Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Safi daktari endelea kuwafunua mafisadi waliojificha ndani ya chama tawala najua magamba ndani ya chama tawala ni mengi na hayawezi kuisha wakisema wayamalize yote basi chama chote kitakufa.
 
ndio maana mzee aling'oa mabomba na koki zake kule mtela...........hili sitalisahau........na kwakuwa sasa hivi amewekwa kwenye list atuthibitishie kuwa hakuiba............

- Hana sababu ya kuthibitisha anything kama vile Chadema ambavyo hawana sababu ya kuthibitisha anything kuhusu kupewa hela toka nje kuleta vurugu nchini.

William @ NYC, USA.
 
- Hana sababu ya kuthibitisha anything kama vile Chadema ambavyo hawana sababu ya kuthibitisha anything kuhusu kupewa hela toka nje kuleta vurugu nchini.William @ NYC, USA.
Mkuu,nimekuwa nathamini sana michango yako lakini nadhani kwa vile damu ni nzito kuliko maji,naona umeamua kuzipa likizo busara zako.Kuna usemi kuwa mahakama ya umma ina nguvu zaidi ya mahakama ya kisheria.Walichofanya Chadema ni kumshtaki Malecela kwa umma (yaani mahakama ya umma).Sasa haihitaji hata busara ndogo tu kumaizi kuwa mwanasiasa huyo ambaye ameutumikia umma kwa miongo kadhaa asingependa akumbukwe zaidi kwa kutajwa kama fisadi badala ya kumbukumbu nyingine njema.

Upo Marekani,na una upeo mkubwa wa siasa za kimataifa.Sitaki kuamini kuwa ndani ya moyo wako unaamini kuwa Chadema wanapewa fedha kutoka nje kuchochea vurugu nchini Tanzania.Katika global financial crisis hii ni nchi gani yenye hela za kuchezea kwa kuzimwaga kwa Chadema ili isababishe vurugu Tanzania?Na baada ya vurugu hizo,Chadema itanufaika vipi?Au baada ya fedha hizo kumwagwa,hao wafadhili watanufaika vipi?Nani anayeweza kuwekeza kwenye vurugu?

Kama nilivyokushauri jana,iwapo mzee wako anaamini kuwa amezushiwa tu tuhuma hizo za ufisadi,basi afanye uungwana wa kwenda mahakamani kudai amekashifiwa.Mahakama ya sheria inaweza kumsafisha iwapo hatokutwa na hatia,na mahakama ya umma pia itaridhia hukumu hiy😵therwise,unaweza kuendelea kusema kila baya dhidi ya Chadema-kwa mfano tuhuma hizo za kupokea fedha kutoka nje kuchochea vurugu-lakini unfortunately,hiyo haitosaidia kumvua mzee Malecela joho la ufisadi alilovikwa na Chadema.

- Chadema mbona hawajaenda mahamamani kumshitaki Sophia Simba mkuu, au?

William @ NYC, USA.

Duh,this is too low.Kwanza,Chadema ni political organisation sio an individual.Pili,Chadema hawajatangaza kinyume cha dhamira yao ya kumshtaki Sophia Simba.Last we heard from them ni kuwa wanakusudia kumshtaki.Third,two wrongs do not make a right.Kama Chadema hawajamstaki Sophia Simba kwa tuhuma mfu ambazo hata wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa walizitolea macho to an extent mwanamama huyo mropokaji akaruka kauli yake,haimaanishi kuwa Mzee Malecela naye asiende mahakamani kukanusha tuhuma kuwa naye ni fisadi.

It's not too late kuzingatia ushauri huu.Unaweza kupoteza nguvu nyingi kumtetea lakini ukweli ni kwamba historia imetufundisha kuwa utetezi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi haujaweza kufanikiwa.
 
Kaka pole na uchovu, niko Dodoma Sasa hivi namalizia shughuli zilizotuleta hapa na majira ya saa moja jioni nitakuwa Dar es salaam Naangalia mpira na kinywaji baridi kufurahia jinsi tulivyowapiga bao CDM na ilani yao ya UFISADI, sasa haina market tena na hii inatokana na kile tulicho kiona Tabora jana jioni.

