Tabia za mwanaume akiwa na pesa

Tabia za mwanaume akiwa na pesa

Huyo atakua na pesa ya mbuzi! Mwenye Pesa ya uhakika mara nyingi sio watu wa kujikweza

We jamaa weweeee, una akili sana. Japo sio wote lakini watu wengi niliokutana nao wenye pesa zao, hawajikwezi. Vilevile wasomi wengi wa waliosoma kwelikweli, hawana madharau. Wale watu walioonja kidogo harufu ya pesa au shule kwa mbaali ndio wanaotusumbua.
 
Nawasalimu all MMU

Leo naomba nidondoshe hii habari kidogo, wanawake pia mwakaribishwa kuongezea baadhi ya tabia za wanaume wachache wakiwaga na hela

1) Yeye sio mkosaji: Hapa nazungumzia kupatikana na hatia. Yaani kama kakukosea lazima atengeneze maelezo mengi mpaka akuset ujione wewe ndie uliyekosea kumbe ni yeye.

2) Hajui kuomba/kutamka SAMAHANI: Hapa hata kama kakukosea kamwe samahani hajaumbiwa kinywani mwake.

3) Hujikweza: Hapa utakuta kila mwenzie au jirani yake akifanya jambo zuri utasikia yeye anaona kama hamna kitu.

4) Ujuaji: Hapa atataka kuonesha umwamba wa kila kitu kwamba anakijua. Mfano unakuta ye ni daktari basi akifika kwa mjenzi atampelekesha kiudaktari na wakati professional ya udaktari haiingiliani na ujenzi.

5) Kiburi: Hapa huwa hasikilizi ushauri haambiwi haambiliki anaweza akanya mlangoni kwako ukimuuliza utasikia inagharimu kiasi gani kwani? Badala hata atoe excuse.

6) Sifa: Hapa akitoa hela ndani atatangaza ukoo mzima hadi wale marafiki wa utotoni wajue au akisikia michango utaona atatoa kiwango kikubwa tofauti nakilichopangwa ili aonekane zimo.

7) Wanamsahau Allah /Mungu: Hapa ibada kwao ni mwiko siku ya Ijumaa ni siku ya kununulia bia wanaita weekend mood. Wale wa Jumapili utasikia ndio nafua.

8)----------
9)--------
10------

Nawakaribisha mmalizie sifa za wanaume baadhi wakipata hela za ghafla..
Acha kutulinganisha Na Bwana wako
 
Kuwa na pesa ndio kiwa na shilingi ngapi?? Maana kwa tabia ulizotaja hapo kuna watu ni maskini tu ila ndio tabia zao
 
Back
Top Bottom