Tabia za mwanaume akiwa na pesa

Tabia za mwanaume akiwa na pesa

Tabia haina pesa wala umaskini! Hizo tabia anaweza kuwa nazo mtu yeyote yule.
Na malezi huwa yanachangia sana kwa kiasi fulani
endelea kuizarau misemo ya wahenga

"pata hela tujue tabia yako"
 
Yap mamaa.najua umenipendea hela zangu.
Nisingekuwa na hela usingenipenda.
Kiukweli naringa siku hizi.
Maana hata wao waliniringia.tena Nina wanyanyasa kweli kweli.naweza nisimtafute siku nzima..najua atanitafuta tu.si ana shida.
Teh
 
Labda unazungumzia wahaya wasukuma waruguru na wachaga ndo tabia zao
hela hainaga kabila.

anaweza kuwa mchaga ila aliye zaliwana kukulia kwa wanyaturu.
 
Wanaume wachache wenye nazo halafu akawa na masimango lkn sisi sasa tupate hizo ngawila uone nyodo zake
Bidada nawe mhenga kama mimi nini....kuna neno hapo umelichomekea si la kizazi hiki
 
Me nnavozidi kufanikiwa ndo nazid kuwa kinyume na hizo sifa!
 
Tupashe habari... Ilikuwa gari ya aina gani hii yenye thamani kuliko mkewe???!!!
Peugeot 504
30571405_1921232291229936_7643356381583507456_n.jpg
 
Nawasalimu all MMU

Leo naomba nidondoshe hii habari kidogo, wanawake pia mwakaribishwa kuongezea baadhi ya tabia za wanaume wachache wakiwaga na hela

1) Yeye sio mkosaji: Hapa nazungumzia kupatikana na hatia. Yaani kama kakukosea lazima atengeneze maelezo mengi mpaka akuset ujione wewe ndie uliyekosea kumbe ni yeye.

2) Hajui kuomba/kutamka SAMAHANI: Hapa hata kama kakukosea kamwe samahani hajaumbiwa kinywani mwake.

3) Hujikweza: Hapa utakuta kila mwenzie au jirani yake akifanya jambo zuri utasikia yeye anaona kama hamna kitu.

4) Ujuaji: Hapa atataka kuonesha umwamba wa kila kitu kwamba anakijua. Mfano unakuta ye ni daktari basi akifika kwa mjenzi atampelekesha kiudaktari na wakati professional ya udaktari haiingiliani na ujenzi.

5) Kiburi: Hapa huwa hasikilizi ushauri haambiwi haambiliki anaweza akanya mlangoni kwako ukimuuliza utasikia inagharimu kiasi gani kwani? Badala hata atoe excuse.

6) Sifa: Hapa akitoa hela ndani atatangaza ukoo mzima hadi wale marafiki wa utotoni wajue au akisikia michango utaona atatoa kiwango kikubwa tofauti nakilichopangwa ili aonekane zimo.

7) Wanamsahau Allah /Mungu: Hapa ibada kwao ni mwiko siku ya Ijumaa ni siku ya kununulia bia wanaita weekend mood. Wale wa Jumapili utasikia ndio nafua.

8)----------
9)--------
10------

Nawakaribisha mmalizie sifa za wanaume baadhi wakipata hela za ghafla..
Izo n tabia kama pesa umeikutia uzeen
 
Tatizo mna inferiority complex mtu akiwa amekuzidi mafanikio kidogo tu kila anachofanya mnasema dharau. Akicheka ooh anacheka kwa dharau...asipocheka anajiona sana huyu hacheki na watu
 
Kuna baadhi ya wanawake waliwavumilia wanaume wao kwa upendo na kuwaheshimu lkn wanaume wao hawakuwatendea haki (Hapa hata mm nalaumu)
Kuna baadhi waliowavumilia wanaume wao kwa kuwasingamana, kuwadharau na kejeli kiasi kwamba mpaka iliwasababishia wanaume kuwa na mawazo. Hapa mwanaume akipata utashangaa anaoa mke mwingine anahama kwako kbsa. Kuna wakati unamvumilia mwanamke jeuri, kiburi na msaliti kwasbb hauna pesa za kutosha kipindi hicho sasa ukipata. Hakuna kugeuka nyuma.
N.B
Kama mwanamke alikuvumilia kwa upendo wa dhati na uaminifu na siku ukipata fedha ukamuacha hautafika popote. Fedha zitaaisha bila ww kujua zimeenda wapi.
Yaani ipo sana jamani badala ya kufaidi wote utasikia usinipangie chagua kuondoka au kuwa na mkemwenza, mpaka mtu kaongeza mwingine basi hapo uliepo hautoshi ndiyo maana yake, ila machozi ya huyo mvumilivu hayaendagi bure
 
Yani mkuu hapo 1,2, 5 in Mr wangu kabisaa yeye huwa hakosi na hajui kuomba msamaha,,tena hyo kwani ina cost shngapi kuna Siku hadi nilimtandika Kofi kwa hasira nyoko zake
 
Back
Top Bottom