Unaishi dunia gani?Hakuna aliyepigwa bao bali kuna ALIYEJIPIGA BAO.Mlitumia nguvu nyiiiiingi kukanusha kuwa chama chenu sio cha kifisadi.Mkasimama majukwaani na mafisadi na kuwapigia kampeni huku mkidai ni watuhumiwa tu.Sasa maji yalipozidi unga mkalazimika kulamba matapishi yenu na kukiri hadharani kuwa miongoni mwenu kuna mafisadi.Halafu bila aibu wala fikra unathubutu kusema mmeipiga bao Chadema!

Ilani ya ufisadi sio ya Chadema pekee bali kila Mtanzania.Na hata kama ingekuwa yao,basi huo ni uthibitisho tosha kuwa ninyi sio tu mmepigwa bao la kubakwa bali pia mmeolewa kwa mahari ya noti feki KWANI NI NYIE MLIOLAZIMIKA KUFUATA MATAKWA YA CHADEMA.

SHAME ON YOU,FISADI
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huyu dkt Slaa hana lake jipya, na hatimaye baada ya kuisaidia CCM kutoka nje atarudi kulekule alikotoka kama wenzake wengi wanavyofanya.Tambwe Hiza,Akwilombwe......
Chama cha upinzani halisi ni CUF tu.

Ama kweli mchanganyiko wa bangi na karafuu mbaya.Upinzani halisi ni CUF?Is that a joke?Wapuuzi nyie mliuawa na CCM kwa kudai haki yenu lakini mkapumbazwa na Mungu wenu Seif Shariff na mmeufyata kwa viongozi wenu wawili watatu kuingizwa ndani ya serikali ya CCM.

Unadhani CUF ina maisha marefu?Mtasema nini kwenye uchaguzi mkuu ujao?Mtawadanganya vipi wapiga kura ilhali ninyi pia ni sehemu ya serikali?

It's like a sad case ya kubakwa kisha kumruhusu mbakaji akuoe bila mahari.You should be ashamed of yourself
 
Nina maoni yafuatayo kuhusu hii list mpya ya Mafisadi:

1. Uwezekano mkubwa ni kuwa CHADEMA wanataka sasa kuisambaratisha CCM baada ya kuona hoja yao ya UFISADI ya awali "imemtoa nyoka pangoni" kwa CCM "kujivua gamba" na "kuwa na nia ya kufukuza mafisadi katika chama".

2. Leo hii katika CCM: Mang'ula; Malecela na Magufuli ni members ambao kwa macho ya wana CCM na mashabiki wao walio wengi ni WASAFI na si MAFISADI. Kwa hiyo ina maana kwa kuwaweka katika kundi la mafisadi na kama kuna ushahidi mzito na unaokubalika kisheria na kisiasa ina maana CCM kwa asilimia kubwa itakuwa imejaa ufisadi.

3. Kama CCM au individuals waliotajwa hawatasimama na kutoa ushahidi wa kutosha na kuridhisha ku-prove their innocence na kuwa allegations za CHADEMA ni za uongo, basi mafisadi katika list ya awali hawatatoka katika chama. Wakilazimishwa kutoka, nao watadai walio katika list mpya watoke: this will mean mkorogano mkuu katika CCM na kama itakuwa handled vibaya ina maana CCM itaporomoka zaidi.

4. for sure kutakuwa na list mpya itakayohusisha mafisadi wa "Stimulus Package" lakini inawezekana unasubiriwa wakati mwafaka na ushahidi upatikane.

5. CCM wataendelea kucheza ngoma ya CHADEMA na wadau wengine mpaka hapo CCM itakapovaa nia ya dhati ya kukisafisha chama na kuwafukuza mafisadi wote CCM na Serikalini na kuwachukulia hatua za kisheria sambamba na kufanya mageuzi ya kweli katika matumizi ya pesa za walipa kodi.

Respect.

QED.

Wanaweza kutukana,kukashifu na kuidharau JF lakini kwa analysis kama hii ni ushuhuda tosha kuwa mahala hapa ni patakatifu zaidi ya Ikulu ya Kikwete.

Yani kuna wazalendo wanaangalia mambo katika angle ambazo inahitaji upeo wa hali ya juu sana kufikiria huko.Mkuu umeniamsha sana katika analysis hii.

Kwa hakika Chadema wanaangalia mbali sana.Kuibua orodha hii mpya kutazua sokomoko la kufa mtu ndani ya CCM.Itakuwa ni atacks,counterattack na mbinde nyingine kama hizo.

Excellent analysis mkuu.You truly are a SUPERMAN
 
Halafu,ushaidi wa kimazingira tu unatosha kum-implicate Malecela na ufisadi uliokuwa unaendelea ndani ya CCM.Kwa mfano,kwani wakati akina Warioba na wakongwe wnegine ndani ya CCM walikuwa radhi kutengwa na wana-CCM wenzao kwa kukemea ufisadi hadharani,Mzee Malecela amekuwa kimya as if ni kiziwi wa kelele dhidi ya ufisadi.Yawezekana alikuwa anafahamu fika kuwa anaishi kwenye jumba la vioo na akianza kurusha mawe atadhurika.

Honestly,sijawahi kumsamehe Malecela tangu atoe kauli yake ya "THEY CAN GO TO HELL".Na pamoja na the so called busara zake,hakuwahi kuwaomba radhi Watanzania kwa matusi hayo.

Hofu yangu ni kwamba huyu mzee alishamalizwa kisiasa na Lusinde.Sasa wakati anaendelea kuuguza machungu ya kubwagwa ubunge,anakumbana na kimuhemuhe kingine cha kutajwa kuwa ni fisadi.Only time could tell hatma ya maisha yake.
 
Mkuu William, with due respect again, hoja nilizokupa ni facts, facts huwa zina supportive evidence, hivyo you are wrong Sir once again. Kwa vile mimi nimetoa facts yenye hoja nzito na wewe ikazipamgua kwa hoja nyepesi, nikuweke evidence humu it will prove you wrong nakuomba ujitidhishe tuu mwenyewe kwa haya yafuatayo.

I. Pata taarifa ya CAG ya ukaguzi wa EPA soma majina ya waliohusika na EPA halafu ufanye reference na waliotajwa, utagundua sio wote waliohusika, wametajwa kwa majina.

2. Soma tena majina ya hao waliotajwa ufanye reference ya majina ya waliofikishwa mahakamani utagundua kuna waliotajwa na hawakufikishwa mahakamani na hawatafikishwa!.

3. Nimekusisitizia itetee CCM as chama that it did nothing wrong in EPA scandal, if CCM did something wrong no matter nani alisaini, viongozi wote wa juu kwenye ngazi za maamuzi hawawezi kukwepa 'collective resiponsibility' kwa makosa ya chama.

4. Hili la true colors, hizi ndizo rangi zangu daima dumu, mimi ni mkweli daima niko crystal clear, I don't beat around the bush, I just speak my mind. The truth has a cost, nimesha ilipa sana gharama ya kusema ukweli. I've even paid by my job na kugeuka jobless. Just tell the truth, and the truth will set you free. I'm free!.
 
Mkuu,nimekuwa nathamini sana michango yako lakini nadhani kwa vile damu ni nzito kuliko maji,naona umeamua kuzipa likizo busara zako.Kuna usemi kuwa mahakama ya umma ina nguvu zaidi ya mahakama ya kisheria.Walichofanya Chadema ni kumshtaki Malecela kwa umma (yaani mahakama ya umma).Sasa haihitaji hata busara ndogo tu kumaizi kuwa mwanasiasa huyo ambaye ameutumikia umma kwa miongo kadhaa asingependa akumbukwe zaidi kwa kutajwa kama fisadi badala ya kumbukumbu nyingine njema.
- Kumshitaki kwa umma kiongozi aliyepumzika na siasa ni dalili za siasa za Desparation za kutaka kumuingiza kila mtu kwenye siasa za kuropoka ropoka, ili kujipatia attention kwa mshitaki, sasa kama unaijua vizuri siasa unajua kwamba huyu sasa amefika mwisho hana agenda tena sasa anajaribu kuanzisha agenda isiyokuwepo ili kuendelea na zile 15 minutes of fame ambazo sio siri kwamba sasa zimefika mwisho. Kwa mwendo huu mpya wa Slaa hata neno fisadi linakosa maana kabisa mkuu, ingawa ni hadithi nzuri kwa media, elewa kwamba wananchi sio wajinga na hizi siasa za kulipua mabomu hata kama hayapo haziwezi kuisaidia Chadema kwenda mbele.

