Nampenda lakini ana tabia za uswahili uliopitiliza. Nifanye nini kumbadilisha?

King Loto

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,573
1,344
Hey! Wakuu wajukwaa hili naamini bado hamjakata tamaa kwenye lolote na bado mapambano mpaka dakika ya 90.

Basi wakuu katika pitapita nikakutana na mtoto mmoja kaloweya Dodoma, sema kwao Handeni, malezi yake kapewa na mama wote wazigua, mtoto anaitwa Hamida, anyway nisitoe utambulisho wote.

Lakini kiufupi nimemuelewa ila mimi sijazoea uswahili wake anaoniletea wakuomba omba kila dakika yaani najisemea mbona ana kuwa na njaa njaa kwani kwao wana dhiki sana, mi mwenyewe nina uswahili lakini wake umezidi.

Mara utasikia viatu, mara nywele zimefumuka, mara hospitali hapa pahospitali ndio kila saa aiseee, mara nimuite aje na rafiki yake eti tuna part tununulie madela, vyote hivyo nampa maana nimemuelewa sana.

Sema huyu mtoto ni muongo pia, afu uswahili mwingi, sijui kaniona mi danga na ujana wangu bado naonekana danga, yaani aisee hata kama anaujua mchezo,

Tabia nyingine mbovu kabisa ni kuropoka ropoka ovyo tena ukute mpo wote mbele za watu, mtoto ana mdomo, lakini anyway sifa ya mwanamke.

Sasa ananiambia anahisi ana mimba tena yang, sema uswahili wake umenishinda wakuu, ana vituko vingi kuliko maelezo, vingine siwezi andika hapa nikamaliza.

Yaani wakuu kila nikiwaza nimbadili hivi kwa kuongea au kumwelekeza unakuta hakusikilizi asharukia maelezo mengine, unakuta unamwambia labda "Hamida naomba unipe lisaa mi na wewe kuna jambo nataka tuongee" utasikia kaleta maneno au anachat yaani hasikilizi.

Natamani angekuwa angalau mstaarabu ninge enjoy kuexchange mengi, huyu mtoto anajua kinoma kwenye 6 kwa 6 afu show yake siyo ya kitoto unavotaka anakupa hapo amna shaka kwangu, mathalani naridhika ila ustaarabu ndio ivoo tena au kisa hana hizi shule za magharibi walizoenda dada zetu. She isn't such an educated, japo siangalii hilo.

Mtu wa hivi nambadili vipi wakuu maana nampenda sana.
 
huenda hata hiyo mimba hana
Ndio nahisi hana mimba, maana nikujisikia vibaya tu nami nimerekodi tarehe kabisa ili akileta mjadala namark tu, kiufupi mimi kusingiziwa mtoto ni uongo na pia sikatai mtoto, wanawake wote sawa tu akili zao zile zile, wanatofauti ndogo, so ukiwa mwanaume kweli kuna wanawake hawaongei labda upate hawa wadada zangu wakichagga lakini hata hawa ivo ivo.
 
Yani wewe utakuja kuumia sana. Unalowaza wewe siyo analowaza mwenzio kwake we danga tu
 
Niliwahi pata mwanamke wa aina hiyo miaka ya nyuma, ilikuwa yeye na hela hela na na yeye, usipompa analalama simpendi, akija gheto akiona hela akili yake inahama, nilikuwa namuelewa sana..

Kuna mtu akanishauri eti kama nampenda nimbadilishe, ha ha kosa likawa hapo..wanawake hawapendi kusikia ukweli aisee, yule dada baada ya kumuelekeza utumbo wake aligeuka mbogo sana, na mapenzi yalifia hapo.

Kifupi hapo huna mwanamke, kusema utambadilisha sio kweli utajidanganya!
 
Navunga tu na kumpotezea, sema kumukomoa nikutoka na mwingine afu ajue ana wivu huyu mwanamke acha tu
 
Mzoee tu,na hapo kashawaambia Hadi shoga zake kwamba,kapata bwana na akiomba kitu anatekelezewa fasta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom