Tabia zipi huzipendi kwa ndugu yako, mpenzi wako, rafiki yako au hata mzazi wako?

Sipendi tabia ya kupangiwa cha kufanya yaani hapo naweza kuchukia hata sikunde haipiti..

Nishauri utakavyo lakini usinipangie cha kufanya simalizi sekunde nabadilika hapo hapo.

Shida mama zetu na wake zetu wana huu ugonjwa wa kumpangia mtu cha kufanya...

Naweza kuwa nimekaa zangu nasoma kitabu,utasikia mwanamke kwanini usile kwanza au ufanye kitu flani hlf ndo uendelee na unachokifanya basi namjibu tu nitafanya baadae saivi najisikia kufanya hivi sasa anarudia tena kauli ile ile hapo sasa anashangaa nimebadilika ghafla nimekuwa serious...

Mtu nikimwambia kitu kinaeleweka kbs hlf anajifanya haelewi aiseee hapo nachukiaga ghafla km nimeshikwa tako vile.Unakuta wife kapiga simu nikamwambia nipo kwenye kikao siwezi kuongea mda huu tuongee badae,mtu ananiambia tuongee hata dk tano namwambia haiwezekani ananiambia basi km huoni umuhimu aiseeeee hapo naweza kata simu.Napenda nikimwmabia mtu kitu km kinaeleweka ananielewe hapo hapo,alooo alooo nipo busy kidogo nitakupigia baadae,Sawa ukiwa free nipigie,sawa.
 
Dah Kuna ndugu yangu mmoja ye kazi yake kuuza mifugo ya home Kama ng'ombe, mbuzi lakini hakuna anachofanyia hizo fedha zaidi kuchezea ( sijui anachezeaje) coz wiki ndefu anabaki Mia Hana!
.. kinachoniuma ni kwamba hafikirii kwamba hatuipendi tabia yake..
Nb . Si mlevi Wala so mpenda wo wo wo
 
Bi mkubwa wangu anaongea mno yaan mnooo. Naweza kupata mgeni kama yupo nitajitahidi aondoke mahala hapo atuache wenyewe tu maana sio muda ataanza kuongea asivyooulizwa na nikimuambia anakuja juu nakua mdogo tu. Kiukweli huwa nakereka sana na tabia ya kuzoea zoea watu hovyo nayo nagombana nae lkn hasikii nimeona nimuache tu.
 
Bi mkubwa wangu anaongea mno yaan mnooo. Naweza kupata mgeni kama yupo nitajitahidi aondoke mahala hapo atuache wenyewe tu maana sio muda ataanza kuongea asivyooulizwa na nikimuambia anakuja juu nakua mdogo tu. Kiukweli huwa nakereka sana na tabia ya kuzoea zoea watu hovyo nayo nagombana nae lkn hasikii nimeona nimuache tu.
Nenda kapange
 
me pia Bi Mkubwa ana tabia hiyo, dawa yake ni kunyamaza kimya tu. Tena anaongeza na chumvi....yaan bi mkubwa angu akikusimulia kuhusu mimi lazima udate na nikikutana nae mbele ya mabest zake full ma-hug. Dah Bi mkubwa bhana
Tuwazoee tu mkuu mama zetu,maana wangu naye yuko hivyo hivyo letsay mmeongoza kwenda mahala,mkikutana na mtu anaanza kukutambulisha huyu ndo flani anaishi sehemu flani anafanya kazi flani yaani hawezi kusalimiana na mtu asikutambulishe mpaka unakoishi na mambo kibao,basi mi sipendi,napenda aseme tu huyu ni mwanangu kaja kunitembelea basi!!!!!vingine asubilie akiulizwa!!all in all nampenda sana na napenda kuongozana naye kila sehemu ninapokuwa nyumbani!!
 
Sipendi kelele iwe kutoka kwa Mama/ndugu

Sipendi kuambiwa nini cha Kufanya Katika maisha yangu

Sipendi tabia ya Dada angu fulani akikufanyia kitu mpaka atangaze..yani ana ile bila mimi kitu fulani kisingefanyika..bila Mimi fulani asingekuwa hivi.😏

Sipendi tabia ya marafiki wanaoniongelea vibaya iwe kwa mpenzi au watu wa karibu

Sipendi tabia za marafiki wanaojifanya wanamjua sana mwanaume wangu na kujichekesha chekesha ovyo..mfyuuuuu
 
Mtu kunichunia kisa tumegomana kumbe kimya kimya ananifatilia

Hii si kwa ndugu/wazazi/marafiki/mpenzi sipendi yani unagombana na mtu mnazinguana kabisa kila mtu na hamsini zake unaachana nae kbsa,unafanya yako lakini kumbe mwenzako anakufatilia kimya kimya.

unakutana na rafiki/ndugu yako mwingine kabisa ambae hamjagombana wala kuchuniana mnapiga story ktk story unamskia anakwambia jana nilikua na flani (anamtaja muhusika mliochuniana) alikua anakuulizia kweli yani kila nikiwa nae lazima akuulizie,inaonyesha anakufikiria sana yani.

unajiuliza kimoyo moyo huyu mtu kwanini aniulizie wakati haongei namimi,hatuwasilini mwaka sasa huwa nini kinamchokonoa kuniulizia na kunchimba chimba? hupati majibu.

next time unakaa na rafiki/ndugu ako mwingine kabisa nae anakwambia story zile zile kuhusu yule jamaa mliechuniana,huwa nakerekwaga kweli yani,mimi nataka ukinipotezea nipotezee mazima,sio unaniulizia ulizia kupitia watu huko,sipendi acha tu.
 
-Mimi sipendi rafiki kunipigia simu Hana cha maana cha kuongea
-Sipendi rafiki ambaye hajui privacy.ukiwa karibu na Mimi nikigundua wewe sio msiri hata kwa issue za kawaida tu,naweka distance kali
 
Huwa tunagombana sana na bi mkubwa wangu tabia yake ya kunipamba sana kwa rafiki/jamaa zake mtaani....ukimpa habari njema au taarifa ya mafanikio fulani uliyoyapata basi mtaa mzima utajua, tena hapo we haupo,.....siku unakuja kitaa unaanza kuhadithiwa, "nasikia umenunua kiwanja bwana, hongera Sana", imefikia stage sasa nikiwa na jambo langu napiga kimya tu.



Let's meet at the top, cheers
Ni afadhali hata wewe si mwingine mwanaye a maendeleo yake ananuna antakà amfanyie yeye ila yeye aendelee kudanga kwenye vyumba vyakupanga kila kukicha?
 
Back
Top Bottom