Upo Marekani,na una upeo mkubwa wa siasa za kimataifa.Sitaki kuamini kuwa ndani ya moyo wako unaamini kuwa Chadema wanapewa fedha kutoka nje kuchochea vurugu nchini Tanzania.Katika global financial crisis hii ni nchi gani yenye hela za kuchezea kwa kuzimwaga kwa Chadema ili isababishe vurugu Tanzania?Na baada ya vurugu hizo,Chadema itanufaika vipi?Au baada ya fedha hizo kumwagwa,hao wafadhili watanufaika vipi?Nani anayeweza kuwekeza kwenye vurugu?
- Well kwa mwendo huu wa Slaa ni kwamba ni fair kila mwanasiasa kukurupuka na kuanza maneno ya kizushi, ili mradi yashile the media attention, mimi mkuu ninasema hivi Tanzania hatuna sheria ya Political finance Campaign kwa hiyo ni sawa kwa chama cha siasa kupokea pesa toka mahali popote pale, however kama unamshitaki kiongozi yoyote kwa wizi wa benki basi ni lazima uwe na karatasi linaloonyesha kwamba amesaini na zile pesa kuchukuliwa, lakini ukisema chama cha yule kiongozi kilipewa hela ndio hapo sasa unakuja mtego wa Political Campaign Finance Laws ambazo bongo hatuna, kwa sababu huwezi with a straight face kusema vyama vyote vya siasa Tanzania vinapokea hela safi kisheria na ukichunguza ukagundua ukweli wa uchafu wake basi viongozi wote wa kile chama ni mafisadi, please Mkuu chadema wanapewa hela na ile Charity ya Tony Blair ambayo pia ndio wanaompa hela Tshangarai kule Zimbabwe, sasa kweli unasema ukizichunguza hizo hela zitakuwa na usafi 100%? Na zisipokuwa basi viongozi wote wa Chadema sio wasafi? Pleasee!

Kama nilivyokushauri jana,iwapo mzee wako anaamini kuwa amezushiwa tu tuhuma hizo za ufisadi,basi afanye uungwana wa kwenda mahakamani kudai amekashifiwa.Mahakama ya sheria inaweza kumsafisha iwapo hatokutwa na hatia,na mahakama ya umma pia itaridhia hukumu hiy😵therwise,unaweza kuendelea kusema kila baya dhidi ya Chadema-kwa mfano tuhuma hizo za kupokea fedha kutoka nje kuchochea vurugu-lakini unfortunately,hiyo haitosaidia kumvua mzee Malecela joho la ufisadi alilovikwa na Chadema.
- Malecela atakuwa mwendawazimu kwenda kumjibu Slaa anywhere kwa sababu atakuwa anajiingiza kwenye mtego wa Slaa wa kujitafutia umaarufu kwa nguvu hata kama time imekwisha, Malecela sio kiongozi wa taifa tena hahitaji kwenda popote, isipokuwa ni haki yangu kujadili anything humu JF kama mwananchi wa Tanzania, na ndicho ninachofanya hayo mengine ni yako mkuu!
Duh,this is too low.Kwanza,Chadema ni political organisation sio an individual.Pili,Chadema hawajatangaza kinyume cha dhamira yao ya kumshtaki Sophia Simba.Last we heard from them ni kuwa wanakusudia kumshtaki.Third,two wrongs do not make a right.Kama Chadema hawajamstaki Sophia Simba kwa tuhuma mfu ambazo hata wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa walizitolea macho to an extent mwanamama huyo mropokaji akaruka kauli yake,haimaanishi kuwa Mzee Malecela naye asiende mahakamani kukanusha tuhuma kuwa naye ni fisadi.
- Ha! ha! hapa imenibidi nicheke kwamba kwa vile Chadema hawajaenda mahakamani basi sio lazima na Malecela asiende mahakamani, hilo limenivunja mbavu mkuu na sina la kuongeza zaidi!

