibu.

-Wazee wa betting.

Chukua pesa ambayo umepanga kupeleka betting, nenda tafuta familia maskini, wanunulie chakula na mahitaji, inenee sadaka Yako ukimwambia Mungu, nakujaribu Kwa sadaka hii, utaniambia majibu.

- Kwa Wafanyabiashara.

Chukua pesa kwenye mtaji wako, usitoe mabaki, Chukua sadaka kubwa itakayokuuma, ichukue peleka Kwa wahitaji mahispitalini, wapewe ombaomba barabarani, au toa Kwa wahubiri INJILI mabarabarani Kisha mwambie Mungu kuwa unamjaribu Kwa kupitia neno lake mwenyewe na asipolitimiza ni Yeye sasa.

HAKIKA Mungu hawezi vumilia jaribu Hilo, atakujibu haraka iwezekanavyo, Mimi nakushuhudia maisha ninayoishi halisi Hadi Leo.

NB: Wanaokwenda Kwa Waganga na wachawi kutafuta utajiri ni "WAPUMBAVU" Kwa maana Mungu ameruhusu ajaribiwe kupitia matoleo na hawezi shindwa kuwajibu sawasawa na NENO lake.

Amen.

Karibuni Kwa maswali na shuhuda Kwa watakaochukua ushauri huu na kuufanyia KAZI🙏
 
Pia wale wenye kupoteza pesa ktk mazingira tatanishi, wanaosumbuliwa na CHUMA ulete madukani ktk biashara zao,

Tumia njia hiyo hiyo, Chukua sadaka, inenee uyatajayo sadaka hiyo iyatimize,

Peleka pesa hiyo Kwa wahitaji, au Kwa wahubiri INJILI mitaani nk nk, walemavu, au wagonjwa hospitalini.

HAKIKA utajibiwa haraka sana, na tatizo la kupoteza pesa litakoma.

Amen
 
Na mimi nilikuwa namaliza mshahara kabla ya mwisho wa mwenzi nikaanza kutoa sadaka kiasi fulani each month kwa mungu nikimuomba huo mshahara uwe unatoboa mwisho wa mwenzi.

Huwezi kuamini hiyo mbinu ilifanya kazi....Unakuta mpaka mwisho wa mwenzi bado nina kasalio maajabu ya musa lazima kuna namna hiyo sadaka hunirudia kwa namna ya ajabu yaaani nitakutana hata na mtu atanipa tu sijaifanyia kazi au nitakuta tu kwenye nguo zile pesa ukijaa unasahau niliwekaga kiasi fulani sehemu fulani.....Ajabu jengine nisipotoa hiyo sadaka mshahara tar..20 umeshaisha! Nakuwa na madeni utitiri. Matomaso yatakataa.

La mwisho mimi si mtu wa magomvi kuna ms.Ng. Akaingia anga zangu ananichokoza sijamkosea chochote..,hata sikumsemesha nikatoa sadaka nikamwambia mungu kama uishivyo...Siendi kwa waganga nakuabudu na nakuamini basi andaa meza machoni pa adui yangu. Ni stori ndefu ila nadhani yule mtu alijuta sana kunichokoza sikufungua mdomo alipambana na mungu mwenyewe.,. Sina motive ya kubadili uwazavyo wewe fanya maisha yako haya ni ya kwangu mimi ukiamini sawa usipoamini pia ni sawa hainipungizii wala kuniongeza chochote.
 
(Malachi 3:10-12). The bible says.

Leteni ZAKA kamili ghalani, ilii kiwemo chakula katika nyumba yangu, "MKANIJARIBU" Kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi, mjue kama sitawafungulia "MADIRISHA" ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la.


Nami Kwa ajili yenu nitamkemea alaye, Wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, Wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.

Na mataifa yote watawaiteni kheri maana mtakuwa Nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.

Aamen.
 
Niombee nami mtumishi
Hapa huhitaji kuombewa ndugu,

Chukua kidogo ulichonacho sasa hivi nenda Kwa bibi yoyote Mzee, au mjane au yatima, au mtumishi wa Mungu,mpe sadaka hiyo, au nunua chakula kidogo, peleka saa hii,

Mwambie Mungu moyoni mwako kuwa ni akujaribu Kwa sadaka hii sawasawa na NENO lako katika (Malachi 3:10-12).

Usipojibiwa, Rudi uniambie nikurudishie sadaka Yako.

Mungu Si mtu aseme uongo, Wala Si mwanadamu adanganye.

Amen.
 
Na Mimi nilikuwa namaliza mshahara kabla ya mwisho wa mwenzi nikaanza kutoa sadaka kiasi Fulani each month Kwa Mungu nikimuomba huo mshahara...
Barikiwa mwana wa Mungu,

Umenikimbusha mtumishi mmoja wa Mungu amewahi tumia 5000 akiba pekee aliyoitinza kwenye coat Kwa miezi kadhaa,

Siku aliposema hizi pesa mbona natoa Kila siku haziishi, zilikata hapo hapo.

Mungu yupo,

Na hakuna jambo Rahisi kupata pesa kirahisi kama Kutoa Kwa kumjaribu Mungu.
 
Back
Top Bottom