Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,329
Barubaru,
..unaposema Waswahili wamewekeza una maanisha wale wenye nywele za singa?
..je, wenye nywele kipilipili wana kasoro gani wasiweze kuwekeza kwenye biashara ya mafuta, majumba, etc etc?
..katika kutembea kwangu nchi hii sijaona mswahili mwenye nywele za singa ameshika jembe analima.
..nadhani wanaozungumziwa hapa kwamba wana hali ngumu ni wana Tabora, Wanyamwezi kindakindaki.
..kuna MIFUMO imekuwepo TANGANYIKA tangu enzi za UKOLONI ambayo inazuia wenye nywele za kipilipili kumiliki BIASHARA KUBWA.
Nafikiri unatakiwa kujitambua na kuacha kuficha ukweli na kutukuza uongo.
Hakuna Sera hiyo (NILIPO RED) kwani huo utakuwa ubaguzi wa rangi jambo ambalo TZ ni muasisi wa sera hiyo sio tu ndani ya Afrika bali pia katika UN.
Mimi nimekaa sana Tanzania na kufanya kazi sana Tanganyika katika mikoa mbalimbali. Tabora ni asli nako na najua fika kuwa watu wenye nywele ngumu wamekuwa waoga sana kujenga kwao nyumba nzuri au kuanzisha investment kubwa kubwa kwao wakiogopa Uchawi na kurogwa, kitu ambacho kwa waarabu au wahindi hakipo kabisa.
Kwa waarab tuna usemi mmoja (nitauweka katika tafsiri isiyorasmi kwa kiswahili). Waarabu wanasema, Kila palipo mwan'Adam unapimwa kwa kile unachoifanyia jamii kwa mikono yako, mali yako na ilmu yako. Na Mola atakulipa kwa hilo"
sasa utaona waarabu pale wanapoishi lazima wawekeze kwani ndio kwao na watalipwa na Mola kutokana na huduma zao kwa jamii ile na sio ilmu au utajiri wao kuutumia kibinafsi.
Hizo tofauti mbili ndio zinaifanya Tabora waarabu na wahindi wengi kuwekeza sana katika sekta mbalimbali. Wana wa Asli ndio kwanza wamezinduka na kuanza kuwekeza.
Binafsi nampongeza sana RAGE kuanza kuonyesha mwanga na chachu la kuizindua Tabora katika usafiri na mawasiliano ya radio na mengine mengi. Tushikamane kuikomboa Tabora yetu.