William @ NYC, USA.
 
Mkuu William, with due respect again, hoja nilizokupa ni facts, facts huwa zina supportive evidence, hivyo you are wrong Sir once again. Kwa vile mimi nimetoa facts yenye hoja nzito na wewe ikazipamgua kwa hoja nyepesi, nikuweke evidence humu it will prove you wrong nakuomba ujitidhishe tuu mwenyewe kwa haya yafuatayo.
I. Pata taarifa ya CAG ya ukaguzi wa EPA soma majina ya waliohusika na EPA halafu ufanye reference na waliotajwa, utagundua sio wote waliohusika, wametajwa kwa majina.
2. Soma tena majina ya hao waliotajwa ufanye reference ya majina ya waliofikishwa mahakamani utagundua kuna waliotajwa na hawakufikishwa mahakamani na hawatafikishwa!.
3. Nimekusisitizia itetee CCM as chama that it did nothing wrong in EPA scandal, if CCM did something wrong no matter nani alisaini, viongozi wote wa juu kwenye ngazi za maamuzi hawawezi kukwepa 'collective resiponsibility' kwa makosa ya chama.
4. Hili la true colors, hizi ndizo rangi zangu daima dumu, mimi ni mkweli daima niko crystal clear, I don't beat around the bush, I just speak my mind. The truth has a cost, nimesha ilipa sana gharama ya kusema ukweli. I've even paid by my job na kugeuka jobless. Just tell the truth, and the truth will set you free. I'm free!.

- Hamna jipya hapa zaidi ya kwamba eti kwa vile CCM imewahi kupokea hela chafu basi viongozi wote wa CCm ni mafisadi ndipo ninapouliza zile hela za Chadema toka kwa Tony Blair alizopewa na Gadafi kumsafisha na yale mauaji ya wananchi wa marekani 350 kwenye ile ndege aliyoibomu kule Lockerbee, unasema ni safi? Sasa kwa vile Chadema wanazipokea zile hela unasema na wao wana damu ya wale wananchi 350 waliokufa kwa kuuliwa na Gadafi?

- It does not make a sense at all!

William @ NYC, USA.
 
JK hawezi kumfikisha mahakamani kwa sababu Dr. Slaa hajaeleza chochote cha kumfanya JK alazimike kumfikisha mahakamani, Dr. Slaa ametoa loop hole ya JK kumpuuza na mwishowe kuonekana kama ni porojo tu kama zile za JK NDIYE MMILIKI WA DOWANS.

Hawezi Kumpuuza anajua Madhara ya Kumpuuza, CCM wamekosea Step sasa CDM watawamaliza
 
Nadhani Dr. Slaa anamaanisha hivi

Kwa kuwa CCM wanawaambia Watanzania kwamba MAGAMBA yao ni WATU WANAOTUHUMIWA KWA UFISADI ( Amabo list yao Ilianikwa na Dr. Slaa)na si MFUMO UNAOLEA UFISADI. Sasa ningependa kuwauliza CCM kwamba je Baada ya Siku Tisini MAGAMBA yafuatayo watayavua?

1. Jakaya Kiwete
2: Rostam Aziz
3. Edward Lowasa
4. Nazir Karamagi
5. Zakia Meghji
6. Anderw Chenge
7. Basil Mramba
8. Benjamin Mkapa
9. Yusuph Makamba
.
.
...
....
.......

Sio Vibaya tukiendelea kuwakumbuka akina Nape Magamba ya CCM ni yapi.
 
# 4 Dr Slaa ---Jizi namba moja.
# 5 Dr Mwakyembe ( Assistant jizi) namba moja kwa uwongo.....List iendelee............
 
Kwa mwendo huu mpya wa Slaa hata neno fisadi linakosa maana kabisa mkuu, ingawa ni hadithi nzuri kwa media, elewa kwamba wananchi sio wajinga na hizi siasa za kulipua mabomu hata kama hayapo haziwezi kuisaidia Chadema kwenda mbele.

Nakubaliana na wewe mkuu.

