Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Naomba kujuzwa kiongozi gani wa Tanzania ambaye ni msafi?jana Slaa ametaja orodha mpya ya mafisadi ila nakumbuka kuna wakati fulani Slaa nae alishatajwa ktk kashfa ya ufisadi akiwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu,mbowe nae ameshalaumiwa ku2mia fedha za chama kwa matumizi yake binafsi,zitto nae ndo huyo anashutumiwa kila mara kuwa kambi ya mafisadi wa ccm

Je wewe una ufisadi gani
 
Huyo anae sema katoka dodoma sa 10 na kuwai mkutano asiwadanganye wana Jf,hakuna miundo mbinu inayo mruhusu kuwai hata angekua na gari ndogo inayo enda km300 kwa saa asingewai,dodoma tabora co kama dar moro istoshe uwanja wa ndege haufanyi kaz na hakuna helkopta iliyotua
 
Jamani orodha mpya ya mafisadi i wapi?

Mambo haya hapa yafuatilie kwenye Tanzania Daima .........................


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaja orodha mpya ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Vigogo hao ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, John Samwel Malecela, aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Philip Mangula, kwa kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu.

Dk. Slaa alitangaza majina hayo jana mjini Tabora alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Chipukizi.

Alisema majina hayo ni muendelezo wa yale ya vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi aliyoyataja Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambayo ni 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Katika orodha ya mwaka 2007, Dk. Slaa aliwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), ambaye sasa ni marehemu, Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM) na Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM).

Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, kada wa CCM, Nazir Karamagi, Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM), Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na Rais Jakaya Kikwete.

Alisema katika orodha hiyo mpya Magufuli amehusika na kashfa ya uuzaji wa nyumba za serikali ambazo ziliuzwa kwa watu wasiostahili na nyingine hazikutakiwa kuwekwa sokoni.

Alibainisha kuwa katika kashfa hiyo, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa naye alihusika kwenye uamuzi huo mbovu uliosimamiwa na Magufuli, ambaye hivi sasa amepewa Wizara ya Ujenzi.

Mangula na Malecela, alisema wao walikuwa wakitoa ‘vimemo’ vilivyokuwa vikitoa maagizo ya kwenda kuchotwa fedha za EPA ambazo zilikisaidia Chama Cha Mapinduzi katika kampeni zilizomuwezesha Rais Kikwete kuingia madarakani.

Alisema Mangula alikuwa akitumia kofia yake ya ukatibu mkuu wa chama na Malecela alikuwa akitumia wadhifa wa umakamu mwenyekiti wa Bara kwa wakati huo.

Aliongeza kuwa Sumaye naye alihusika kwa kuwa alikuwa waziri mkuu na alikuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea lakini aliamua kunyamaza kimya na kushirikiana na wabadhirifu hao.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa ametoa siku 90 kwa Rais Kikwete, kuueleza umma zilipo sh bilioni 70 zilizorejeshwa na wezi wa EPA.

Alisema Rais Kikwete aliahidi kuwa fedha hizo zitapelekwa katika Benki ya TIB, ambako kumeanzishwa dirisha la kuwakopesha wakulima.

Alibainisha kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), fedha hizo hazionekani zilipo kwa kuwa hakuna akaunti yoyote inayoonyesha zimewekwa.

Slaa, pia ametoa tuhuma kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kuna upotevu wa sh bilioni 220 kwa mujibu wa taarifa ya CAG.

Alisema mfanyabiashara mwenye malori kadi za magari yake zimekuwa zikishikiliwa na TRA kwa muda wa miaka 10 sasa na ameishitaki serikali na imeamriwa kumlipa kiasi hicho cha fedha.

“Sioni sababu ya serikali kulipa kiasi hicho cha fedha wakati aliyesababisha hasara hiyo yupo na bado anaendelea kufanya kazi TRA,” alisema.

Slaa alitumia fursa hiyo kumtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, asitumie nafasi ya uspika kama jukwaa la kisiasa kwa sababu yeye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema Makinda anatumia nafasi hiyo kuwa mwanasiasa badala ya kufanya kazi za uspika zilizoingiliana na kazi za siasa.

Slaa, ameahidi kuwa CHADEMA itazirudisha hoja zote za ufisadi kwenye mjadala ili zijadiliwe upya kwa kuwa Kikwete ameshindwa kuchukua hatua.

Naye Mwasheria wa CHADEMA, Mabere Marando, aliwataja wafanyakazi wawili wa kampuni ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM) ya Caspian Ltd, ambao walighushi majina yao na nyaraka ili kufanikisha wizi wa sh bilioni 40.

Wafanyakazi hao ni John Kato, ambaye alijulikana kwa jina la Kamando William, na Bharaeti Goda, alijulikana kwa jina la Francis William, waliofanikiwa kuiba kiasi hicho cha fedha kupita Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd.

Alisema anao ushahidi wa jambo hilo na yuko tayari kuisaidia serikali kama ikiwapeleka mahakamani wahusika.

Naye Fred Mpendazoe, alisema kilichofanywa na CCM kujidai kujivua gamba ni usanii mtupu, kwani katika uchaguzi mkuu uliopita Kikwete mwenyewe aliwanadi watuhumiwa wa ufisadi huku akiwasifu kuwa ni viongozi bora na hakuna kama hao.

“Kama alivyo kuhani kanisani ndivyo walivyo waumini wake na kama alivyo sheikh msikitini ndivyo walivyo waumini wake…Kikwete hawezi kutenganishwa na hao waliovuliwa gamba”, alisema Mpendazoe.
 
- Another genius now what this has anything to do na maneno ya leo ya Slaa kwamba Malecela ni mmoja wa mafisadi wa EPA meaning kwamba alisani makaratasi ya kuchukua hizo hela benki kuu au?

William @ NYC, USA.

ndio maana mzee aling'oa mabomba na koki zake kule mtela...........hili sitalisahau........na kwakuwa sasa hivi amewekwa kwenye list atuthibitishie kuwa hakuiba............

 
Inaonekana dhahiri kutokana na baadhi ya thread ninazoziona humu jamvini, mkakati wa CCM wa kujivua ghamba, ni pamoja na kulipa neno ufisadi maana pana zaidi, kwa kuhusisha rushwa ndogo, ili hatimaye vita hiyo ikose mwelekeo. Katika hali nawashauri CHADEMA kufanya haraka kuweka wazi vigezo wanavyovitumia katika kuainisha hiyo "LIST OF SHAME."
 
Slaa
S-shujaa l-lazima a-atimize a-ahadi naona yameanza kutimia
 
Anachoongea ni ch kweli, na ndio maana wanaotajwa hawathubutu kuinua midomo
 
tujikumbushe orodha ya 2007
1. Dr. Daudi t.s. Balali
2. Andrew j. Chenge
3. Basil pesambili mramba
4. Gray s. Mgonja
5. Patrick p.r rutabanzibwa
6. Nazir karamagi
7. Nimrod mkono
8. Rostam aziz
9. Edward lowassa
10. Benjamin w. Mkapa
11. Jakaya mrisho kikwete

tooobaaaaa...... Fwiiileeee
 
Huyo anae sema katoka dodoma sa 10 na kuwai mkutano asiwadanganye wana Jf,hakuna miundo mbinu inayo mruhusu kuwai hata angekua na gari ndogo inayo enda km300 kwa saa asingewai,dodoma tabora co kama dar moro istoshe uwanja wa ndege haufanyi kaz na hakuna helkopta iliyotua

Kaka pole na uchovu, niko Dodoma Sasa hivi namalizia shughuli zilizotuleta hapa na majira ya saa moja jioni nitakuwa Dar es salaam Naangalia mpira na kinywaji baridi kufurahia jinsi tulivyowapiga bao CDM na ilani yao ya UFISADI, sasa haina market tena na hii inatokana na kile tulicho kiona Tabora jana jioni.
 
Kama ni movie naona bado tupo kwenye trailer, orodha ya mafisadi ccm ni kubwa mno...watajivua sana magamba,mpaka watabaki skeleton tupu; kwishne.
 
Hivi mbona huyu dokta anajihamini sana?

Yaani lazima ajiamini. udr wake nii wa ukweli wala si wa kupewa, Ushahidi anao na ndo maana hawawezi kumpeleka mahakamani kwa kuogopa aibu sasa kwanini asijiamini?
 
Mafisadi aliyowataja Dr Wa ukweli ni wale nguli,bado wale wadodowadogo walokula vibilioni.CCM ni wachafu na wezi wakubwa hawaosheki.Kazi yetu ni moja tu wana-CDM,ni mapambano bila kuchoka na tushikamane kumtoa mwendawazimu chumbani asijekuwatwanga watoto nyundo na kuwauwa kabisa.Kazi mbele,ngoma juu,manyanga chini.Hakuna kulala twende mbeleeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!111
 
Safi daktari endelea kuwafunua mafisadi waliojificha ndani ya chama tawala najua magamba ndani ya chama tawala ni mengi na hayawezi kuisha wakisema wayamalize yote basi chama chote kitakufa.
 
Hao aliowataja kama mafisadi kwangu hapana, haijakaa vizuri kiuhalisia, naamini waliponzwa na uchumia tumbo wao tu, waliogopa kumwaga unga kwa kufukuzwa kwa kuwa kama mkubwa wao alikuwa ameamua wao wangefanya nini?.

Mangula yule mzee hana chochote cha kumfanya niamini ni fisadi,mali anazomiliki thamani yake ni sawa na jasho lake kwa muda wote aliokuwa mtumishi,ni mwaminifu sio mwizi, aliponzwa tu na system kwamba imeamuliwa hivyo na yeye akiwa ndio katibu mkuu akawa hana budi kuandika memo.

Magufuli naye suala la kuuza nyumba za serikali hakuamua yeye,bali alikuwa mtekelezaji tu kwa mujibu wa madaraka yake, kama baada ya kuwa imeamuliwa nyumba ziuzwe aliamua kumuuzia hawala yake,hilo ni suala dogo kwa kuwa hata kama asingemuuzia hawala yake nyumba ilishaamuliwa iuzwe tu na ingeuzwa.

Sumaye na Malecela nao hivyo hivyo, kosa lao lilikuwa kukosa ujasiri wa kupinga kuogopa kumwaga unga wao kwa kufuata kanuni ya collective responsibility.Tatizo letu tunawazia sana matumbo yetu kuliko maslahi ya taifa.

Kwa hiyo hawa kwa upande wangu naona sio mafisadi, kwa kuwa siamini kwamba katika fedha hizo walipata mgao hata wa senti moja.

Hao watu wote waliotajwa mali walizonazo ni za kawaida kabisa, ambazo naamini walizipata kwa haki kabisa kama kipato halali kwa muda waliokuwa kazini katika maisha yao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom