Mchana
Senior Member
- Sep 27, 2007
- 183
- 16
Wageni watatu walikwenda kupanga chumba kwenye hoteli kilichokuwa kikipangishwa kwa Tshs 30,000. Kila mmoja alichanga shs 10,000 na kumkabidhi mhudumu. Bosi w ile hoteli alipoletewa zile pesa alimweleza mhudumu kuwa chumba kile bei yake ilikuwa ni Tshs 25,000 na sio 30,000, hivyo akamwamuru yule mhudumu awarudishie wale wageni watatu shs 5,000. Yule mhudumu alirudi na kuwakabidhi kila mmoja sh 1,000 kwani hakuwa na chenji kamili ( hivyo jumla Tshs 3,000) kisha yeye akabakiwa na shs 2,000. Hivyo ukiangalia ndio kusema kila mgeni alikuwa amechangia sh 9,000 kwenye kile chumba, hivyo jumla ni Tshs 27,000. na mhudumu alikuwa amebakiwa na shs 2,000, hivyo jumla tshs 29,000. Je shs 1,000 ilipotelea wapi?