Kwa mtu anayemfahamu Mzee Mangula na hali yake ya kiuchumi atamshangaa sana Dr. Slaa kumtaja kama fisadi "nyangumi", naona sasa Dr.Slaa anatajataja tu majina kama wanamuziki wa Bongo Flavour.
 
Nakubaliana na wewe mkuu.

Kwa mtu anayemfahamu Mzee Mangula na hali yake ya kiuchumi atamshangaa sana kuwa jana Dr. Slaa amemtaja kama fisadi, naona sasa anatajataja majina tu kama wanamuziki wa Bongo Flavour mpaka itapoteza maana.

Fisadi si lazima awe Tajiri Mkuu, kuna watu waliiba Mali ya Uma lakini sasa Hivi ni Maskini wa Kutupa, kama Alishiriki kwa namna yeyote ile hata hakunufaika na Huo Ufisadi na yeye ni Fisadi tu
 
Hawezi Kumpuuza anajua Madhara ya Kumpuuza, CCM wamekosea Step sasa CDM watawamaliza

Atampuuza na katika hili zaidi ya Dr.Slaa kufanya kazi kwa niaba ya Rostam na Lowassa, hana atakacho-accomplish zaidi ya kupoteza credibility yake!!

Hivi sikuhizi Augustino Mrema akitangaza anakwenda kulipua mabomu kuna mtu anamchukulia serious?huku ndipo anapoelekea Dr.Slaa.

Alianza na JK Mmiliki wa Dowans and the list go on!!
 
Mkuu Waweza kuwa Hujui Lakini CCM wanajua na Linawaumiza. CCM walitaka Kuuaminisha uma kwamba Katika CCM tatizo ni la watu watatu tu, Hapa Dr. Slaa amekuwa very reactive na Kuikumbusha CCM kwamba Kama wao wanaamini kwamba Tatizo la CCM ni Watu waliotuhumiwa kwa Ufisadi kuna Orodha kubwa sana na Si Suala la wao CCM kukaa na Lowasa na Ku Compromise nao kwamba waachie Ngazi ili watangaze mafisadi wamejitoa.

Nasema tena Baada ya Siku tisini (90) ndio utajua Logic ya Slaa. Inabidi uwe Mtu wa Kufikiria nje ya Box ndio utajua Dr. Slaa (PhD) anamaanisha nini
 
- Hamna jipya hapa zaidi ya kwamba eti kwa vile CCM imewahi kupokea hela chafu basi viongozi wote wa CCm ni mafisadi ndipo ninapouliza zile hela za Chadema toka kwa Tony Blair alizopewa na Gadafi kumsafisha na yale mauaji ya wananchi wa marekani 350 kwenye ile ndege aliyoibomu kule Lockerbee, unasema ni safi? Sasa kwa vile Chadema wanazipokea zile hela unasema na wao wana damu ya wale wananchi 350 waliokufa kwa kuuliwa na Gadafi?

- It does not make a sense at all!

William @ NYC, USA.
Mkuu William, nadhani kufikia hapa, lazima tukubali yaishe, mimi binafsi nakubaliana na wewe, sio busara kumuita kila mwana CCM fisadi, simply because kuna wana CCM mafisadi ambao wameifisadisisha CCM
Mzee Malecela namfahamu kwa kina, at one time or another, nimetokea kusoma shule moja na wanae 4 at diferrent times tangu primary mpaka UD hivyo namfahamu at heart, sio fisadi, ila hawezi kukwepa collective resiponsibility kama ilivyo kwa mzazi kuwajibika kwa makosa ya mtoto wake.

NB. Nimefurahi kukuona ukirudi in full swing kwenye issue hii, nakuomba isiwe hii tuu, tuendeleze mapambano, safari bado ni ndefu. Pia tusiogope kutofautiana na marafiki zetu au hata kugombana kwa jambo ambalo mtakuja kupatana. Naamini Watanzania wote wenye nia njema na Taifa hili, wanauchukia ufisadi kwa dhati toka ndani ya mioyo yao, hivyo ukisikia wale tunaowaaminia nao kujumlishwa kwenye listi ya mafisadi, ni lazima tuwatetee kwa nguvu zetu zote!.

Pasco.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom